Mwanafunzi ajinyonga baada ya wazazi wake kumzuia kutojihusisha na mapenzi

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Lasmini Kondo mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Masaki wilayani Kisarawe mkoani Pwani, amekutwa akiwa amejinyonga baada ya kukatazwa na wazazi wake kutojihusisha na mapenzi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani, ACP Pius Lututumo amesema mwanafunzi huyo amejinyonga baada ya kugombezwa na wazazi wake kutojihusisha na mapenzi kufuatia kukutwa na barua aliyokuwa amemuandikia mpenzi wake.

“Baada ya wazazi wake kukuta barua ambayo marehemu alimuandikia mpenzi wake walimfokea kwa kumtaka kuachana na masuala hayo kwani yeye ni mwanafuzi.

“Kutokana na kitendo hicho marehemu aliamua kuchukua uamuzi wa kujinyonga jambo ambalo linasikitisha,” amesema.

Jamhuri
 
Hiki ndo aina ya kizazi kilichopo sasa na hii ipo kwenye familia zilizo nyingi eti mtoto hataki kugombezwa. Aisee.

Na ukiona mpaka mtoto anafikia hatua hiyo basi jua mzazi alishashindwa kumdhibiti na kumuweka wazi kuanzia chini na mwisho wa siku madhara yake ndo hayo.

Pole kwa familia.
 
Hiki ndo aina ya kizazi tulichonacho sasa kwani hii ipo kwenye familia zilizo nyingi eti mtoto hataki kugombezwa. Aisee.

Na ukiona mpaka mtoto anafikia hatua hiyo basi jua mzazi alishashindwa kumdhibiti na kumuweka wazi kuanzia chini na mwisho wa siku madhara yake ndo hayo.

Pole kwa familia.
Tulinacho au mlichonacho

Sisi wengine hayo ya hovyo ndo tunayasikia kwa radio huku watoto ni Heshima na utii 24/7.
 
Back
Top Bottom