Mwana JF umewafumbua wangapi?

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Wengi wapo kizani katika kiza kinene
Ukiwakuta mtaani wanapigana vijembe
katiba ya zamani huijui mpya waitakaje
wewe mungu kakubariki, umewajuza wangapi?

Humu JF hatukosi kujadili mada na hoja motomoto za kisiasa,kuelimishana na kukosoana pale tunapokuwa tumepotoka,lakini jambo jema zaidi ni kuwa wengi wetu humu jamvini japo si haba lakini tuna ufahamu wa nini kinachoendelea hadi kufikia kukijadili humu

Hoja yangu ama swali langu kwako mwana JF mwenzangu je nje ya ulingo huu umefanya jitihada gani au kiasi gani kuwafumbua waliopo usingizini?

Mahali pako pa kazi,nyumbani kwa wanafamilia,shuleni au Chuoni, katika sehemu za umma na usafiri wa umma,majirani na hata vijiwe vya burudani umejaribu kuwafumbua wangapi kwa kuwaeleza unachokijua ama unachojifunza humu?

Nimeshangaa kukuta vijana wakibishana mtaani kwa jazba walio wengi wakisema watz wanadai katiba mpya wakati ya zamani hawaijui!

hawajui kama wanaishi katika ubepari wakati katiba ni ya kijamaa!
hawajui tuna vyama vingi vya siasa wakati katiba inasupport chama kimoja!

ukiwapata wawili watatu kwa siku popote ulipo nina hakika tanzania ya kesho haitakuwa hii ya leo iliyojaa IGNORANCE

hebu jiulize umewafumbua wangapi??
 
Wengi hadi wengine wamenipa cheo cha information officer.

nakupa big up Husninyo...bado upo Dom? kama ni hivyo hao washikie bango kabisa maana baado somo halijawaingia huko,nadhani zile shamrashamra za kijani wakati wa mikutano zinawachanganya hawajui kama kuna the blues na the combatzz
 
Me meneja wa mawasiliano wa kijiji.
tena wewe village mawasiliano manager utasaidia sana maana kule watu hawaelewi..
ikija sinema inaonyeshwa ofisi za ...
ikija chanjo inafanyikia ofisi za...
akikamatwa mwizi wa ng'ombe anapelekwa ofisi za...
basi hao villagers wanadhani hiyo ndio serikali na vingine ni uasi
tusaidie meneja mawasiliano wa kijiji uwaambie zile ni timu tu kama simba na yanga,itakayosajili vema na kuwa ni viongozi na mipango imara ndio inastahili kushinda kombe!! sio ndumba,hongo wala fitna!
 
nakupa big up Husninyo...bado upo Dom? kama ni hivyo hao washikie bango kabisa maana baado somo halijawaingia huko,nadhani zile shamrashamra za kijani wakati wa mikutano zinawachanganya hawajui kama kuna the blues na the combatzz

hamna noma inko.
Huku bado hawajaisoma namba vizuri.
Wataelewa tu.
Karibu dom.
 
Mimi sipo bongo ila nimejitaidi kuwaelimisha wazazi wangu coz inaonekana wazee wengi bado wanakiamini sisiem lakini sasa ivi wameshaelewa ubaya wa sisiem, na ningependa sana JF kama tungewaelimisha wazee wetu kwanza ili 2015 kuwe na pigo kubwa sana kwa susiem!
 
Ngoja nikuendee pm then niwe boss wako....mkurugenzi wa mawasiliano wa kata. Hahaahaa!

ha ha ha ha!
Mabosi wenyewe siku hizi noma. Kuna sredi fulani hivi linalalamika ofisi za mabosi zina vitanda na mabafu.
Lol!
 
Mimi sipo bongo ila nimejitaidi kuwaelimisha wazazi wangu coz inaonekana wazee wengi bado wanakiamini sisiem lakini sasa ivi wameshaelewa ubaya wa sisiem, na ningependa sana JF kama tungewaelimisha wazee wetu kwanza ili 2015 kuwe na pigo kubwa sana kwa susiem!
hongera kwa moyo huo mkuu..wazee wengi wastaafu bado hawajalipwa mafao kutokana na kile kiitwacho ufinyu wa bajeti!! lakini Dwns watalipwa na wabunge waliostaafu august 2011 walishalamba mshiko wakaupigia na jaramba za kampeni!
haki ipo wapi? badala wale mafao yao wanasubiri kidogo unachopata mgawane uwatumie!! chao kinaliwa na wajiitao wajanja!
 
tena wewe village mawasiliano manager utasaidia sana maana kule watu hawaelewi..
ikija sinema inaonyeshwa ofisi za ...
ikija chanjo inafanyikia ofisi za...
akikamatwa mwizi wa ng'ombe anapelekwa ofisi za...
basi hao villagers wanadhani hiyo ndio serikali na vingine ni uasi
tusaidie meneja mawasiliano wa kijiji uwaambie zile ni timu tu kama simba na yanga,itakayosajili vema na kuwa ni viongozi na mipango imara ndio inastahili kushinda kombe!! sio ndumba,hongo wala fitna!

Mkuu....tenaona kuna kibaka sanamleta hapa bila ushabidi.......mi kazi yangu ni kutoa ushauri wa kiintelijensia....!
 
Lakini je ni kweli nyie ma-village information officer mnafikisha hizi informartion correctly?????
 
Lakini je ni kweli nyie ma-village information officer mnafikisha hizi informartion correctly?????

watu wanaogopa kusutwa,maana ukianzisha mjadala kijijini lazima usimame kidete kuufafanua vinginevyo utaonekana unawavuruga wananchi na mazoea yao ya zamani
 
ha ha ha ha!
Hata mimi kijiji kizima wananitegemea katika hilo. Lol!
Usiniulize kijiji gani.

Mie kijijini kwetu wananiita mchawi kujua yanayotokea dasalama kabla wao hawajajaua na mengi huwa nayapata humu sasa hivi na kabla sijajiunga rasmi!
 
Mie kijijini kwetu wananiita mchawi kujua yanayotokea dasalama kabla wao hawajajaua na mengi huwa nayapata humu sasa hivi na kabla sijajiunga rasmi!

lakini uchawi wako unawasaidia mkuu au ndo unafanya wakuogope??
 
Back
Top Bottom