Mwana Mpotevu 'KULIKONI', Karibu tena Nyumbani!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwana Mpotevu 'KULIKONI', Karibu tena Nyumbani!.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Sep 3, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Wana bodi,

  Yule mwana mpotevu kwa jina la 'KULIKONI', (Gazeti), amerejea rasmi nyumbani asubuhi ya leo, kwa kumkuta amejibanza tena kwenye meza za magazeti, hivyo kuufuta ile dhana kuwa amepotea jumla, na huenda kaka yake 'THIS DAY' naye angemfuata baada ya kitambo kifupi.
  Karibu Nyumbani!.

  Hivyo hatuna budi kumkaribisha tena nyumbani, na kumfanyia kajisherehe kadogo hapa jamvini, ni hizi ni salamu zangu kwa mpotevu huyu.
  Karibu Nyumbani!.

  Kama mtakumbuka, kupotea kwa KULIKONI, kulifuatia kufungiwa kwa miezi mitatu kwa kuandika habari za 'GESHI LETU' ambazo zimekwenda kinyume cha ile sheria maarufu ya Magazeti ya mwaka 1976, na sheria ndogo ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1972 kuhusu mambo ya Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
  Karibu Nyumbani!.

  Kifungo hicho kilichoanza Januari 9 kingemalizika Aprili 9, hivyo Jumatatu ya Aprili 12 KULIKONI lilitarajiwa kutinga tena kwenye meza za magazeti, lakini ndio ilikuwa kimya mpaka leo asubuhi ambapo tahariri yake imesema "Tumerejea, tutaendelea kuanika uovu bila woga wala upendeleo".
  Karibu Nyumbani!.

  Nimesoma tahariri hiyo, haikueleza kilicholipoteza gazeti hilo zaidi ya kusema 'misuko suko ya hapa na pale', bila kufafanua ni misukosuko gani, hivyo kutoa uwezekano wa ile dhana ya 'mchacho', 'rumba kali' au 'mambo ya fedha', kupata uhalali wakati ile dhana ya 'kusalimu amri kwa mafisadi' kufutika rasmi kwa kurejea ulingoni.
  Karibu Nyumbani!.

  Bila kujali sababu zilizoipoteza KULIKONI ulingoni, swali linabaki ni Jee, KULIKONI limerejea kuendeleza ule moto wa kuwalipua mafisadi?, (ambao karibu wote wanapeta, na hivyo vikesi uchwala sasa hivi vitamalizika), ama limerejea kipindi hiki cha kelekea Uchaguzi Mkuu tuu ili likamilishe a particular mission, then off for good?!.
  Karibu Nyumbani!.

  Kwa vile 'KULIKONI' ni gazeti la ukweli na uwazi, na haliogopi kitu, tulitegemea baada ya kifungo, lingetoa japo statement kusema kile kifungo kimekuja as a blessing in disguise, infact wamepanga kukiendeleza wenyewe kwa raha zao na kutoa sababu, lakini hilo halikifanyika, na leo wamerejea bila kutoa sababu, lakini cha msingi hapa sio mwana mpotevu, alipotelea wapi au alikuwa wapi, bali amerejea nyumbani.
  Karibu Nyumbani!.

  Time will tell,
  Mwana Mpotevu, 'KULIKONI'..
  Karibu tena nyumbani!.
  Karibu Sana Nyumbani!.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hivi na lile la ACHA UMBEA limeenda wapi?
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  It is the story of an Alsatian being sent to the veterinarian.....for deteething....sorry mate halitakuwa kali tena with Mengi now in the bandwagon of Fisi-Hards :confused2::confused2::confused2:
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Limekuja kwa sura mpya, kwa hiyo yale mambo yaliyokuwa yanatolewa zamani labda sasa hatutayapata.
   
Loading...