Mwanafunzi ajinyonga hadi kufa kwa taulo

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,900
2,000
Wanafunzi wawili wa Darasa la tano Shule ya Msingi Mikiroy Magugu Mkoani Manyara waliokuwa wanakaa Dawati moja wamefariki dunia katika matukio yanayofanana, wa kwanza alifariki Mwezi Januari mwaka huu kwa kujinyonga, mwingine amejinyonga februari 20.

Mwanafunzi huyo (11) wa darasa la tano Shule ya Msingi Mikiroy kijiji cha Magugu kata ya Magugu Wilaya ya Babati Mkoani Manyara amejinyonga kwa taulo hadi kufa.

Akizungumza na MUUNGWANA BLOG Mtendaji wa Kijiji cha Magugu Leonsi Daniel Lumbu ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Februari 20 mwaka huu baada ya mwanafunzi huyo kutoka Shuleni majira ya Jioni ambapo hakuwakuta wazazi wake ndipo alipoenda kwa jirani kuchukua ufunguo na kuingia ndani na kujinyonga kwa taulo hadi kufa.

Amesema ni mtoto ambaye anaishi na Mama yake ambaye ameolewa na mwanaume mwingine huku baba yake mzazi akimuacha tangu alipokuwa na miaka miwili baada ya kufarakana.

Mtendaji huyo amemtaja Mwanafunzi huyo kuwa ni Mathayo Ezekiel huku akieleza kwamba Sio tukio la kwanza kutokea kwani January mwaka huu 2019 mwenzake waliokuwa wanasoma darasa moja na kukaa katika Dawati moja naye alikufa kwa kujinyonga hali iliyowaacha wengi midomo wazi wakijiuliza kulikoni?

Amewataka Wazazi kuwa waangalifu na Watoto muda wote waangalie mara kwa mara mienendo yao na kuwa na muda wa kuzungumza nao ili kujua matatizo yanayowasumbua.

Hata hivyo kumeibuka mzozo wa kugombea maiti kati ya baba mlezi na baba mzazi yupi anastahili kuuzika mwili huo, hali iliyopelekea Uongozi wa Kijiji kuingilia kati na kushauri waende Mahakamani na kusikiliza amri itakayotolewa na Mahakama.
 
hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
38,772
2,000
Mmh so sad "

Hapo kuna mamna sio bure " Kuna mtu itakuwa Yupo nyuma ya mauaji hayo .kisha ana frame hiyo miili iliionekane kuwa marehemu walijinyonga "

.Au la basi hao watoto itakuwa waliathirika ki-psychology kutokana na baadhi ya matukio yenye mfanano na tukio ambalo wamelifanya " ila inastaajabisha sana kuona watoto wenye makamo hayo kuweza kufikia maamuzi ya kujiua tena kwa kujinyonga " Hii inaleta mashaka kwakweli "

police waupeleke huo mwili hospital ukafanyiwe postmortem

BTW ---Haya ni maoni yangu tu na wala sio sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kedekede

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
3,982
2,000
Mmh so sad "

Hapo kuna mamna sio bure " Kuna mtu itakuwa Yupo nyuma ya mauaji hayo .kisha ana frame hiyo miili iliionekane kuwa marehemu walijinyonga " ..... police waupeleke huo mwili hospital ukafanyiwe postmortem

BTW ---Haya ni maoni yangu tu na wala sio sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
Unauhakika?
 
Kasomeko

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
442
1,000
sidhan.kama ndo ustaarabu huo jaman...kwann asiachiwe tu baba mlezi amzike ..mtu umemuacha toka ana miaka 2 leo unataka ukamzike
Hapo sasa mkuu, hata wakienda mbele nazani uongozi unaweza kumpa haki baba mlezi. Unashindwa kumsamini mwanao akiwa hai unakuja kuthamini mwili wake!

Ni sawa kabisa na wale wasiosaidia chochote mtu awapo ngonjwa anakosa hata usafili wa kwenda hospital ila akifa utaona kuna ndg yake kahitolea kumchongea jeneza la milioni, mwingine suti ya laki3, mwingine anajitolea magari yake mawili yabebe waombolezaji. Mwingine atajitolea kuulisha msiba!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkulima msomi

Senior Member
Nov 28, 2018
159
250
Mmh so sad "

Hapo kuna mamna sio bure " Kuna mtu itakuwa Yupo nyuma ya mauaji hayo .kisha ana frame hiyo miili iliionekane kuwa marehemu walijinyonga "

.Au la basi hao watoto itakuwa waliathirika ki-psychology kutokana na baadhi ya matukio yenye mfanano na tukio ambalo wamelifanya " ila inastaajabisha sana kuona watoto wenye makamo hayo kuweza kufikia maamuzi ya kujiua tena kwa kujinyonga " Hii inaleta mashaka kwakweli "

police waupeleke huo mwili hospital ukafanyiwe postmortem

BTW ---Haya ni maoni yangu tu na wala sio sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
serial murder.labda kafara.ilo dawati waliokalia la kuogopa kama ukoma
 
mkulima msomi

Senior Member
Nov 28, 2018
159
250
Hapo sasa mkuu, hata wakienda mbele nazani uongozi unaweza kumpa haki baba mlezi. Unashindwa kumsamini mwanao akiwa hai unakuja kuthamini mwili wake!

Ni sawa kabisa na wale wasiosaidia chochote mtu awapo ngonjwa anakosa hata usafili wa kwenda hospital ila akifa utaona kuna ndg yake kahitolea kumchongea jeneza la milioni, mwingine suti ya laki3, mwingine anajitolea magari yake mawili yabebe waombolezaji. Mwingine atajitolea kuulisha msiba!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
umejuaje alikua akimudumia akiwa uko uko kwa baba mlezi
 
mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
4,396
2,000
Tabia za watani zangu wanyakyusa kugombabia maiti
Waga wananunua maiti hata kwa kulipia ng'ombe ati wakazike
 
andjul

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
17,304
2,000
Tabia za watani zangu wanyakyusa kugombabia maiti
Waga wananunua maiti hata kwa kulipia ng'ombe ati wakazike
Mwaka jana nimeenda kuzika mamaangu mkubwa Kyela, ilikuwa ni aibu,walio nisindikiza walishangaa sana.
 
Kasomeko

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
442
1,000
umejuaje alikua akimudumia akiwa uko uko kwa baba mlezi
Hakuna mwanaume anaeweza kufanya mkuu. Kwamba utume matumiz ya mtoto anaeishi kwa mwanaume nwenzio tena mwenye watoto wengine!! Hata kama hana watoto wengine wivu lazima uwepo tu na uhakika wa kwamba matumizi yanamfikia mtoto ni mdogo sana. Unaweza kutuma laki moja mtoto asipate hata mia! Unaweza kutuma nguo pea tano mwanao akapewa pea moja halafu hizo nne zilizobaki wabapewa watoto wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom