Mwanafizikia Stephen Hawking afariki dunia akiwa na miaka 76

Mwanafizikia Stephen Hawking afariki dunia akiwa na miaka 76

Chamoto

Platinum Member
Joined
Dec 7, 2007
Posts
9,883
Reaction score
22,309
Hawking.jpg

Prof Stephen Hawking
​
Prof Stephen Hawking, mwanafizikia maarufu duniani, amefariki dunia akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.

Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali nururishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka.

Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama 'Black Hole'.

Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na angani.

Alikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).

Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema: "Tumehuzunishwa sana kwamba baba yetu mpendwa ametuacha."

"Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi."

Mambo muhimu kuhusu maisha ya Stephen Hawking

  • Alizaliwa 8 Januari 1942 Oxford, England
  • Alipata nafasi chuo kikuu cha Oxford kusomea sayansi ya mambo asilinia mwaka 1959, kabla ya kwenda kusomea shahada ya uzamifu chuo kikuu cha Cambridge
  • Kufikia 1963, alipatikana na ugonjwa ulioathiri mfumo wake wa neva na mawasiliano mwilini. Madaktari walimwambia hangeishi zaidi ya miaka miwili.
  • Alieleza nadharia yake kwamba 'black hole' kutoa "Miali ya Hawking" mwaka 1974
  • Alichapisha kitabu chake A Brief History of Time mwaka 1988. Nakala zaidi ya 10 milioni za kitabu hicho ziliuzwa.
  • Maisha yake yaliangaziwa kwenye filamu ya The Theory of Everything ya mwaka 2014 ambapo Eddie Redmayne aliigiza nafasi ya mwanasayansi huyo
Stephen Hawking alipokuwa na miaka 22 pekee aliambiwa na madaktari angeishi miaka mingine miwili pekee baada yake kupatikana na ugonjwa nadra sana wa mfumo wa neva.

Ugonjwa huo ulimfanya kulemaa na kulazimika kutumia kiti cha magurudumu.

Nyakati za mwisho za maisha yake, alikuwa hawezi kuzungumza ila kwa kutumia kifaa cha kufasiri mawazo yake na kuyageuza kuwa sauti


=====

Stephen Hawking has died at the age of 76, his family has said.

The British physicist was known for his work with black holes and relativity, and wrote several popular science books including A Brief History of Time.

"We are deeply saddened that our beloved father passed away today," a family statement said.

At the age of 22 Stephen Hawking was given only a few years to live after being diagnosed with a rare form of motor neurone disease.

The illness left him wheelchair-bound and largely unable to speak except through a voice synthesiser.

In the statement his children, Lucy, Robert and Tim said: "He was a great scientist and an extraordinary man whose work and legacy will live on for many years."

Source:BBC

Soma

Wasifu wa Profesa Stephen William Hawking

God not needed for creation: Stephen Hawking

Stephen Hawking on Religion:Science will Win!!!

Stephen Hawking says black holes don’t exist

Mwanasayansi nguli adai baada ya miaka 1,000 Dunia itateketea

God not needed for creation: Stephen Hawking

Hawking: God did not create Universe

Mwanasayansi nguli Stephen Hawking adai baada ya miaka 1,000 Dunia itateketea
 
Dah...
R.I.P. Steve...
Minds kama hizi zikiondoka, naumia na kupata faraja wakati huo huo; maana ni pengo kubwa lakini at the same time, tumeachiwa a legacy and an inspiration to never stop trying to understand ourselves and the environment we are living in.
 
Mara ya kwanza kumjua ilikua 2014/2015 nilimuona kwenye kipindi discovery science kilikuwa kina host-tiwa na michuo kaku nakumbuka kilikuwa kina husu telepotation, mara ya kwanza nilishangaa kumuona mwana fikizia anafanyaje kazi zake akiwa kwenye hali kama hiyo.. Kama sio kuumwa huyu jamaa angebadilisha/angeshangaza dunia.. R.I.P Stev.
 
Rip mwanafizikia mbobezi, hope pengo lako tutaliona Kule Discovery science Morgan Freeman atakumiss sana maana theorem zake nyingi zilipata chachu toka ktk mifano yako hai. RIP Hawking
 
R.I.P . You shaped human knowledge of the universe sorry universes .
 
Hawking said: “Because there is a law such as gravity, the Universe can and will create itself from nothing. Spontaneous creation is the reason there is something rather than nothing, why the Universe exists, why we exist.”
He added: “It is not necessary to invoke God to light the blue touch paper and set the Universe going.”
 
Huyu jamaa aliishi kwa maajabu ya Mwenyezi Mungu wakati alipoanza kuugua akiwa na umri wa miaka 20 madaktari walimwambia hataweza kuishi zaidi ya miaka 2 zaidi lakini jamaa kaishi miaka 56 zaidi
RIP Stephen Hawking
 
Mwanafizikia Stephen Hawking afariki dunia
  • Saa 2 zilizopita
Haki miliki ya picha BBC/Richard Ansett
Prof Stephen Hawking, mwanafizikia maarufu duniani, amefariki dunia akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.

Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali nururishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka.

Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama 'Black Hole'.

Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na angani.

Alikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).

Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema: "Tumehuzunishwa sana kwamba baba yetu mpendwa ametuacha."

"Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi."

Mambo muhimu kuhusu maisha ya Stephen Hawking

  • Alizaliwa 8 Januari 1942 Oxford, England
  • Alipata nafasi chuo kikuu cha Oxford kusomea sayansi ya mambo asilinia mwaka 1959, kabla ya kwenda kusomea shahada ya uzamifu chuo kikuu cha Cambridge
  • Kufikia 1963, alipatikana na ugonjwa ulioathiri mfumo wake wa neva na mawasiliano mwilini. Madaktari walimwambia hangeishi zaidi ya miaka miwili.
  • Alieleza nadharia yake kwamba 'black hole' kutoa "Miali ya Hawking" mwaka 1974
  • Alichapisha kitabu chake A Brief History of Time mwaka 1988. Nakala zaidi ya 10 milioni za kitabu hicho ziliuzwa.
  • Maisha yake yaliangaziwa kwenye filamu ya The Theory of Everything ya mwaka 2014 ambapo Eddie Redmayne aliigiza nafasi ya mwanasayansi huyo
Stephen Hawking alipokuwa na miaka 22 pekee aliambiwa na madaktari angeishi miaka mingine miwili pekee baada yake kupatikana na ugonjwa nadra sana wa mfumo wa neva.

Ugonjwa huo ulimfanya kulemaa na kulazimika kutumia kiti cha magurudumu.

Nyakati za mwisho za maisha yake, alikuwa hawezi kuzungumza ila kwa kutumia kifaa cha kufasiri mawazo yake na kuyageuza kuwa sauti.

Source: Mwanafizikia Stephen Hawking afariki dunia
 
Back
Top Bottom