Mwanafunzi China auwawa kwa kuchomwa kisu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi China auwawa kwa kuchomwa kisu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by engmtolera, Jan 13, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  NDUGU wana Jf,habari
  napenda niwape habari iliyotokea saa moja lililopita,kuwa hapa china Yangling katika chuo nisomacho NORTHWEST A&F UNIVERSITY mwanafunzi kutoka Bangradeshi ameuwauwa na raia wa kichina kwa kuchomwa kisu,mwanafunzi huyo ameuwawa chumbani kwake bwenini wakati akiwa anajiandaa na mtihani kesho,Ndugu wana jf tupo ktk mazingira magumu kwani watanzania hapa tupo wawili mmoja anatokea Moshi na mimi natokea Morogoro,hivyo tunaomba mjue kuwa chochote chaweza tokea kwa sisi ndugu zenu tulio hapa china
  hii ni taarifa tu nawaomba wapeni taarifa na ndugu zetu walio china ktk vyuo vingine wajihadhari na hili


  mapinduzi daimaaaaaa
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Poleni sana. Muwe waangalifu na epukeni mambo yanayoweza kuwaweka katika mgongano na wenyeji wenu.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Thadharini na wabangaladeshi na watu kutoka maeneo ya Pakistani hao ni kama hawana akili vizuri ,wao ni hasira tu na hawachagui cha kukupiga kama ni kisu au shoka chochote kilichopo karibu basi kwake ni silaha ya maangamizi,na zaidi hawajui au hawana time ya kupigana kwa ngumi sijui urushe kichwa ,wao ni watu wa kutumia njia za mkato kumaliza mapigano au ugonvi ,kesi baadae maana hawajali kufa kutokana na shida za nchini kwao. Na wengine wasomali maana hawa ukimtizama tu na akikushitukia kama unamdeku basi ujue ni vita na maswali kibao. Hao wachina sio watu wa ugonvi lazima kutakuwa na jambo tu,sasa huko imekuwa kuviziana ,hebu tafuta sababu tuone.
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Poleni sana ila kwa experience ya nje ya nchi nakushauri kama alivyokushauri Jasusi kuwa muwe waangalifu na wenyeji mara nyingi ni wivu, tabia na visasi kwa unavyojua culture za nchi zinatofautiana sana kwako jambo unaweza kuliona dogo kumbe ni tusi kwao. Pia kama kumetokea hivyo ni bora kama mnatoka chuo muwe pamoja maana inasaidia saa zengine.
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Muwe waangalifu, especially na mabinti wa huko..
  Tumepoteza wengi e.g. kule Urusi kutokana na wivu wa kimapenzi wanaokuwanao wenyeji
   
 6. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  mbona hukutueleza chanzo cha mauaji hayo ni nini? Kindly do some investigation a bit ili utujuze
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Watanzania always ni wapole sana hutasikia mwanafunzi yeyote wa kigeni ameuawa hapa Tanzania iwe kwa wivu wa kimapenzi wala mambo mengine may be iwe bahati mbaya sana ila kweli kwa wenzetu nchi hasa za westers europe na Asia hawapendi kabisa wageni jitahidini sana muwe mnachukua tahadhari mara zote hasa kwenye madisco,clubs na kutembea usiku pia kutembea mchana pekeyenu!muwe macho na hilo!ila sasa nashangaa tukio hili mtu kafuatwa chumbani ni hostel au alikua anaishi mtaani
   
 8. D

  DOCTORMO Member

  #8
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  napenda kutoa taarifa kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia kama ifuatavyo:
  wasifu wa jamaa alikuwa ni mwanafunzi wa Phd. na alikuwa nimpole naasiye na maneno mengi sana pindi uongeapo na mtu mwenyekujali muda wake na masomo. siku ya tukio inasemekana alikuwa chumbani kwake na huyo muuaji wa kichina alikuwa akipita na kugonga gonga milango ili afunguliwe, lakini alipofika mlango wa mwisho kwenye chumba cha mwsho cha mrehemu alivunja mlango na kuingia. Marehemu aliyekuwa anaishi gorofa inavyoonekana alifanikiwa kumkimbia muuaji(mchina) na kukimbilia gorofa ya 3 akiomba msaada huku akikimbizwa na huyo mtoaroho(mchina). Bahati yake ilikuwa mbaya kwani hakukua na watu imara wakuweza kuzuia tukio hilo kutokana na muuwaji kuwa na kisu nakuanza kumshambulia mbaghaladeshi wa watu mpaka kumuua. Kisha mchina huyo alisikika akisema 我杀了他
  (l killed him) na kama unaweza njoo na wewe nikuuwe alisikika hivyo.
  Baada ya tukio hilo ilichukua muda wa 30min kwa wahusika police kufika eneo la tukio bila ya ambulance kwaajili ya kumchukuwa mtu huyo kwenda huspitali kwasababu tulihisi kama angekuwa bado anauzima, lakini ilichukuwa kama muda wa masaa matatu nakuona mwili ikitole na police ukiwa umefunikwa nakutoweka nao kwaharaka kwenda kuhifadhiwa hospital.
  Hii ndiyo taarifa ya private intelligence agent(me)
   
 9. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mimi nimeshawaasa sana waafrika wenzangu kuhusu hili, waache kutembea ovyo kwenye maclub na sehemu zote za starehe na mazingira hatarishi. Waafrika wengi wamekufa kutokana na ajali au kama yalivyomkuta huyo jamaa, polisi wa nje wakisikia ni muafrika basi watakuja baada ya 30 mins which is too late.. na ukifika hospital ktk nchi za far east nyingi wakiona muafrika wanakunyanyapaa mpk unakufa. Wengi wamepotea kwa njia hizi yani hata kama una hela hazikusaidii
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,894
  Trophy Points: 280
  waafrika wanaitwa manyani.
   
 11. p

  p53 JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hujasema bado,sababu hasa ni ipi iliyomfanya huyo mchina kuua?kujua chanzo cha ugomvi wao ndiyo muhimu ili iwe fundisho kwenu mnaoishi huko china na hata nchi nyingine pia
   
 12. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,935
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  Xiongdi bui bu qi ...
   
 13. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  POLENI sana ndugu zetu, chukueni tahadhali. Huyo muuaji ni mwanafunzi mwenzenu na je kesha kamatwa, au kaishia ki namna?
   
 14. D

  DOCTORMO Member

  #14
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  alisubiri aje kukamatwa na alikamatwa, akipelekwa huku akilia, sijui kilichoendelea tena. lakini nahisi, atafikishwa kunakoshahili na hatimaye kunyongwa. mwiho wa kuwasilisha
   
 15. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Tumekuwa tukisikia katika vyombo vya habari Wachina wakiua watu bila sababu huko China. Tumesikia wakati fulani mmoja alivamia sule ya chekechekea na kuanza kuchama watoto visu. Nadhani waningiwa na ukichaa fulani hivi.
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,069
  Trophy Points: 280
  ..poleni sana.
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hii habari tija yake ni nini? mbangladeshe na watanzania wawili katika hicho chuo nk? then! alafu ipo Jukwaa la Siasa?! Moderators mnakula karanga na watoto wa mtendeni tu au mko nyuma ya pazia!
   
 18. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  ni mbwembwe tu za mtoa mada.
  Poleni sana jamani.
  Huyo mchina amechukuliwa hatua gani?
   
 19. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Poleni wote mlioguswa na msiba huo.

  Ni taarifa ya kusikitisha,
  Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la mauaji kwa kutumia visu,unaona mtu ameejichokea maisha anakwenda shule ya chekechea kuua watoto,inatisha mno. Mbali na wivu wa kimapenzi wachina hawajatulia kabisa kiakili.

  Jambo jingine la kushangaza ni kuwa hata ikitokea ajali,hawa wenzetu hawako sharp kusaidia majeruhi,watawaacha hapo mpaka polisi waje,na hata polisi wakija watafanya taratibu zao za kipolisi halafu ndo wanawapeleka hospitali.Kama ni maiti zitakaa hapo bila kufunikwa hata kama ni masaa kadhaa,hali hii inashangaza sana,nilisha wahi shuhudia mtu amegongwa anamaumivu lakini watu wanamuangalia tu,eti wanasubiri polisi.Inaudhi.
   
 20. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Poleni/inasikitisha sana. Kumbe ni kweli huko China wananyongwa papo kwa papo? Nasikia hata dreva akigonga na kuua kwa bahati mbaya?
   
Loading...