Mwanafunzi atangaza kuwania nafasi ya Spika wa Bunge

Dr wa Kaliua

JF-Expert Member
Sep 20, 2020
1,636
3,808
Mwanafunzi wa chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere MNMA, Amos sollo(26)

amejitokeza kuchukua form ya kuwania Nafasi ya spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa TANZANIA.

Amos sollo, amefika ofisi ndogo ya chama Cha mapinduzi CCM.

Zilizopo mtaa wa Lumumba jijini dar es salaam..

Nini maoni yako??? Ni nguvu ya ukomavu wa Umoja wa vijana wa CCM(uvccm)
IMG_20220112_161924.jpg

===
Wakati hatua ya uchukuaji fomu za kuomba uteuzi wa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania ikiwa imeingia siku ya tatu, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Amos Sollo (26) ajitokeza kuitaka nafasi hiyo.

Sollo amefika katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo Jumatano Januari 12, 2022.

Akizungumza na Mwananchi baada ya kutoka katika ofisi hizo, Sollo amesema yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni hapo akisomea shahada ya uchumi na maendeleo na amefika ofisini hapo kujua utaratibu wa kupata fomu ukoje na kuambiwa kuwa gharama ni Sh1 milioni.

"Niliamua kufika hapa ofisi za chama kujua utaratibu wa kupata fomu ili nami nitie nia ya kugombea uspikana ndipo nikaambiwa ni Sh1 milioni.

" Lakini mpaka sasa nina Sh300,000 ambapo Sh100,000 nikiwa nayo taslimu na Sh200,000 ikiwa benki, hivyo naenda kuomba kwa wadau wengine wanichangie ili itimie niweze kuchukua fomu kwa kuwa nia na sifa ninazo za kukalia kiti hicho cha uspika na vijana tunaweza," amesema Sollo.

Akielezea uzoefu wake katika uongozi, amesema ameshawahi kuwa Mbunge Wizara ya Uchumi katika chuo hicho na pia amewahi kutia nia nafasi ya urais akiwa chuo cha Maswa na hivi karibuni kastafu Uenyekiti wa chama cha Wanafunzi wanaosomea uchumi chuoni hapo.
 
Dogo wakati mwingine wakishinda kutoa maneno ya dhihaka tayari ameshaonekana na atafika mbali.
 
Mwanafunzi wa chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere MNMA, Amos sollo(26)

amejitokeza kuchukua form ya kuwania Nafasi ya spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa TANZANIA.

Amos sollo, amefika ofisi ndogo ya chama Cha mapinduzi CCM.

Zilizopo mtaa wa Lumumba jijini dar es salaam..

Nini maoni yako??? Ni nguvu ya ukomavu wa Umoja wa vijana wa CCM(uvccm)
View attachment 2078284

Huko bado sana, walau afike umri wa 50
 
Vijana wengi wa elimu ya juu wanajihusha na CCM huwa wanaongozwa na tamaa, ubinafsi, na kujipendekeza ili watambuliwe na kufikiriwa kwenye teuzi mbalimbali.

Vv
Ujue kwa namna fulani hiyo ni sawa na interview and business process ya aina yoyote. Bila networking, connections, strategic plans, referees, initiatives, intelligence, humility na KUJITOSA KIAINA, aiseeeeeeeeeeeeeeeeeeee utaishia kutusoma wenzio magazetini na kututazama ITV na Channel 10.
 
Mwanafunzi wa chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere MNMA, Amos sollo(26)

amejitokeza kuchukua form ya kuwania Nafasi ya spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa TANZANIA.

Amos sollo, amefika ofisi ndogo ya chama Cha mapinduzi CCM.

Zilizopo mtaa wa Lumumba jijini dar es salaam..

Nini maoni yako??? Ni nguvu ya ukomavu wa Umoja wa vijana wa CCM(uvccm)
View attachment 2078284

Mkuu,,kijana ana ulemavu wa mguu nini?? Mguu wa left nauona hauko sawa au macho yangu
 
Back
Top Bottom