MwanaFA aposti wimbo wa Juma Nature unaozungumzia muungano wa CCM na CUF

MwanaFA aposti wimbo wa Juma Nature unaozungumzia muungano wa CCM na CUF

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Nadhani hali ni tete, leo MwanaFA amepost wimbo wa Juma Nature ft Prof Jay. Huu wimbo ni wa zamani lakini wameuboresha kidogo ili kwenda sawa na siasa za sasa. Ikumbukwe wimbo huu ulikuja baada ya fujo na sio kabla. Kumuona FA amepost nimestuka maana unazungumzia masuala ya maandamano.

Kwa wanaokumbuka wimbo huu ulikuja baada ya fujo ya CCM na CUF kipindi kile CUF ina nguvu kuliko ilivyo sasa, wimbo una beat ileile ila wameongezea ubeti wa kumtakia mitano tena Rais Samia. Ila stanza ya kwanza inazungumzia masuala yale yale ya maandamano. Chorus ya wimbo huu umebadilishwa kusema tu "Huree! Huree! Tanzania" Chorus ya zamani ilikuwa "Muungano CCM na CUF sote tunaulilia, kilichobaki kuijenga imani sote tunashangilia, Huree! Huree!"

Sikiliza huu wimbo wa sasa

View: https://www.youtube.com/watch?v=hegEI46FZBM

Na huu ni wimbo original uliokuwa kwenye album ya Ugali.

View: https://www.youtube.com/watch?v=h6pHudzbehI
 
Swali muhimu la kujiuliza ni hili:

Nani kabadilika kati ya hao wote: CUF au CCM, kwamba wawli hao waanze kuwa na ushirikiano kati yao?
 
Back
Top Bottom