Mwanadada huyu ajitengeneza mwenyewe kama roboti (snyths Robotic Humanoids from sanctuary AI)

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
Wasalaam

Mafundi na wataalamu au Wakurugenzi na Wakuu wengi katika dunia ya sasa ya maendeleo ya sayansi na teknolojia iliyopanuka mithili ya ndege afunuae mbawa zake ., wanaonyesha mifano ya roboti zinazofanana na kuonekana karibu kila kitu na binadamu huu umekuwa mchezo wa mashindano hivi sasa kila kampuni(shirika) ya maroboti kuibuka na roboti ya aina yake.

Kuna msemo maarufu hapa kwetu kutoka katika media fulani hapa nchini namimi kama DaVinci XV nmekuwa ni mwenye kuuhusudu sana huo msemo na kuutumia kwenye matumizi ya hapa na pale

" TUNAKUFUNGULIA DUNIA KUWA UNACHOTAKA"

Basi sayansi au teknolojia au vyote kwa Pamoja imeamua kutufungulia Dunia kisha wewe na Utashi wako utachagua kuwa unachokitaka.

Wakati dunia ikiwa bize na utaalamu wa yule dogo njiti aliezaliwa kule Rosario Argentina , Masihi wa mpira , mnamwita la pulga na chenga zake za haja na Maudhi tele mithili ya Mama mjamzito na kichefuchefu

Mimi ninawaza nitamsimulia mangapi Babu yangu Wa kule songea Mzee kinjeketile Ngwale au Chifu Mangungo wa huko msovero kilosa kama atafufuka saivi, Pengine nitamsimulia mengi kuhusu sayansi na teknolojia hadi nikashindwa kumuelezea namna ya vijana wa sasa wanavyomcheka baada ya kusainishwa Bogus Treaty na kijana mmoja wa ovyo mjerumani mwenye roho chafu kijana wa Miaka 28, Karl Peters.

8A3B3B47-264C-446C-87BC-94C165046CDF.jpeg


Synth (short for sythetic humanoids, also called androids or artificial human)
Hilo ni neno la kawaida linalotumiwa kuwatambulisha roboti za kutengeneza kibiolojia zinazotengenezwa ndani ya maabara za Taasisi ya Sanctuary AI., ambao wanafanana karibia kila kitu na binbinad.

Suzanne Gildert Mwanamama huyu fundi mwanafizikia na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Sanctuary AI, yeye amekuja na lakwake tena la kwanza kabisa baada ya kuonyesha moja ya roboti ambayo imeundwa ikifanana kabisa na yeye mwenyewe.

EE6255FD-48BE-40E8-868A-CE3DD0140C7A.jpeg


Akizungumza katika mkutano wa Canadian Innovation Exchange (CIX) huko Toronto , Canada , doppleganger ya roboti ya Gildert ilionyeshwa kwenye skrini mwishoni mwa maelezo yake , ambapo pia aliwashukuru watazamaji kwa muda wao.

Roboti hiyo ilikuwa na miwani ileile, nywele ndefu zilezile, na ilikuwa lafudhi ileile ya Kama ya kwake.

Gildert aliweka wazi kuwa roboti hiyo haikukusudiwa kama zoezi la narcissism (kujikubali yeye zaidi) lakini Ni katika hali ya kutafuta utofauti wa kipekee na sanaa fulani tu na njia ya kuanza kufikiria juu ya ya "haki za roboti" kama mashine zenye akili nyingi na zinazoweza kuhitaji mara moja kuingia maofisini na kwenye jamii kwa ujumla, kufanya shughuli za kibinadamu kwa ufanisi zaidi.

2DBD39CA-079F-45B3-A4B3-EE88AA25FC88.jpeg


Gildert alisema kama amepata mrithi wake ambaye atadumu milele, yeye kwakati atakaoondoka alisema

"Nataka watu waitendee(itumie) roboti hii vizuri, na kuona kwamba inarithi maadili yangu."

Ingawa kampuni zingine zinaweza kudharau kufanana kati ya roboti na wanadamu,Gildert yeye alisema dhamira ya Sanctuary AI ni kuwafanya wawe karibu na kile ambacho kimeonyeshwa katika filamu za kisayansi, sawa na kazi ya kampuni kama Hanson Robotics.
Kwa maneno mengine, roboti zinazofanana na kufanya kazi sawa na waundaji wao.

F74C9CE9-ECC5-4AEF-BCFE-0B43FC4750AE.jpeg


Gildert alisema

"Ulimwengu wetu umeundwa kwa ajili ya wanadamu, Tunaweza kubadilisha miundombinu iliyopo, ambayo inaweza kuhitaji matrilioni ya dola kuendana na hali ya roboti na AI kwa sasa, au kuwafanya kama tulivyo sisi hivi sasa ili waweze kuchukua faida ya rasilimali hizo zote za ziada."

Kando na kuondoa hitaji la kubuni mazingira ya kufanya kazi karibu na roboti, Gildert alisema mbinu ya Sanctuary AI itatoa jukwaa la aina ili kuendeleza utafiti katika maeneo kama vile kujifunza kwa mlolongo, maono ya kompyuta, usanifu wa utambuzi na mchanganyiko wa sensorer. Kuunda androids za uhalisia pia kutawasaidia kujifunza vyema wao wenyewe na kuwasiliana kwa ufanisi zaidi.
411414D9-B9CF-410E-8BE7-8F8497337FDA.jpeg


Roboti kama hizo, au "synths" kama vile Sanctuary AI wanavoziita, hazihitaji kuwa na gharama kubwa kutokana na maendeleo mengine ya hivi karibuni ya teknolojia, Gildert alisema.

Baada ya muda, Sanctuary AI inatarajia roboti kama hizo kugharimu sawa na za gari tu.

Ingawa Gildert alisema kampuni yake bado inachunguza mwanya wa soko la bidhaa yao hiyo, baadhi ya maeneo yaliyowezekana kwa Roboti zao kufanya kazi ni pamoja na maeneo kama vile ustawi na utunzaji wa wazee, ambapo synths Sanctuary AI inaweza kufanya zaidi ya kazi za binadamu pasi na kuchoka lakini kutoa thamani ya kijamii na ubunifu katika aina mbalimbali za mwingiliano wa kibinadamu. Na wahudumiwa huhisi wakipewa na wanadamu wenzao wa kawaida.

Wakati huo huo, moja ya roboti zake, inayoitwa Nadine, tayari inatumiwa katika Ulimwengu wa Sayansi B.C. huko Vancouver katika vipindi vya kuwafundisha na kuwaelimisha watoto.

Tunajaribu
kuweka usawa kati ya kutotaka kuchukua kazi za watu lakini pia kuangalia kile ambacho ni kizuri kijamii,"


aliambia Mtandao wa Habari wa B2B.

"Tunataka kuzingatia mahali ambapo kuna uhaba wa watu wa kufanya kazi na ambapo mwingiliano na wanadamu ni wa kujali sana na wenye huruma kufanya kazi katika kazi hizi za malipo.


Da VINCI XV
 
Kuna jambo ambalo linakuja taratibu. Ulimwengu wa artificial intelligence ambapo robots zitaishi na wanadamu
Kabisaaa mkuu duniaa inakokwenda dates za binadamu na robboti ni kawaida sana itakuwa mkuu
 
Kuna movie hii hapa fungua uangalie raha na karaha za hawa Artificial Intelligence.
👇🏾



Na lazima mjue mwisho wa siku hawa AI watakuwa kama Covid, i mean watakuja kuleta matatizo kwenye uso wa dunia.

Mfano watazalishwa kina Clara 10 na wote wakaingia kufanya kazi ofisi iliyokuwa na employed 10 je, hao 10 employee wataenda wapi?.

Kumbuka kina Clara hawaendi lunch, dinner wala kupumzika zaidi ni kuchaji kama smartphone otherwise ni full kazi.

👉🏾On this open that movie above and watch it.
 
Kuna movie hii hapa fungua uangalie raha na karaha za hawa Artificial Intelligence.
👇🏾



Na lazima mjue mwisho wa siku hawa AI watakuwa kama Covid, i mean watakuja kuleta matatizo kwenye uso wa dunia.

Mfano watazalishwa kina Clara 10 na wote wakaingia kufanya kazi ofisi iliyokuwa na employed 10 je, hao 10 employee wataenda wapi?.

Kumbuka kina Clara hawaendi lunch, dinner wala kupumzika zaidi ni kuchaji kama smartphone otherwise ni full kazi.

👉🏾On this open that movie above and watch it.

Ni kweli ...
Ndiyo maana duniani hivi sasa kuna wimbo wa chinichini 'UPGRADE YOURSELF '
 
atengeneze robotic papuchi azilete uku, tumechoka mizinga
Hizo zipo kitambo sana na zinauzwa mpaka madukani.

Hizi za sasa AI zimeUpgrade na kuweza kujishugulisha as real human but zile zenye hiyo sijui papuchi ni women robot unaweza kuivisha nguo au kuivua but aitembei ina kila kitu as mwanamke inakuwa na self power unamchaji kwenye umeme so wakati wa kujamiiana nayo kazi ni wewe tu utakavyo na inatoa sauti za mahaba kama kawa.
 
Wasalaam

Mafundi na wataalamu au Wakurugenzi na Wakuu wengi katika dunia ya sasa ya maendeleo ya sayansi na teknolojia iliyopanuka mithili ya ndege afunuae mbawa zake ., wanaonyesha mifano ya roboti zinazofanana na kuonekana karibu kila kitu na binadamu huu umekuwa mchezo wa mashindano hivi sasa kila kampuni(shirika) ya maroboti kuibuka na roboti ya aina yake.
"Tunataka kuzingatia mahali ambapo kuna uhaba wa watu wa kufanya kazi na ambapo mwingiliano na wanadamu ni wa kujali sana na wenye huruma kufanya kazi katika kazi hizi za malipo"

Tunasema hakuna ajira kila kona yeye anakuja kusema kuna mahali kuna uhaba wa watu wa kufanya kazi!??

Labda yeye asema haya maroboti yapelekwe sehemu hatarishi kama migodini,vitani au kwenye viwanda hatarishi.
 
"Tunataka kuzingatia mahali ambapo kuna uhaba wa watu wa kufanya kazi na ambapo mwingiliano na wanadamu ni wa kujali sana na wenye huruma kufanya kazi katika kazi hizi za malipo"

Tunasema hakuna ajira kila kona yeye anakuja kusema kuna mahali kuna uhaba wa watu wa kufanya kazi!??

Labda yeye asema haya maroboti yapelekwe sehemu hatarishi kama migodini,vitani au kwenye viwanda hatarishi.
Mkuu nadhani huku kwetu tu ndiko ajira kipengere ....juzi kati nmeona nchi zilizoendelea kama Canada zinavyohitaji wafanyakazi katika nyanja tofauti wengi mno

Kwa wenzetu si haba kuona mtu anafanya kazi karibu sehemu tatu tofauti na anaingia kwa siku moja

Nadhani hilo la kuwapeleka katika kazi ngumu kama migodini limenivutia zaidi🤝🤝
 
Back
Top Bottom