Mwanadamu na maisha baada ya kifo

Mwanadamu na maisha baada ya kifo

Kumekua na imani na theories mbali mbali kuelezea maisha ya mwanadamu baada ya kifo. Kila mtu anaamini ktk chake kutokana na alivyoaminishwa.

Huko kwetu uchagani, ipo imani kuwa mtu akifa, hurudi kwa wajomba, hivyo wanafanya mila ya kwenda kumchukua kwa wajomba na kumrudisha kwa baba yake na anakua ancestor ambaye wanakua wakimwomba awasaidie kutatua matatizo pale wanapokumbwa na magumu.

Imani nyingi za kidini zinaeleza kuwa mtu akifa, kama alitenda mema, basi huenda mbinguni kwa Mungu kuishi kwa furaha na kama ulikua mwovu enzi za uhai wako, basi unadimbukizwa jehanamu kwenye everlasting fire..

Wapo wanaoamini kuwa mtu akifa ndo mwisho wake na hakuna maisha mengine baada ya hapo.

Binafsi mimi imani yangu ni ile ya kidini (Ukristo) kwamba mtu ataenda mbinguni baada ya kifo endapo alitenda mema,, na ataenda motoni endapo alitenda maovu..

Vipi wewe kwa upande wako unaamini vipi kuhusu hili?
Iko hivi ukifa unakuwa umekufa kabisa. Yaani unakuwa haupo kabisa na kinachobakia ni mwili tu ambao nao unaanza kuoza. Roho ya Mwanadamu haina uwezo wa kuona, kusikia, kunusa, kuhisi, kufikiri, kuongea wala kufanya chochote kile. Roho ya Mwanadamu ni pumzi tu unayoivuta ukiwa hai. Kumbuka baada ya MUNGU kumuumba Mwanadamu wa kwanza, alimpulizia puani pumzi ya uhai ndipo Mwanadamu akawa kiumbe hai. Ili Mwanadamu awe kiumbe hai ni lazima mwili wake uungane na pumzi ya MUNGU. Unapokufa ile pumzi inamrudia MUNGU na kuifadhiwa, iwe ulitenda mema au mabaya haijalishi, pumzi zote zinahifadhiwa kwa MUNGU. Kumbuka nimekuambia kuwa pumzi haina ufahamu wowote ule.

Sasa kitakachofanyika siku ya mwisho, kwa uwezo alionao MUNGU atapuliza tarumbeta kubwa sana inajulikana kama "PARAPANDA", kwa kuipuliza parapanda hiyo, pumzi zile zilizohifadhiwa zitatoka kwenye parapanda hiyo na kurudi kwenye mifupa yote iliyolala popote pale na kuwafanya wote waliokufa kuwa hai tena. Unaweza ukasema sasa itakuwaje kwa wale waliokufa kwa kuteketea kwenye moto na mifupa yao kuungua kabisa? Jibu ni rahisi sana, MUNGU anauwezo wa kuwarudishia kila kitu, kuanzia mifupa yao na hata mavazi waliyokuwa wamevaa siku ile walipokuwa wakichomwa moto. Kama aliweza kumfinyanga Mwanadamu kutoka kwenye udongo, atashindwaje kuwafanya waliokufa hata kama ni kwa kuteketea kwenye moto kuwa hai tena??

Baada ya wafu kufufuliwa ndipo sasa watu wote watahukumiwa kwa kadiri ya matendo yao. Biblia imeandika vizuri sana kuhusu hili. Isitoshe MUNGU ni mwenye haki sana, hawezi kuwatupa kwenye moto sasa hivi baadhi ya wafu wanapokufa, kisha mwisho wa dunia awafufue na kuwatupa tena kwenye moto kwa mara ya pili? Kwa kuwa MUNGU ni mwenye haki, ndiyo maana ametenga siku moja tu ya hukumu kwa watu wote, wafu na walio hai (kumbuka pia imeandikwa siyo watu wote wataonja mauti, kuna watu hawatakufa kabisa).

Tena kuna watu waliokufa zamani walishafufuliwa tayari. Watu hao ni Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Na wengine ni Musa, Eliya na wengine wengi tu bila kumsahau MESSIAH (YESU KRISTO). Ukitaka kujua kuna watu wamefufuliwa tayari, soma Biblia yako; MATHAYO 27:51-53. Pia ukisoma Biblia yako utaona Yohana anaelezea katika kitabu cha UFUNUO kuwa aliwaona Wazee 24 wakiwa Mbinguni pamoja na MUNGU. UFUNUO 4:4, 5:5. Hivyo basi ili uweze kufika kwa MUNGU ni lazima ufufuliwe kwanza, sababu pia imeandikwa MUNGU siyo MUNGU wa wafu, bali ni MUNGU wa walio hai.

Kuna wengine watasema hapa inakuwaje basi wakati mwingine tunatokewa na ndugu zetu waliokufa? Yule anayekutokea baada ya ndugu yako kufa siyo yeye aliyekufa, bali ni shetani, anajibadilisha na kuwa na sura kama ya ndugu yako na kukutokea ili kukudanganya na kukupoteza ili uamini kuwa watu wakifa wanaendelea kuishi.

Kumbuka shetani alimdanganya HAWA pale Bustanini kwa kumwambia kuwa; akila matunda ya Mti ule hatakufa kabisa, bali atakuwa kama MUNGU akijua mema na mabaya. Sasa ili shetani aendelee kuutetea huu uwongo wake ndiyo maana mtu akifa, shetani hujibadilisha na kujifanya yeye ni yule mtu na kuwatokea ndugu na hata wakati mwingine kuongea nao na kuwaambai ili wafanikiwe kwenye maisha, wafanye mambo fulani fulani, kama kuchinja Mbuzi juu kaburi au kutoa sadaka fulani. Kwa kufanya hivi shetani anakuwa anawadanganya watu hao na wanaanza kuwaabudu wafu badala ya kumwabudu MUNGU. Tena siyo wanawaabudu wafu, hapana bali wanamwabudu shetani mwenyewe bila ya wao kujua.

Biblia imonya kuwa shetani ni mjanja sana na mweruvu. Tunapaswa kumwomba MUNGU sana ili tuing'amue mitego na uwongo wa huyu Ibilisi. Mbaya zaidi uwongo wake huu, ameueneza mpaka kwenye Makanisa. Makanisa mengi sana yanaamini eti mtu akifa anaendelea kuishi wakati siyo kweli. MUNGU alisema hivi; "U mavumbi wewe, na mavumbini utarudi".

 
Watu wataenda mbinguni ama Jehanum siku ya kiama na sio sasa... Kilichopo sasa hivi mtu akifa ni roho yake kutohangajka popote kama alitenda mema... Hii ndio dhana ya mbinguni na kwa wale waliotenda mabaya roho zao hutangatanga huku na kule na kukutana na mambo mabaya mengi... Hii ndio dhana ya Jehanum kwa sasa... Wafu wote wanasubiri parapanda kuu... Siku ya kiama ama hukumu kuu
Vilevile umemsahau na wanaoamini katika maisha baada ya kifo -reincarnation
Nakubaliana na wewe mkuu
 
Mimi naomba nilikatishe jukwaa hili kutokuwa na matumaini hewa!! Hakuna maisha baada ya kifo. Umekwisha umekwisha tu. Hii tuliyonayo ni huruma za mwanaadamu kuelekea kifo!! Tusingependa kutenganishwa na wapendwa wetu for good, badala yake tunabaki kwenye matumaini haya hewa ya kuonana paradiso

Hii ni imani yangu na si ya jumuia yoyote
Sawa ni imani yako na uitilie mkazo sasa
 
We jidanganye hivyo hivyo kifo huja kama ajali na siyo lazima uugue unaweza ukazima kama umeme saa yoyote hata hapo unaposoma hii comment unaweza ukaanguka hapohapo na ukawa umeiyanza safari ya kuzimu. Kikubwa nikuamini mungu na ukafanya yale yanayo mpendeza mungu na kuacha asiyo yapenda bac.
Sawa nitaacha yote lakini papuchi na bia siachi ng'oooo
 
Take ur time to read this short story..

An Egg Story..

You were on your way home when you died. It was a car accident. Nothing particularly remarkable, but fatal nonetheless. You left behind a wife and two children. It was a painless death. The EMTs tried their best to save you, but to no avail. Your body was so utterly shattered you were better off, trust me. And that's when you met me. "What… what happened?" You asked. "Where am I?"
"You died," I said, matter-of-factly. No point in mincing words. "There was a… a truck and it was skidding…"
"Yup," I said.
"I… I died?"
"Yup. But don't feel bad about it. Everyone dies," I said. You looked around. There was nothingness. Just you and me.
"What is this place?" You asked. "Is this the afterlife?"
"More or less," I said.
"Are you god?" You asked.
"Yup," I replied. "I'm God."
"My kids… my wife," you said. "What about them?"
"Will they be all right?"
"That's what I like to see," I said. "You just died and your main concern is for your family. That's good stuff right there."
You looked at me with fascination. To you, I didn't look like God. I just looked like some man. Or possibly a woman. Some vague authority figure, maybe. More of a grammar school teacher than the almighty.
"Don't worry," I said. "They'll be fine. Your kids will remember you as perfect in every way. They didn't have time to grow contempt for you. Your wife will cry on the outside, but will be secretly relieved. To be fair, your marriage was falling apart. If it's any consolation, she'll feel very guilty for feeling relieved."
"Oh," you said. "So what happens now? Do I go to heaven or hell or something?"
"Neither," I said. "You'll be reincarnated."
"Ah," you said. "So the Hindus were right,"
"All religions are right in their own way," I said. "Walk with me." You followed along as we strode through the void. "Where are we going?"
"Nowhere in particular," I said. "It's just nice to walk while we talk."
"So what's the point, then?" You asked. "When I get reborn, I'll just be a blank slate, right? A baby. So all my experiences and everything I did in this life won't matter."
"Not so!" I said. "You have within you all the knowledge and experiences of all your past lives. You just don't remember them right now." I stopped walking and took you by the shoulders. "Your soul is more magnificent, beautiful, and gigantic than you can possibly imagine. A human mind can only contain a tiny fraction of what you are. It's like sticking your finger in a glass of water to see if it's hot or cold. You put a tiny part of yourself into the vessel, and when you bring it back out, you've gained all the experiences it had.
"You've been in a human for the last 48 years, so you haven't stretched out yet and felt the rest of your immense consciousness. If we hung out here for long enough, you'd start remembering everything. But there's no point to doing that between each life."
"How many times have I been reincarnated, then?"
"Oh lots. Lots and lots. An in to lots of different lives and experiences." I said. "This time around, you'll be a Chinese peasant girl. "Wait, what?"
"Time, as you know it, only exists in your universe. Things are different where I come from."
"Where you come from?" You said.
"Oh sure," I explained "I come from somewhere. Somewhere else. And there are others like me. I know you'll want to know what it's like there, but honestly you wouldn't understand."
"Oh," you said, a little let down. "But wait. If I get reincarnated to other places in time, I could have interacted with myself at some point."
"Sure. Happens all the time. And with both lives only aware of their own lifespan you don't even know it's happening."
"So what's the point of it all?"
"Seriously?" I asked. "Seriously? You're asking me for the meaning of life? Isn't that a little stereotypical?"
"Well it's a reasonable question," you persisted.
I looked you in the eye. "The meaning of life, the reason I made this whole universe, is for you to mature."
"You mean mankind? You want us to mature?"
"No, just you. I made this whole universe for you. With each new life you grow and mature and become a larger and greater intellect."
"Just me? What about everyone else?"
"There is no one else," I said. "In this universe, there's just you and me."
You stared blankly at me. "But all the people on earth…"
"All you. Different incarnations of you."
"Wait. I'm everyone!?"
"Now you're getting it," I said, with a congratulatory slap on the back.
"I'm every human being who ever lived?"
"Or who will ever live, yes."
"I'm Abraham Lincoln?"
"And you're John Wilkes Booth, too," I added.
"I'm Hitler?" You said, appalled.
"And you're the millions he killed."
"I'm Jesus?"
"And you're everyone who followed him."
You fell silent.
"Every time you victimized someone," I said, "you were victimizing yourself. Every act of kindness you've done, you've done to yourself. Every happy and sad moment ever experienced by any human was, or will be, experienced by you."
You thought for a long time.
"Why?" You asked me. "Why do all this?"
"Because someday, you will become like me. Because that's what you are. You're one of my kind. You're my child."
"Whoa," you said, incredulous. "You mean I'm a god?"
"No. Not yet. You're a fetus. You're still growing. Once you've lived every life and experiences throughout all time, you will have grown enough to be born."
"So the whole universe," you said, "it's just…"
"An egg." I answered.
Now it's time for you to move on to your next life...
 
Tuhame kidgo

Hv kuku anajua mema na mabaya?
Ingekuwa hujui asingekukimbia ukimkaribia, kuku Ana akili nyingi sana, kama ulizani hana akili umekosea sana, kuku hatelekezi watoto wake wakiwa wadogo, binaadamu anawatelekeza na kuja kuwa tafuta ukubwani,
 
Dini nyingi zinazoabudu miungu zinaamini ukifa utazaliwa tena kwenye umbo tofauti kulingana na matendo yako ya nyuma... Unaweza kuzaliwa kama mbwa koko kama uliwatesa mbwa your past life
Nakushukuru kwa maelezo .... SERIES moja ya huko far east iitwayo JOURNEY TO THE WEST wengine huiita MONKEY ama SHIVO ndani yake pana muhusika ambaye story yasema ni REINCANATION ... anawindwa kwa imani kuwa nyama yake ikiliwa mlaji ataishi milele ...
 
Nakushukuru kwa maelezo .... SERIES moja ya huko far east iitwayo JOURNEY TO THE WEST wengine huiita MONKEY ama SHIVO ndani yake pana muhusika ambaye story yasema ni REINCANATION ... anawindwa kwa imani kuwa nyama yake ikiliwa mlaji ataishi milele ...
Sahihi kabisa na yule SHIVO ni SHIFU au master kwa kichina
 
Dini nyingi zinazoabudu miungu zinaamini ukifa utazaliwa tena kwenye umbo tofauti kulingana na matendo yako ya nyuma... Unaweza kuzaliwa kama mbwa koko kama uliwatesa mbwa your past life
Na toleo la binadamu ni nini?
 
Na toleo la binadamu ni nini?
Unaweza kuzaliwa mbwa lakini kwenye nyumba ya kitajiri usiwe na shida yoyote na unaweza kuzaliwa binadamu Lakini ukazaliwa Syria Sudan au mogadishu inategemea na past life yako
 
Back
Top Bottom