Mwanachama Mkongwe wa CCM na TANU ajiunga na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanachama Mkongwe wa CCM na TANU ajiunga na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagamoyo, Aug 9, 2010.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,540
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  UTANGULIZI:

  Kwa muda mrefu nimeulizwa na baadhi ya Wananchi wa Wilaya yetu ya Ngara ni kwa nini sigombei ubunge wa Wilaya hii. Kila nilipoulizwa hivyo nilijibu kuwa mimi nimekuwa mbunge wa Ngara tangu nikiwa shuleni hadi sasa. Nimekuwa nikitoa mifano michache ifuatayo:

  Tarehe 4 Oktoba 1968 ilichapishwa kwenye gazeti la “ The Standard “ barua yangu kwa wasomaji iliyokuwa na kichwa cha habari “NGARA - A PART OF TANZANI ?” nikiuliza iwapo Ngara ni sehemu ya Tanzania. Katika barua hiyo nilieleza kuwa Wilaya ya Ngara imesahaulika kimaendeleo na kwamba kiasi cha kodi ya kichwa (Shs. 56/= kila mtu mzima kwa mwaka) kilikuwa juu kuliko Wilaya nyingine ya Tanzania. Aidha nilieleza masikitiko yangu kuwa mara kadhaa viongozi wa kitaifa walikuwa wanatembelea Wilaya za Bukoba, Karagwe na Biharamulo bila kufika Ngara.

  Mwezi Januari, 1969 niliandika barua nyingine kwenye gazeti hilo hilo. Barua hiyo ilichapishwa tarehe 31 Januari, 1969 chini ya kichwa cha habari ‘ANOTHER CRY FROM NGARA’ yaani kilio kingine kutoka Ngara. Katika barua hiyo ‘nilijiunga mkono’ kwa ile barua ya kwanza na kusisitiza kuwa Wilaya ya Ngara imetelekezwa na Serikali na wanasiasa, huku watu wakiumizwa na kiwango kikubwa sana cha kodi bila kuona maendeleo yanayotokana na kodi hiyo. Nilieleza kwamba hospitali chache zilizokuwapo wakati huo zilikuwa zinatoa huduma mbovu kutokana na kukosa vifaa na maawa ya kutosha. Nililalamikia pia huduma mbovu za posta ndogo ambayo wakati huo ilikuwa inatumika kutunza fedha huku ikishindwa kulipa wateja pale walipotaka kuchukua sehemu ya fedha zao.

  Ukiacha “uwakilishi” huo wa kwenye ujana, baada ya kuhitimu na kuanza kazi, mimi nimekuwa sehemu ya Ngara zaidi ya nilivyokuwa sehemu ya ughaibuni nilikokuwa ninafanya kazi. Kila mwaka nimekuwa nakuja nyumbani na kukaa na wananchi na pia viongozi wa Wilaya na kubadilishana mawazo juu ya maendeleo ya watu wetu.

  Sipendi kujisifia juu ya mchango wangu binafsi kwa Wilaya ya Ngara, lakini ni dhahiri kwa wote wanaonifahamu kuwa nimewekeza zaidi katika Wilaya hii kuliko sehemu nyingine yoyote. Kwa muda wa miaka 20 na zaidi nimekuwa nawekeza wilayani si pungufu ya Shs milioni 20 kila mwaka hivyo kuinua uchumi wa wilaya yetu na kutoa ajira kwa baadi ya watu wake.

  MCHANGO WANGU KITAIFA

  Pamoja na kwamba niliondoka katika utumishi wa umma kutokana na vitendo vya shari na kibaguzi vya baadhi ya viongozi katika serikali ya awamu iliyopita, mimi nimeendelea kutoa mchango wangu katika ujenzi wa taifa hili. Wengi mtakuwa mmesoma makala yangu katika gazeti la RAIA MWEMA mwezi Julai, 2010. Katika makala hiyo nilieleza kwa kirefu njia mbalimbali ambazo Serikali inaweza kutumia kupunguza matumizi ili kuboresha maslahi ya watumishi wake na pia kuongeza bajeti ya maendeleo.

  Hata hivyo baada ya uzoefu niliopata katika siasa za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani) wakati nikigombea urais wa serikali ya wanafunzi, nimekuwa mwoga wa kushiriki siasa za ushindani. Hii haina maana kwamba sijashiriki siasa za nchi hii. Kwa mfano mimi nilishirikiana nyuma ya pazia na wanasiasa wa kundi lililojulikana kama G.55 lililoshinikiza (bila mafanikio) kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika. Aidha nilishiriki vivyo hivyo nyuma ya pazia kwenye mkakati wa kuleta mageuzi yaliyolazimisha marekebisho ya Katiba ya nchi hii na kuruhusu mfumo wa vyama vingi.

  UANACHAMA WA CCM

  Mwaka 1976 nilijiunga na TANU nikiwa Chuo cha Chama cha Kivukoni na kupewa kadi namba E 735352. Kwa maana hiyo nilikuwa muasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya TANU kuungana na ASP mwaka 1977. Kadi hiyo hiyo iliendelea kutumika kama ya CCM baada ya kupewa Kumb. Na. B 321241.

  Tarehe 21 Julai 2010 nilifika hapa Wilayani Ngara si kwa sababu ya kupumzika au kufuatilia mchakato wa uteuzi wa wagombea wa udiwani na ubunge kwa tiketi ya CCM. Nililetwa na mapenzi yangu kwa Padri Marcel Bashaka ambaye alikuwa amelazwa hospitali na hatimaye kufariki na kuzikwa Rulenge juzi tarehe 3 Agosti, 2010. Hata hivyo nikiwa hapa Ngara sikuweza kujizuia kufuatilia kampeni zilivyokwenda. Katika kufanya hivyo nimeshuhudia uchafu wa kila aina katika mchakato wa wana-CCM kutaka kuteuliwa kugombea nafasi hizo. Uchafu huo ni pamoja na rushwa kwa viongozi na wanachama wenzangu ndani ya CCM. Mashindano ya nani anaweza kuhonga zaidi wakati mwingine yalikuwa yanachefua! Nimeshuhudia jinamizi la ukabila likirejea na kutumika kwa uwazi wa kutisha. Siyo siri kuwa sasa Wilaya ya Ngara imegawanyika katika vipande viwili na itachukua muda mrefu na umakini wa hali ya juu kwa watu wa Ngara kurejea kujiona kama familia moja badala ya kuwa Washubi au Wahangaza.

  Nimesikitishwa sana kuona wachezaji wa timu moja wakiraruana na kuvunjana viungo kabla ya kucheza na timu pinzani. Sina shaka tena kwamba mustakabali wa Chama changu na Taifa zima uko katika hali ya kutetereka. Nimepatwa na woga zaidi baada ya kugundua kuwa kilichotokea Ngara ndicho kimetokea nchi nzima. Tuliyoyaona katika nchi ya jirani ya Kenya wakati wa uchaguzi uliopita yanatunyemelea. Angalau wao wameweza kupata suluhu hasa baada ya kutunga katiba mpya. Sina hakika iwapo sisi tuko salama.

  HITIMISHO
  Kutokana na maelezo hayo hapo juu, Leo tarehe 5 Agosti 2010 nimeona ni vema nirejeshe kadi yangu ya CCM kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwa nina hakika kwamba uongozi wa CCM wilayani na hata kitaifa hauwezi kuipokea kadi hiyo kwa uwazi ninaoutaka kama ningeamua kwenda huko. Nimeomba viongozi wa CHADEMA hapa wilayani wanisaidie kufanya hivyo na baada ya hapo wao watanipima na wakiona kuwa ninafaa kuwa mwanachama wao wataniambia.

  Mungu Ibariki Tanzania

  Mushengezi J.J. Nyambele
  NGARA
  Source: mjengwa
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mushengezi anawafahamu sana viongozi wakuu wa CCM wa sasa kwani alikuwa nao JKT 'OPERATION TUMAINI" na pia CHUO kikuu UDSM class of 1975!! Uwezo wao anaujua kwani alikuwa pia kiongozi wa DUSO wakati huo!! Anaelezea rafiki yake wa karibu.
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mmmh, mwaka huu kuna mambo!
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Alikuwa Darasa moja na Muungwa kama ni miaka hiyo!
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hahahaha, inachekesha! Ila inaniuma haswa naposikia ukabila na udini vikiingia ndani ya kampeni, rushwa ndo kichefuchefu, Chadema wawe makini na hawa watu maana kuna wengine wanajiengua ccm kikazi. Karibu mwanachama mpyaaa tuendeleze harakati za kuikomboa nchi yetu.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Aliwahi kufanya kazi Idara ya Ushuru wa Forodha na baada ya kuanzishwa TRA alikuwa Corporation Secretary wake. Inavyosemekana alijiuzulu au alifukuzwa baada ya kukwaruzana na Mwenyekiti wa TRA wakati huo, Enos Bukuku. Mwenye data kamili kuhusu hili atueleze.
   
 7. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Huyu Bwana Mushengezi Nyambele ni mmoja kati ya waanzilishi wa TRA kwa kushirikia na Melikizedeck Sinare (RIP).Wao ndio walikuwa watu wa mwanzo ktk kushiriki na baadaye kuiunda TRA.Mwaka 2006 kwa kuutambua umuhimu wa Bwana Nyambele aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi serikalini Bw.Deogratias Ntukamazina alimuomba Nyembele mawazo kuhusu namna ya kuboresha Maslahi ya watumishi wa Umma,Bw.Ntukamazima ambaye kwa muda mrefu alikuwa Katibu Mkuu ofisi ya Rais Utumishi anafahamiana na Mushengezi Nyambele kwa muda mrefu.

  Tamko la Ndg Nyambele la kurudisha kadi ya CCM na kuchukua kadi ya Chadema ni maamuzi yake na ni moja ya njia sahihi ya kutumia haki yake ya kikatiba katika kuikuza Demokrasia.Ndg.Nyambele nafikiri amechukua kadi ya Chadema ili aombe wananchi wa Ngara kura ya kutaka kuwawakilisha Bungeni kwa kupitia Chadema.
  Katika Kinyang'anyiro cha kura za maoni ya Ubunge huko Ngara,ambako Bwana Nyambele analalamika kuwa kulikuwa na rafu za Udini,Ukabila na matumizi makubwa ya pesa, aliyeshinda ni Mtumishi mstaafu wa serikali Ndg.Deogratias Ntukamazina kwa kuwabwaga wagombea wengine Tisa akiwemo Mbunge anayemaliza muda katika Jimbo hilo Pro.Banyikwa.

  Pamoja na mambo mengine Bwana Nyambele ni mwanzilishi wa Ngara Jatropha Foundation,Foundation ambayo imepanda miti ya Jatropha katika maeneo mengi kwa lengo la kupata mafuta nafuu yaitwayo Jatropha curcas oil ambayo yanaelezwa kwamba ni bora kutumia kwa kuwashia stoves kwa sababu ya gharama nafuu na kuweka mazingira ya hewa safi.

  Wanachama wa Chadema watampima Ndg Nyambele na kuona kama atafaa kubeba Bendera yao kwa kuomba uwakilishi wa wana Ngara.Kwa mazingira aliyoyaona Ngara ni wazi atatoa Ushindani Mkubwa na hatimaye kuweza kuibuka na Ushindi mkubwa dhidi ya Mzee Ntukamazina.(kama atapitishwa na vikao vya mchujo vya CCM).
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,963
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Kama ni Nyambele wa TRA,this guy was sacked kwa madudu ya kitu kidogo na kiburi.Alifika mbali sana kwenye uongozi akalewa madaraka.Alikuwa akidai "kitu kidogo" kwa nguvu na usipotimiza ana kufix.Maisha yake hayajawa mzuri baada ya kutimiliwa TRA(Zamani Idara ya kodi na ushuru wa forodha)
   
 9. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Ndio Nyambele huyo wa TRA.
   
 10. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Good guy or bad guy,at least inasaidia kuwatikisa CCM.Na hapo bado mchujo wa kura za maoni.
   
 11. N

  Namaki Member

  #11
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  We Nyambele wadanganye wasiokujua,Fitina zote za ngara wewe ndio mwasisi wake,ulipandikiza mamluki wawili ukiwa nyuma ya pazia kama kawaida yako,kwanza mmojawao ni shemeji yako nyuma ya pazia, wote wamegalagazwa na Nuru mpya kwa maendeleo ya ngara,nawatahadharisha chadema kwamab wewe hufai na una kadi za vyama mbalimbali na kote hukubaliki,unabisha kwamba wewe sio mwanzilishi wa nccr mageuzi??? wewe pamoja na akina mvungi, marando na Bagenda ndio waasisi na kadi yako ni namba 6 au 7 sikumbuki vizuri ni lini umerudisha hiyo kadi!!!kama kweli una ubavu jipime ni wapi umewahi kugombea hata ukatibu kata ukashinda? sasa jaribu ubunge uone utakavyoaibika kama enzi zile Duso ulipolizwa na JK!!
  Waeleze watu pia TRA kwamba ulistaafishwa kwa manufaa ya umma, kwa skendo lukuki ikiwa pamoja na kuifanya TRA kama NGO yako,ukakimbilia mahakamani kuishtaki serikali na madai yako uchwala ukaishia kutupiwa vilago vyako na sufuria nje ya nyumba ya serikali uliokuwa unaishi pale oysterbay!!! wanangara wanayajua hayo si wanakuona kwenye vilabu vya pombe usiku kucha ukiwadanganya kwa kuipona serikali ya awamu ya nne kwa sababu ya chuki zako kwa JK toka enzi zenu chuo kikuu?
  Ndoa ngapi zimekushinda? mke wa kwanza ulimvuruga mpaka akawa kichaa, wa pili amekuwa alcoholic wa kutupwa na kazi yake amefukuzwa na alikuwa msomi wa sheria aliyebobea kuliko wewe yote haya wa kulaumiwa ni wewe na wala huoni aibu na sasa umeenda Burundi wasipokujua na kuchukua bint wa watu amakamu ya mwanao umeoa tena na umeshazaa naye mtoto umri wa mwaka mmoja sasa! kweli unataka wanangara wakuamini eti uwe kiongozi wao au uwachagulie kiongozi,inaingia akilini kweli?
  Bishop Nyamubi ameapa kuzunguka wilaya nzima kutangaza maovu yako ikiwa ni pamoja na kumtelekeza bint yake kipenzi anayekesha kwenye vilabu vya pombe kwa frustrations zako.
  Tuache wanangara tujipange tuendelee wewe umekwisha, umechoka,huna maadili mema usituvuruge asialni!
   
 12. M

  Msuruhishi Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Mchangiaji Namaki amemtaja mgombea wa jimbo la Ngara kana Nuru Mpya kwa maendeleo ya Ngara. Nilitegemea atuambie baadae kuwa NURU MPYA IMEFIFIA. Baada ya kushindwa kuanza kampeni kutokana na matatizo ya afya ya muda mrefu ya Bw. Ntukamazina, tulitegemea wananchi wa Ngara kuambiwa ukweli juu ya afya yake. Ukweli ni kwamba kazi ya ubunge haiwezi tena hata kama CCM wanahaha kumpitisha huku wakikampeini kwa kuonyesha picha yake tu.

  Aidha kashfa ya kutembea na mtoto mdogo wa Form I iliyotoka kwenye mtandao ni ya kweli. Jambo ambalo halikuelezwa ni kwamba mhanga wake huyo ni binti wa jirani yake waliosoma pamoja enzi za Middle school. Mimi nimefanya kazi chini yake pale Utumishi. Mwandiko ule haina shaka lolote kuwa ni wa kwake na haujabadilika tangu nimfahamu. Namba ya simu iliyowekwa ni ya kwake na imebadilika kuwa 0784. Si hayo tu, pale ofisini utumishi aliigeuza ofisi yake kuwa chumba cha kulala na wanawake na hata masekretari wake. Huyu ni FATAKI wa muda mrefu na ugonjwa wake wa mgongo unaweza kutokana na overuse!

  Mpaka sasa wanaomtetea kwenye mtandao hawamjui na kama wanamjua, ni makuwadi wake. Tungependa ajitokeze hadharani na kukanusha kama yeye siye mwandishi wa barua ile kwa kabinti kale. Tayari sisi tumekwisha kupeleka mwandiko wa barua ile kwa wataalamu na wamelinganisha mwandiko na dokezo la ofisini aliloliandika kwa mkono wake. Hakuna shaka. Akanushe hadharani halafu tuuthibitishie umma. Tutatoa ushahidi zaidi wa vetendo vyake vichafu kwa watoto wa marafiki zake waliomwamini ikiwa ni pamoja na mwanajeshi ndugu yake aliyefariki na kumwachia kuangalia familia yake.
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Hii ni kauli ya kiutu uzima:-

   
 14. NAWAPASULIA

  NAWAPASULIA Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyembele Mushegezi..................who is he?..............what is his role?.............sasa wewe bagamoyo unadhani habari hiyo ya Mushegezi inamsaidia vipi kuli wa pale bandarini Dar es salaam?...................kwanini unakuwa mjinga paka unapitiliza kiwango cha ujinga wa kawaida?....................kichwa yako ipo sawa kweli? au ina mdudu?.........unapaswa kujadili mambo yenye tija kwa taifa na sio kuendeleza propaganga mdumao...............remove your stupid crap from this forum
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Loh...!
   
 16. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,565
  Likes Received: 624
  Trophy Points: 280
  Taratibu wewe Chambio la Mafisadi.....
   
 17. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Taratibu jaribu kutumia lugha ya kistaharabu.
   
 18. NAWAPASULIA

  NAWAPASULIA Member

  #18
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I wonder if fool can speak a point,
  I wonder if fool have a point to say,
  I wonder if they use their common sense,
  speaking nonsense throughout their life
  ooh i wonder i wonder i wonder these fool want to be listened.
   
 19. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Data zake ninazo za kutosha! Let me digest!
   
 20. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaka Ni PA naona una data....sina tatizo na CHADEMA ila huyu lofa hawezi kuongoza watu, labda wanyama! All i need is a strong opposition in this country...but not through this idiot! Huyu ni ndumila kuwili na ndiyo hullka yake, divyo alivyozaliwa. Ni opportunist wa kutupa. Kipande cha shamba lao, baba yake aligawiwa na babu yangu, maana alikuwa mfanyakazi wetu sisi/babu yangu! Mnafiki mkubwa. Na huyo Mama wa Kirundi, alizalishiwa na Sebuyoya, wakiwa safarini kwenda Ngara, jamaa akawa anakula guest..si unajuwa Ngara kulivyo mbali! Alimpa amsindikizie..kumbe jamaa..na mzee mwenyewe ana ngoma! Patamu hapo!
   
Loading...