Mwanafunzi azimia baada ya kupata div 0 matokeo ya form four 2011

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,643
68,592
MWANAFUNZI aliyekuwa kidato cha nne Shule ya Sekondari Morogoro inayomilikiwa na serikali, Sikuzani Kibwana, leo ameanguka ghafla na kupoteza fahamu katika chumba cha Intanet baada ya kusoma matokeo na kujikuta amefanya vibaya kwenye mtihani huo ambapo alioongozana nao wote wakiwa wamefanya vizuri.
Mwandishi wetu alishuhudia tukio hilo kwenye chumba cha Intanet cha Valentenes karibu na Uwanja wa Jamhuri katika Manispaa ya Morogoro ambapo wanafunzi wa shule mbali mbali walikuwa bize kuangalia matokeo ya kidato cha nne mwaka 2011 yaliobandikwa jana kwenye mtandao na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
Mwanafunzi huyo alianguka na kupoteza fahamu na kuzua taharuki kubwa kwa watu wote waliokuwemo ndani ya chumba hicho.
Wanafunzi wenzake walimtoa nje ili apigwe ubaridi na kuwapigia simu wazazi wake.
Hadi mtandao huu unaondoka hapo, mwanafunzi huyo alikuwa bado hajazinduka.

NECTA:: http://196.44.162.14/necta2011/CSEE 2011/s0332.htm

Sikudhani Kibwana-Zero ya 34

SOS:GPL
 
Jana wamezimia wengi sana,mi nimeshuhudia! Wako bize na mambo yasio na maendeleo, utakuta mtu kwao kuna tv lakini kutwa anaangalia bongofleva na movie za ki Nigeria badala kuangalia Cnn, Bbc, voa, majarida mbalimbali,wapi! Wako juu juu tu!
 
Je Baba na Mama wanaangalia hiyo CNN BBC VOA na kusoma vitabu mbalimbali??
 
Da ina maana alivyofanya mtihani yeye alijitathmini vipi?
 
Watoto hawajishughulishi lakini wanavyopenda mafanikio,
utakuta siku za mitihani wanadanganyana na feki
 
Mbona shule za Kiislam wamezoea Zero na four lakini wako n furaha tu!
 
Jina tu SIKUDHANI tayari nimepata jawabu la kwanini kapata zero!Ni kwasababu HAKUDHANI kuwa atafeli japo hakujiandaa vizuri na mtihani!!Ha ha haaa!!!Pole sana mdogo wangu wewe mtoto wa kike heri yako waweza olewa vidume vilivyozungusha sijui itakuwaje?
 
Da ina maana alivyofanya mtihani yeye alijitathmini vipi?
wengi ni wazembe sana, mwanafunzi hata kwa kuongea naye tu unagundua ana ufahamu wa chini kabisa, ila anapofanya mtihani anatarajia miujiza... anaota I wakati hata knowlege ya IV hana. its just crazy...
 
Jana wamezimia wengi sana,mi nimeshuhudia! Wako bize na mambo yasio na maendeleo, utakuta mtu kwao kuna tv lakini kutwa anaangalia bongofleva na movie za ki Nigeria badala kuangalia Cnn, Bbc, voa, majarida mbalimbali,wapi! Wako juu juu tu!
hii bongofleva italeta balaa kweli!Hadi wanaandika kwenye mtihani?
 
nampa pole asikate tamaaa na akasome certificate chuo cha ifm,cbe,mzumbe aje diploma akimaliza atakuja bachelor degree
 
Back
Top Bottom