Mwanadamu na maisha baada ya kifo

Mwanadamu na maisha baada ya kifo

Imani yangu kuhusu mtu akifa nikwamba , ile roho inaingia kwenye kiumbe kingine kinachozaliwa , ila kama jinsia haibadiliki,

Kama roho ilitoka kwenye jinsia ya kiume basi itaingia kwenye kiumbe kingine cha kiume kinacho zaliwa,

Roho za binadamu kwa binadamu, wanyama kwa wanyama, wadudu kwa wadudu nk
Hii imani umeitoa wapi mkuu.. Je angalau kuna ushuhuda wa kitu chochote kifananacho na hiki?
 
UFUNUO WA YOHANA: SURA 20
11 Kisha nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe, na yule aketiye juu yake. Dunia na mbingu vikatoweka mbele ya macho yake, na havikuonekana tena. 12 Kisha nikawaona watu wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu cha uzima, kikafunguliwa pia. Wafu wakahukumiwa kadiri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo. 13 Bahari ikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yake; kifo na kuzimu vikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yao. Kila mmoja akahukumiwa kufuatana na matendo yake. 14 Kisha kifo na kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili. 15 Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto.
Shukran mkuu ila mbona maandiko haya yanaelezea kifo na uzima pamoja na mbinguni na kuzimu na wala siyo roho km nilivyokuomba?
MANENO HAYA ALIYASEMA YESU MWENYEWE- LUKA 16:

19 Akasema, “Palikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima, alikuwa akiletwa mlangoni kwa huyo tajiri kila siku. 21 Lazaro alikuwa akitamani kula makombo yaliyodondoka mezani kwa tajiri. Hata mbwa walikuwa wakiramba vidonda vyake.

22 “Hatimaye, yule maskini alikufa. Malaika wakamchukua akakae pamoja na Ibrahimu mbinguni. Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa. 23 Alipokuwa kuzimuni ambapo alikuwa akiteseka, alita zama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro karibu yake. 24 Akaita, ‘Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.’ 25 Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwa nangu, kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka, ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka. 26 Isitoshe, kati yetu na ninyi huko, kumewekwa bonde kubwa lisilopitika ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.’ 27 Akasema, ‘Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, 28 awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.’ 29 Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.’ Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, 30 ‘Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.’

31 “Ibrahimu akamwambia, ‘Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.”’
 
Maelezo mazuri sana mkuu..

Ila hujaweka reference ya hoja ya kwamba, roho ni pumzi na haioni wala kuwa na ufahamu..
Usichanganye habari mkuu, siyo roho zote ambazo hazioni wala hazisikii wala kuhisi chochote zinapokuwa nje ya mwili, ni roho ya Mwanadamu ndiyo iko hivyo. Lakini viumbe wale ambao hawana miili bali wao ni roho moja kwa moja wao wako tofauti. Malaika wao hawana miili kama yetu, wao ni Roho moja kwa moja, hivyo wanaona, wanasikia, wanafikiri tena wananguvu kutuzidi sisi.

Roho ya Mwanadamu, ambayo ni pumzi, ikiwa nje ya mwili haiwezi kufanya lolote lile. Kuhusu reference soma MHIBIRI 9:5, 9:10, 12:7, ZABURI 115:17, 146:4.
 
Tukifa tunaenda kuimba "mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, " tunakizunguka kiti cha enzi. Tukishangilia.
 
Uzuri ukitubu dakika tano kabla ya kifo unasamehewa makosa yako yote, mimi nasubiri nikianza kuugua pale nitakapoona kuwa huu ugonjwa siwezi kupona ndiyo nitatubu dhambi zangu ili nikaendelee kula raha kwa Mungu

OMBA TOBA SASA MAANA UNAWEZA KUFA KWA AJALI USIPATE HUO MUDA WA KUOMBA TOBA
 
Anglia inzi, anaishi siku saba tu! Akifa ameondoka jumla. Hata binadamu japo ana utashi anapotea kama inzi .Hakuna maisha baada ya kifo ila ni hofu tu ili uishi vizuri pasipo kutenda mabaya. Basi pambana na hali yako
 
Anglia inzi, anaishi siku saba tu! Akifa ameondoka jumla. Hata binadamu japo ana utashi anapotea kama inzi .Hakuna maisha baada ya kifo ila ni hofu tu ili uishi vizuri pasipo kutenda mabaya. Basi pambana na hali yako
Haha.. Wewe unaamini uwepo wa Mungu?
 
Kumekua na imani na theories mbali mbali kuelezea maisha ya mwanadamu baada ya kifo. Kila mtu anaamini ktk chake kutokana na alivyoaminishwa.

Huko kwetu uchagani, ipo imani kuwa mtu akifa, hurudi kwa wajomba, hivyo wanafanya mila ya kwenda kumchukua kwa wajomba na kumrudisha kwa baba yake na anakua ancestor ambaye wanakua wakimwomba awasaidie kutatua matatizo pale wanapokumbwa na magumu.

Imani nyingi za kidini zinaeleza kuwa mtu akifa, kama alitenda mema, basi huenda mbinguni kwa Mungu kuishi kwa furaha na kama ulikua mwovu enzi za uhai wako, basi unadimbukizwa jehanamu kwenye everlasting fire..

Wapo wanaoamini kuwa mtu akifa ndo mwisho wake na hakuna maisha mengine baada ya hapo.

Binafsi mimi imani yangu ni ile ya kidini (Ukristo) kwamba mtu ataenda mbinguni baada ya kifo endapo alitenda mema,, na ataenda motoni endapo alitenda maovu..

Vipi wewe kwa upande wako unaamini vipi kuhusu hili?
Watu huwa hawaamini vitabu vya dini japo maandiko huwa yanatimia polekwapole

Naamini baada ya kifo ni kama usingizi tu yani mtu kutojitambua kwa namna yoyote ile na siku ya hukumu ndiposa uhai utarudishwa na watu kupata mishara yao hapo

Wema kwa wema na wabaya kwenye ubaya na ndipo wema wataishi milele duniani na sio mbinguni
serikali haitakuwa ya binadamu tena mungu ndio atakuwa mtawala wa dunia yote na kila kitu kitaenda sawa

Uovu na waovu wote vitaketezwa na kurudi katka hali ya kutokuwepo tena

Leo shetani ndio mtawala wetu ndio maana mambo yanaenda kama tunavyoona
 
Ni Atheism. Na atheist hana haja ya kubelieve maana yeye huangalia facts zenye evidence. Thats all
Nashukuru kwa hiyo correction ... actually it was simply a typing error ... by the way waweza nidokeza japo ONE among those CONCRETE EVIDENCES about ATHEISM who knows I may be among ATHEISTS
 
Kama maisha yapo baada ya kifo labda ile roho inaanzisha maisha mengine tofauti na yale ya mwanzo. Wewe mwili unaoza unapotea katika uso wa dunia. Tuachane na kutafuta chanzo cha hayo roho kwani akina Aristotle, Socrates, Plato walikufa bila jibu, na sisi tugange yaliyopo na yajayo tu, ila pambana na hali yako
 
Kama maisha yapo baada ya kifo labda ile roho inaanzisha maisha mengine tofauti na yale ya mwanzo. Wewe mwili unaoza unapotea katika uso wa dunia. Tuachane na kutafuta chanzo cha hayo roho kwani akina Aristotle, Socrates, Plato walikufa bila jibu, na sisi tugange yaliyopo na yajayo tu, ila pambana na hali yako
Wewe pia ni atheist?
 
Back
Top Bottom