Mwanachuo kupewa Sh. 2750 kwa mwaka na Bodi ya Mikopo?

Ukisikia watu wanasema ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni basi ndio hii.
Mmoja wa mwanachuo wanaoanza mwaka huu, atapewa sh.2750 kwa mwaka.
Kwa lugha nyepesi kabisa huyu mwanachuo anapaswa kutumia Sh.10 kwa siku ili aweze kusoma semister zote mbili kwa mwaka.
Yes, Sh.10. mwenye ushauri atoe ili dogo aweze ku-survive chuo kwa hiyo sh.10 kwa siku.
......kazi iendeleee.......
View attachment 1984548
Ni dosari tu itarekebishwa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Huu Ni upuuzi wa kiwango Cha juu..maofisa wa bodi wenyewe wamenenepeana Kama wajawazito alafu mtoto wa masikini anapewa mkopo sh 2700
 
Ashukuru tu serikali ya CCM hata kwa hiyo elfu mbili. Kuna wengine hawapati hata shilingi.
Sasa hiyo hela inamsaidia Nini ???
Bora wangemnyima hivyo Ila wakampa meals and accommodation,,
maana hiyo walompa haiusiani na chakula ni mwendo wa kuteseka tu
 
Ina maana huyo mwanafunzi aliyepata 2750 hajajulikana tu jina lake na chuo gani kadahiliwa..?
Kwenye ile PDF ya heslb yuko namba ngapi.. Nataka nithibitishe hii issue kama ni kweli kupitia lile PDF maana bodi ilishakanusha hii habari.. Aliyefanikiwa kupata jina la huyo mwanafunzi kupitia PDF la heslb tunaomba mturahisishie basi
 
hiyo mbona ni kawaida mkuu, hivi mtu amesoma olevel St Francis ya Mbeya ada millioni sijui 5 huko, advance kasoma Feza ada milioni sita huko, unampatiaje mkopo wakati ada ya chuo tu ni milioni moja na laki tatu.
Una uhakika gani huyo mwanafunzi kasoma St Francis na Feza??
 
Kuna haja ya bodi kuwa inaeleza sababu za waombaji kupewa hela kidogo au kukosa kabisa.
Mtu anaomba mkopo mwaka wa kwanza anakosa - hakuna sababu ya kwa nini hakupata, anasubiri mwaka unaofuata anaomba tena hapati na hakuna sababu!
Ni vizuri mkaeleza kuwa hukupata mkopo kwa sababu hizi akiona hawezi kuzirekebisha asijisumbue kuomba tena na tena. Angalia majibu kwa mtu aliyeomba, akakata rufaa, majibu ya rufaa yako hivi:

Uchambuzi na upangaji mikopo kwa 2021/2022 umekamilika. Tumeanza kupokea maoni ili kuboresha utendaji kazi na kuwafikia wahitaji wengi zaidi katika mwaka 2022/2023. Barua pepe: info@heslb.go.tz

Je haya ndiyo majibu kuwa amekosa mkopo?
 
Halafu utaskia mama amewapa mikopo watoto 45,000 tofauti na mwendazake aliewapa watoto 29,000 tu 😂😂😂 mkopo wenyewe hata mimi naweza nikasponsa watoto 10 kwa hio hela 😅
 
Back
Top Bottom