Mwanafunzi atangaza kuwania nafasi ya Spika wa Bunge

Mwanafunzi wa chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere MNMA, Amos sollo(26)

amejitokeza kuchukua form ya kuwania Nafasi ya spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa TANZANIA.

Amos sollo, amefika ofisi ndogo ya chama Cha mapinduzi CCM.

Zilizopo mtaa wa Lumumba jijini dar es salaam..

Nini maoni yako??? Ni nguvu ya ukomavu wa Umoja wa vijana wa CCM(uvccm)
View attachment 2078284

===
Wakati hatua ya uchukuaji fomu za kuomba uteuzi wa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania ikiwa imeingia siku ya tatu, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Amos Sollo (26) ajitokeza kuitaka nafasi hiyo.

Sollo amefika katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo Jumatano Januari 12, 2022.

Akizungumza na Mwananchi baada ya kutoka katika ofisi hizo, Sollo amesema yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni hapo akisomea shahada ya uchumi na maendeleo na amefika ofisini hapo kujua utaratibu wa kupata fomu ukoje na kuambiwa kuwa gharama ni Sh1 milioni.

"Niliamua kufika hapa ofisi za chama kujua utaratibu wa kupata fomu ili nami nitie nia ya kugombea uspikana ndipo nikaambiwa ni Sh1 milioni.

" Lakini mpaka sasa nina Sh300,000 ambapo Sh100,000 nikiwa nayo taslimu na Sh200,000 ikiwa benki, hivyo naenda kuomba kwa wadau wengine wanichangie ili itimie niweze kuchukua fomu kwa kuwa nia na sifa ninazo za kukalia kiti hicho cha uspika na vijana tunaweza," amesema Sollo.

Akielezea uzoefu wake katika uongozi, amesema ameshawahi kuwa Mbunge Wizara ya Uchumi katika chuo hicho na pia amewahi kutia nia nafasi ya urais akiwa chuo cha Maswa na hivi karibuni kastafu Uenyekiti wa chama cha Wanafunzi wanaosomea uchumi chuoni hapo.
Ni Haki yake kikatiba.
 
Anhaa! Kuhusu pesa...IPO hivi.. alienda kwa lengo la kujua gharama za kuchukua form! Ila. Baada ya kuambiwa Ni 1m akawa katoka Sasa sijui kesho ataifata hiyo form au ndio Basi tena
Ok. Lakini mkuu taifa linashida sana sababu vijana wengi wanawaza kiki za uteuzi tu. Hakika hatutakuwa nauwezo wa kuhoji mambo kabisa. Wote tutakuwa nahofu ya kukosa uteuzi.
 
Hongera zake huyu kijana ana udhubutu na jasiri kuliko wanaotukana humu JF.
Yaani hawa wenye negativity juu ya huyu kijana wanajionyesha wazi jinsi nafsi zao zisivyojiamini, na zilivyokosa uthubutu katika maisha. Watu wa namna hii wakikutana na changamoto kidogo tu wanasema "Yote namwachia Mungu" wakati Mungu alishakupa power nadni yako ni wewe tu kuamua uitumie vipi hiyo nguvu. Huyu kijana ni wa kupongeza siyo kubeza hata kidogo na ni haki yake kikatiba kama anakidhi vigezo vyote. Akina Dimond na wengine waliofanikiwa katika music wangeogopa kwamba kuna magwiji kama Profesa J. n.k wasingefika hapo walipo leo. Na isitoshe safari moja uanzisha nyingine. KUJIAMINI, KUTHUBUTU NA KUJARIBU HAKUJAHI KUWA KOSA BALI KUKATA TAMAA, KUTOJIAMINI NA KUTOKUTHUBUTU NDIO KOSA KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA.
 
Wengi hawajiamini na watakuwa pia wanafeli kwenye maisha, kijana kaamua kujaribu na huo ni udhubutu
 
Mpumbavu tu huyo.
Msomi anaonesha upumbavu wake nje nje.Nchi ina vijana wa hovyo sana.
Amekuzidi kete.
====
Kijana amefanyia kazi wazo na ushauri wa Mama, kuwa vijana wazione furusa na kuzifanyia kazi. Hivyo wasiendelee kuwa ngazi kwa wengine.

Hongera sana Amos Sollo kwa kuiona furusa, achana na wale ambao hawataki kuziona furusa.
 
IKIWA hatua ya uchukuaji fomu za kuomba uteuzi wa kikiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania ikiwa imeingia siku ya tatu, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Amos Sollo (26) ajitokeza kuitaka nafasi hiyo.

Sollo amefika katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo Jumatano Januari 12, 2022.
Akizungumza na Mwananchi baada ya kutoka katika ofisi hizo, Sollo amesema yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni hapo akisomea shahada ya uchumi na maendeleo na amefika ofisini hapo kujua utaratibu wa kupata fomu ukoje na kuambiwa kuwa gharama ni Sh1 milioni.

“Niliamua kufika hapa ofisi za chama kujua utaratibu wa kupata fomu ili nami nitie nia ya kugombea uspikana ndipo nikaambiwa ni Sh1 milioni.

“Lakini mpaka sasa nina Sh300,000 ambapo Sh100,000 nikiwa nayo taslimu na Sh200,000 ikiwa benki, hivyo naenda kuomba kwa wadau wengine wanichangie ili itimie niweze kuchukua fomu kwa kuwa nia na sifa ninazo za kukalia kiti hicho cha uspika na vijana tunaweza,” amesema Sollo.

Akielezea uzoefu wake katika uongozi, amesema ameshawahi kuwa Mbunge Wizara ya Uchumi katika chuo hicho na pia amewahi kutia nia nafasi ya urais akiwa chuo cha Maswa na hivi karibuni kastafu Uenyekiti wa chama cha Wanafunzi wanaosomea uchumi chuoni hapo.
 
Mpumbavu tu huyo.
Msomi anaonesha upumbavu wake nje nje.Nchi ina vijana wa hovyo sana.
Nikusihi sana jitahidi uwe na moyo wenye uvumilivu na ulojaa hekima. Kijana huyu amekosea wapi? Ni haki yako pia kikatiba kwenda kuchukua fomu. Unadhani viongozi kama JK, BWM na wengineo wengi walianzaanzaje hadi kufika hapo? Hata mti haunzi tu hivi hivi....una hatua zake za ukuaji. Hivyo, hiki kilichofanyika ni sehemu ya ukuaji na ukomavu katika siasa. Hongera mwanafunzi umeamua kuitendea haki eleimu yako ya uraia.
 
Mwanafunzi wa chuo Cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere MNMA, Amos sollo(26)

amejitokeza kuchukua form ya kuwania Nafasi ya spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa TANZANIA.

Amos sollo, amefika ofisi ndogo ya chama Cha mapinduzi CCM.

Zilizopo mtaa wa Lumumba jijini dar es salaam..

Nini maoni yako??? Ni nguvu ya ukomavu wa Umoja wa vijana wa CCM(uvccm)
View attachment 2078284

===
Wakati hatua ya uchukuaji fomu za kuomba uteuzi wa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania ikiwa imeingia siku ya tatu, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Amos Sollo (26) ajitokeza kuitaka nafasi hiyo.

Sollo amefika katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo Jumatano Januari 12, 2022.

Akizungumza na Mwananchi baada ya kutoka katika ofisi hizo, Sollo amesema yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni hapo akisomea shahada ya uchumi na maendeleo na amefika ofisini hapo kujua utaratibu wa kupata fomu ukoje na kuambiwa kuwa gharama ni Sh1 milioni.

"Niliamua kufika hapa ofisi za chama kujua utaratibu wa kupata fomu ili nami nitie nia ya kugombea uspikana ndipo nikaambiwa ni Sh1 milioni.

" Lakini mpaka sasa nina Sh300,000 ambapo Sh100,000 nikiwa nayo taslimu na Sh200,000 ikiwa benki, hivyo naenda kuomba kwa wadau wengine wanichangie ili itimie niweze kuchukua fomu kwa kuwa nia na sifa ninazo za kukalia kiti hicho cha uspika na vijana tunaweza," amesema Sollo.

Akielezea uzoefu wake katika uongozi, amesema ameshawahi kuwa Mbunge Wizara ya Uchumi katika chuo hicho na pia amewahi kutia nia nafasi ya urais akiwa chuo cha Maswa na hivi karibuni kastafu Uenyekiti wa chama cha Wanafunzi wanaosomea uchumi chuoni hapo.
Maamuzi mengine kwa kweli ni 'tamaa na sifa za kijinga' tu.
 
Hongera zake huyu kijana ana udhubutu na jasiri kuliko wanaotukana humu JF.
Mkuu umeona Kama Mimi, huyo mwezangu anatengeneza njia yake, atajadiliwa na m/kiti wa ccm (Rais),na tayari atakuwa amesafisha njia kulingana na mfumo wa siasa yetu.
 
Back
Top Bottom