kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,687
R.I.P Jackline Musa Matiko (kuzaliwa 2/8/1998-kuf. 1/1/2013)' Mwanafunzi aliyekuwa anasoma shule ya Sekondari Juhudi ilioko Ukonga, Dar es Salaam. Siku ya Mwaka Mpya aliondoka na ndugu wa upande wa mama yake mzazi kwenda south Beach Kigamboni, kusherehekea sikukuu hiyo maeneo ya "south beach reports" bila ya kumtaarifu baba mzazi wa Jackline. Inasemekana kuwa wanafamilia walipofika eneo hilo walianza kusherehekea kila mtu kivyake. Kufuatana na wasifu wa marehemu uliosomwa kwenye msiba "ilipofika saa tatu usiku wanafamilia walianza kutafutana ili kuelekea nyumbani, lakini Jackline hakuoneka, waliendelea kumtafuta bila ya mafanikio, ndipo wakahamua kutoa taarifa kwa uongozi husika, na kutoa taarifa kituo cha Polisi" wasifu ulieleza kuwa "Jackline ameonekana jana ktk eneo hilo lakuogelea akiwa amefariki' ndani ya maji" Kwasasa tunaelekea eneo la kufanyia mazishi' lakini kuna habari zinazokingana juu ya kifo cha mwanafunzi huyu Jackline. Inaoneka taarifa iliyotolewa kwenye wasifu wa marehemu siyo sahihi. Cha kusikitisha zaidi nikwamba wazazi wa Jackline walikuwa hawaelewani katika maisha yao. Update itakuja baadaye....
Update:KIFO CHA JACKLINE MUSA MATIKO
Kwa taarifa zaidi kutoka kwa ndugu wa karibu wa marehemu Jackline' inasemekana kuwa mwanafunzi Jackline aliongozana na dada yake na mjomba zake, jumla walikuwa watu nane kwenye gari waliloondoka nalo kwenda kusherehekea ujio wa Mwaka mpya maeneo ya South Beach resorts' na ilipofika muda wa kurudi ndipo walipokusanyana lakini wakawa wamesahau mkeka waliokuwa wamekalia, ndipo dada wa marehemu Jackline akamwambia aurudie ule mkeka' marehemu Jackline alienda kufuata mkeka, na hakurudi tena.
Mjomba wake marehemu Jackline baada ya kuona kuwa muda umepita alihamua naye kumfuata, lakini hakuweza kumuona Jackline, ndipo aliporudi kwenye gari nakuwaeleza wezake kuwa hajafanikiwa kumuona Jackline.
Hapo ndipo walipochukua jukumu la kwenda kutoa taarifa sehemu ya mapokezi, na baadaye kituo cha polisi.
HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Inasemekana kuwa kwa ushirikiano wa polisi wahudumu walitoa maji yote kwenye eneo la kuogelea kwa kutumia mitambo maalum ya kumwaga maji nje ya eneo la kuogelea, bado hawakufanikiwa kumuona Jackline.
Mjombaze Jackline waliendelea kutafuta bila mafanikio, wakahamua kurudi nyumbani bila Jackline.
NYUMBANI KWA MJOMBA WA JACKLINE
Baada ya kufika nyumbani kwa mjomba, dada yake Jackline alipiga simu kwa jirani karibia na nyumbani kwa baba yake Jackline kuulizia kama Jackline ameishafika nyumbani, jirani akajibu kuwa hana habari zozote kuhusu Jackline' "kwani ilikuwa imeishafika usiku wa manane" Na jirani akamueleza dada yake Jackline, kwanini asimpigie baba yao ili kujua kama mdogo wake amefika, lakini dada mtu akajibu kuwa anaogopa kwani waliondoka bila ya kumuaga baba yao.
JIRANI
Jirani wa kwa baba yake na Jackline baada ya muda alisikia mlango wa kwa Jackline unafunguliwa, naye jirani akatoka nje; bahati akakuta ni baba yake na Jackline, akamuliza " Jackline amerudi" baba akajibu hapana: ndipo jirani akamueleza jinsi alivyoelezwa na dada yake Jackline.
BABA
Usiku huo baba Jackline akafunga safari kwenda ukweni. Alipofika akaambiwa kuwa mama Jackline na bibi yake Jackline wamekwenda Kigamboni South Beach Resorts kumtafuta Jackline, ndipo babaye Jacline naye akafunga safari ya kwenda Kigamboni.
KIGAMBONI SOUTH BEACH RESORTS
Mara hii ni Bibi, Mama na Baba wa Jackline;
Wakati baba Jackline anafika Kigamboni South Beach Resorts, alikuta tayari bibi na mama Jackline walishafika na kutafuta kila seheme bila ya mafanikio, wakiwa kwenye harakati za kwenda kwenye vituo vya polisi'
Ndipo baba Jackline akawakatiza safari ya kwenda polisi na kusisitiza warudi kutafuta tena.
BABA wa marehemu JACKLINE, inasemekana alipofika sehemu ya mapokezi alitia mkwala mzito kwa wafanyakazi wasaidie kumtafuta mwanae; Inasemekana wafanyakazi walitii na kufanyakazi ya kusaidia kutafuta;
Pia inasemekana baba marehemu Jackline aliendelea kupekua kila sehemu ya eneo hilo la south beach resorts; ndipo atimaye mfanyakazi mmoja akawaeleza kuwa kuna mtu amefunikwa kwa shuka karibia na eneo la kuogelea; walipofika eneo hilo walikuta ni Jackline akiwa amefariki, huku akiwa na mapovu meupe mdomoni.
Ndipo walipoita polisi na mwili wa Jackline ukatolewa eneo hilo.
"taarifa zaidi zitafatia kadri tunavyozidi kudodosa kutoka kwa ndugu wa karibu na marehemu Jackline…."
"GAZETI LA MWANANCHI, JANUARI 7, 2013 (JUMATATU)
Matokeo ya uchunguzi kifo cha mwanafunzi hotelini South Beach Resorts Kigamboni kutolewa.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/-...zi kifo cha mwanafunzi hotelini kutolewa leo http://www.facebook.com/share.php?u=/habari/-/1597578/1659188/-/vjnxh7/-/index.html?relative=truehttp://www.mwananchi.co.tz/habari/-...zi kifo cha mwanafunzi hotelini kutolewa leo http://www.mwananchi.co.tz/habari/-...zi kifo cha mwanafunzi hotelini kutolewa leo http://www.mwananchi.co.tz/habari/-...zi kifo cha mwanafunzi hotelini kutolewa leo
Kwa ufupi
"Kazi yetu (madaktari) tulimaliza juzi na kesho ripoti itakuwa tayari" alisema daktari huyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe kwa maelezo kuwa si msemaji wa hospitali hiyo.
Pia alisema hawezi kuingia kwa undani kuhusu ripoti hiyo lakini alisema uchunguzi kufuatia utata juu ya kifo hicho umekamilika.
RIPOTI ya madaktari kuhusu uchunguzi wa sababu za kifo cha kutatanisha cha Jacqueline Matiko, mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Juhudi iliyopo Gongo la mboto, inatarajiwa kutolewa leo.
Mwanafunzi huyo alikutwa amekufa maji Januari Mosi mwaka huu katika Hoteli ya South Beach Resorts, iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Kulingana na maelezo ya mmoja wa madaktari walioufanyia uchunguzi wa kitabibu mwili wa marehemu juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ripoti hiyo ataiwasilisha polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

Kamanda wa Polisi Temeke, Englebert Kiyondo, alikiri kukutwa kwa mwili wa mwanafunzi huyo na kwamba kutokana na madai ya ndugu zake, mwili huo umefanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na jeshi lake linasubiri ripoti ya madaktari.
"Tunasubiri ripoti ya madaktari ili tuweze kujua ukweli," alisema na kuongeza kuwa ni mapema mno kuzungumzia suala hilo.
Alisema utata wa kifo hicho unatokana na baadhi ya wafanyakazi wa hoteli kuwa marehemu alifia katika bwawa la kuogelea.
Baba wa mwanafunzi huyo, Mussa Matiko alithibitisha kupewa taarifa na madaktari waliofanyia uchunguzi mwili wa mwanafunzi huyo kuwa ripoti watapewa leo.
Utata huo unatokana na ndugu wa marehemu ambao walikuwa nao siku ya tukio, kupingana na maelezo ya wafanyakazi wa hoteli hiyo kuwa marehemu alifia katika bwawa la kuogelea na inadaiwa siku ya tukio marehemu alipotea katika mzingira ya kutatanisha akiwa hotelini hapo.
"Alitafutwa sehemu zote bila kuonekana na tulirudi tena kesho yake asubuhi na kuulizia na walitueleza kuwa hajaonekana na hata bwawa wamebadilisha maji na kuweka dawa," alisema bibi wa marehemu Saida Hussein.
Alisema kuwa walipoondoka katika eneo la hoteli kwa lengo la kwenda hospitali tofauti kumtafuta, walikutana na baba wa mtoto katika Kivuko cha Kigamboni na kurudi tena hotelini.
Alisema katika eneo hilo waliwakuta askari polisi huku mwili wa marehemu ukiwa umefunikwa kwa shuka, pembeni ya bwawa la kuogelea.
"Inashangaza wenzangu walikuja wakaambiwa hajaoneka, lakini tuliporudi tena baadaye, bila kutarajiwa tukaukuta mwili huku askari polisi wakiwa wameitwa kuja kuuchukua," alisema' Musa Matiko, baba mzazi wa Jackline.
Baadhi ya kinamama ambao walishiriki katika kuosha mwili wa marehemu mwanafunzi huyo waliliambia Mwananchi kuwa kuna kila dalili kuwa binti alibakwa kasha kunyongwa kwani shingo yake ilikuwa imevimba na pia alikuwa na michubuko sehemu za siri.