Mwampamba Amjibu Dr Slaa

Mwampamba Amjibu Dr Slaa

Ndugu Mwampamba, yawezekana una hoja katika malalamiko yako na una nia nzuri tu kwa ustawi wa demokrasia hapa nchini. Lakini swali ambalo mm huwa najiuliza kila mara kwa nini mashambulizi yenu yote yanaelekea kwa Dr. Slaa? Je Dr Slaa ndio CHADEMA? Inawezekana vipi kama ww ni mpenda maendeleo na ustawi wa nchi kuna mambo mengi yanayofanywa na viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza kuelekea kwenye chi ya Neema ambayo yanenda kinyume na ni ya kifisadi, ungetumia nguvu kuyapigia kelele hata nusu tu ya hizi nguvu u(M)nazotumia mna(u)nazozielekeza kwa Dr Slaa, Hakika ningeku(wa)ona wa maana sana. Naomba mumuache Dr,
. Slaa kama mna ushahidi wa hizo tuhuma zenu zipelekeni kwenye vyombo halali vya chama mikiwa na ushahidi.
 
Jibu hoja ya msingi katiba ya cha inasemaje kuhusu pesa za chama.

Jamani mimi sihitaji kujitambulisha ni mshabiki wa chama gani ila thread zangu hapa JF zinaweza jibu hoja hiyo. Hapa JF panaonekana ni jukwaa la watu fulani ambao wamefuta ujinga. Tuache ushabiki, huu Uslaaism haujengi chama.

Hapa Mwampamba ametoa hoja kwa njia ya kuuliza maswali genuine. Binafsi naona Dr. Slaa mtu ninayemshabikia sana hapa amechemka. Mlioko kwenye uongozi tusaidieni grounds za kusupport Dr. Slaa kukopa na Josephine kulipwa akiwa anahudhulia kesi Arusha basi.

Na tunakoelekea wanachama wa chadema wataomba CAG awasaidie audit ya fedha za M4C. Sijui nao wataitwaje. Ni lazima CDM itofautiane na CCM si kwa maneno na sera tu bali hata kwa matendo na tabia za viongozi. Hii ya kuiga tabia chafu za CCM za kujitafunia hela za chama watakavyo isihamie CDM. Hapa kwa CCM ninaushahidi kuwa hela za parking ya magari kwenye zile open space walizojibinafsishia zinaliwa bila utaratibu wowote ule. Wa kunipinga hili alete hoja.
 
Huu ni ukosefu wa shukrani,hekima,adabu na staha.Kijana kama Mwampamba anawezaje kumwita Dr.Slaa 'mzinifu'? Semeni hoja za kujenga jamani...si majungu na matusi tu
vipi vijana wadogo kabisa kama ninyi mnaowaita baadhi ya viongozi wa nchi mafisadi! hizi bwana ni sifa haijalishi nani kasema. mfano kama mtu anafundisha kimsingi ni mwalilimu,kama mtu anasoma ki msingi ni mwanafunzi, kama mtu kafisidi kimsingi ni fisadi,n.k sasa suala la msingi ni kama kweli mtu kafanya kitendo husika? hapo ndipo kunakoweza kuwa na hoja.
 
Napata kigugumizi kuaminin kuwa huyu mwampamba haliwai japo kuwa pendo la kweli kwa kilichokuwa chama chake, na nashawishika kuamini alikuwa ni pandikizi napenda asome maneno haya kila pando asilopanda baba litang'oka,gugu hata likijifanya ni suke la mpunga ipo siku litang'olewa tu wapo wengi mithili ya mwampamba na wataibika na kupeperushwa toka CDM.
 
Mwapamba naona sera au siasa zimeshawashinda na ndugu yako makata lenu ni mmoja amueni mmoja msijee mkachelewa kama wachawi
 
Hivi kumbe pesa za CDM ni muhimu kwa ccm, kuliko mabilioni ya ufisadi ya viongozi wao!
 
Kutokana na mchango wake Chadema Dr Slaa anastahili kukopeshwa pesa nyingi zaidi na sio 20m/-. Kukopa pesa sio dhambi na wala sio ufisadi kama nyie vibaraka wa CCM mnavyo-suggest. Dk Slaa analipwa mshahara na Chadema, kwanini asiweze kukopa hapo kama sisi tunavyokopa sehemu zetu za kazi? Halafu mbona hamkitaji hicho kipengele kwenye katiba au kanuni kinachomzuia kiongozi au mwanachama mwingine kukopa fedha kwenye chama?
 
Jibu hoja ya msingi katiba ya cha inasemaje kuhusu pesa za chama.

Mkuu Ritz
Matokeo ya kuwa karibu na tutusa hata akili zako zitabadilika ni yaleyale tu matutusa! Yaani inaonekana ni jinsi gani Chadema ilivyo NGO vipi kina Matola nao wameambulia?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Jibu hoja ya msingi katiba ya cha inasemaje kuhusu pesa za chama.
Mkuu, si umwulize huyo Mwammpamba uliyemsifia kwamba ni kijana makini?

Binafsi ningemwona makini kama hoja zake zingeambatana na vifungu vya katiba, miongozo na kanuni za chama chao CDM zinazoonesha na kudhihirisha kwamba kitendo cha Dr. Slaa kukopeshwa hizo mil. 20 ilikuwa ni kosa na kwa katiba/kanuni na miongozo hiyo adhabu yake ni kadhaa.

Lakini kama vifungu hivyo hana, basi kwangu mimi huyo bwana ni debe tupu......., na nilipata kusema humu ndani ya JF kwamba huyu bw. ni kati ya wale wenye kisebusebu na kiroho papo. CDM ulishaondoka na uko huko uliko unakokupenda. Mambo ya CDM yanakuumaje?
 
Jibu hoja ya msingi katiba ya cha inasemaje kuhusu pesa za chama.

Wewe Ritz Nakuuliza swali dogo, ila halitazuia wewe kupata ujira wako wa leo kwa Nape.
Kipi kibaya zaidi - katibu wa CHADEMA Dr. Slaa aliyekopa fedha za chama kwa uwazi au kwa katibu wa MAGAMBA Kinana aliyeuza pembe za ndovu - nyara za serikali? Any way tunawashukuru kwa kuleta post za kumjenga Dr. kisiasa. Kwa maana kila kukicha ninyi ni kumuwaza na kutaja jina la Dr. Slaa tu, sidhani kama mnapata muda wa kufanya kazi zingine
 
MAGAMBA wamefilisi fedha na raslimali za hii nchi kiasi cha kuita mabilioni fedha ni vijisent. Ritz na magamba wenzake hawapigi kelele yeyote. Wanakomaa na 20m. Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza, ccm kila mti wanaojaribu kupanda sasa unateleza sasa. Hayawi hayawi sasa yamekuwa!!! Tanzania hatimaye imepata chama cha upinzani chenye nguvu na uwezo wa kutosha kuindoa CCM. HONGERENI SANA CHADEMA, kazi nzuri sana!!!
 
MAGAMBA wamefilisi fedha na raslimali za hii nchi kiasi cha kuita mabilioni ya fedha ni vijisent. Ritz, chama, Zemacorpolo na magamba wengine hawapigi kelele yeyote. Wanakomaa na 20m. Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza, ccm kila mti wanaojaribu kupanda sasa unateleza. Hayawi hayawi sasa yamekuwa!!! Tanzania hatimaye imepata chama cha upinzani chenye nguvu na uwezo wa kutosha kuindoa CCM madarakani. HONGERENI SANA CHADEMA, kazi nzuri sana!!!
 
Habari wanajamvi.
Imenisitua kidogo taarifa ya kamanda anaelekea kuacha ukamanda wake, hadi nimefikia hata kujiuliza kama alishawahi kufanya kazi mahali popote. Majibu ya ndg yangu yanaonesha kuwa hana uzoefu wa kutosha katika masuala mbalimbali.
1. Ofisi nyingi zinakopesha wafanyakazi wao, hata kama katika Kanuni zake za kuanzishwa hakuna kipengele cha namna hiyo
 
kukopa..!!!!!,watu wanaiba fedha za serikali

wanazificha uswisi,halafu wanamtuma kijana kupigapiga kelele bungeni
tutajuaje kama Katibu Mkuu wa Chadema kazihifadhi hizo 140/20mil Uswissi vile vile!
Maana ndo fasheni ya mafisadi ati!
 
Hbari wanajamvi
Napenda kuchangia kidogo kwenye hoja ya ndg yangu ambayo kama si mizengwe leo angekuwa Mbunge wa Mbozi

Kusema ukweli ndg yangu katika hoja yako hiyo umeonesha kuwa hauna uzoefu katika masula ya kazi na maofisini. ni dhahiri kabisa haujawahi kufanya kazi na kujua ofisi zina-operate namna gani:
1. Suala la mkopo; Ofisi nyingi huwa na utaratibu wa kutoa mikopo ya dharula kwa wafanyakazi wake ambayo mara nyingi hujulikana kama salary adavance, na salary advance haina riba kwa hiyo kukopa kwa Dr sidhani kama ni kosa wakati watu wengi katika taasisi zao hukopeshwa kwa utaratibu huo.

2. Unaposema sema kuwa kwa nini asikope NSSF au PPF kama Mbowe, Mbowe anachukua business loan, siyo salary advance. Japo sina u=hakika kama Mbowe amekopa au la, lakini ninachotaka kukutaarifu hapa kuwa, kukopa katika mifuko hii inategemea pia umechangia kwa muda gani, na mara nyingi mifuko hutoa mikopo ya nyumba kwa wateja wake na si ada za kusomesha watoto au vinginevyo.

3. Sioni hoja ndg yangu Mwampamba inayoweza kukufanya usimame kupitia hoja hiyo. Wale wenye uzoefu na kazi wanaona unafanya kitu cha kitoto, kisicho ma mashiko na chenye kuonesha kuwa huna uzoefu katika maisha.

4. Suala hili limenifanya nitambue kuwa hata wana Mbozi wangekuchagua hakika msaada wako kwao ungekuwa mdogo sana pengine hata wangejuta. Ladba ungepata uzoefu ukiwa Bungeni.

5. Nakushauri uachane na mabishano haya maana hayakujengi, yanakubomoa, mahala popote utakapohamia unaonekana wewe ni bomu, hauna tija, ni vyema utafuta njia ya kupata msaada zaidi, na ikiwezekana nakushauri uombe msamaha na utubu ili urudishwe kundini.


.
 
Mtamuua mzee wa watu kwa presha,mwenyewe alikopa kwa siri nyie mnayaleta hapa,shauri zenu

Watu wamefilisi nchi kuanzia BOT mpaka hazina na ufisadi bado ni mbele kwa mbele lakini hawafi kwa pressure zaidi ya Kuwa Balali halafu leo mtu afe kwa ajili tu ya mkopo!!!
 
NIWA


Wana JF nianze kwa kumba samahani kuchelewa kuchangia tangia jana kwa matatizo niliyojitakia mwenyewe kwa kukbali kuajiriwa badala ya kujiajiri. Muda ulikuwa kiduchu hivyo niendeleze thread hii mpaka leo. Nilipokuwa nafundishwa elimu ya dini ya Kikatoliki maarufu kama Kateksimu nilifundishwa kuwa anayejua mengi ataulizwa mengi. Naamini Mwampambwa anajua mengi maana amesoma mpaka ngazi ya chuo kikuu. Anapoamua kuandika kitu ni vizuri kiahakisi uelewa wake na kama anataka kuelezea ubaya wa kitu afanye hivyo kuonyesha ni kwa jinsi gani kile anachomtuhumu kimefanya jamii idhurike, iteseke na isononeke. Halafu aonyeshe pasipo shaka na jinsi yeye alivyodhurika na tuhuma hizo. Failure to show the magnitude of damage at individual and communal level makes the whole criticism a means to explode vendetta. Nimesoma majibu ya Mwampambwa yamekosa umakini wa uelewa na jinsi jamii au chama kilivyodhurika na tuhuma ya kukopa within the party. Na basi ili aonekane katumia chembe ya uelewa basi angetupatia na empirical study kuwa kiongozi wa jamii, taifa au chama fulani ndani na nje ya nchi aliwahi kufanya kinachofanana na hiki na akasababisha madhara. Lakini hakuna hata kitu cha aina hiyo. This is purely meeting trouble half way.

Pili haonyeshi ni lini kukopa pesa ndani ya chama imekuwa ni kosa la kulinganisha na ufisadi. Analalamikia taratibu, sheria na kanuni zisizokuwepo. Sasa malalamiko ya nini yasiyokuwa na basis. Bila basis in place everybody can fabricate things as long as the aim is implicate another person and put one's integrity in question. Ni ajabu tena kuona mtu wa aina hii mwenye kuibuka na vitu visivyokuwa na basis anapata mashabiki.Bado tunaweza kupoteza muda kwa kushabikia visivyokuwepo na tukaacha vikubwa ambavyo vimekosa mtu wa kuvisema the likes of EPA, Richmond, Rada ya kuongozea ndege, ununuzi wa ndege ya rais, waarabu wa Loliondo, mikataba ya madini, uchimbaji wa uranium, mikata ya gesi na bomba la gesi toka mtwara (nite majibu kwa wanamtwara hayajapatikana), Buzwagi, Meremeta na mengine.


Tatu, matatizo ya vyama huanzia ndani ya vikao rasmi vya vyama. Ni lini Mwampamba alipeleka dukuduku lake lijadiliwe ndani ya vikao vya vyama. Alete ushahidi kimaandishi ili tupime bila shaka kuwa alitenda kisomi na kiulewa ili hoja ikazimwa. Ilipozimwa alifanya nini. Kuna appeal organs. je alifanya hivyo. Maana kama kuna ufujaji wa pesa za ruzuku angeweza kwenda kwa CAG ili mahesabu ya CDM yakaguliwa au kwa msajiri ili CDM iwajibike. Alete ushahidi humu jamnvini na tutasema mengine. Short of that all said is a reflection of vendetta and power monger

Nne na ushauri huu nilimpa hata dada Shonza kuwa ukiwa umedhurika na maamuzi ya jamii au chama, kabla hujaenda public kujitetea kwanza fanya mambo manne;-

1. Mwombe Mungu akupe unyenyekevu katika utetezi wako- Lugha chafu, matusi na kejeli hata kwa mtu mdogo kiumri na kiutawala haina neema ya Mungu. Mwampama umekosa hofu ya Mungu. Kajute saa bado ipo.

2.Wakati na nyakati- Ulipaswa ujipe muda na ukajithathmini na uone kuwa mlichokuwa mnakifanya kiko sahii katika kanuni ya demokrasia ya magharibi yaani collective responsibility. Hii inataka mwende kwenye vikao vya ndani mbishane lakini mkitoka nje you are one hata kama mawazo yako hayakukukubaliwa au hukubaliana na mawazoya wengine. Hii ni kanuni ya demokrasia. Ukiona huiwezi basi wewe siasa si mahali pako tafuta kwingine. Hujajipa muda tangu ufukuzwe na sasa unaibuka na tuhuma. Watu makini hawawezi kukuelewa na chama makini hakiwezi kukuchukua nna kukupa madaraka nyeti maana wanajua hata kesho ukitoka utawatukana wakati maamuzi yalikuwa ni ya pamoja. Tena nakushauri kuwa better satan you know thean God you don't. Ni afadhali ukakaa kwanza halafu kesho ukaenda kwa wale voingozi wa CDM uliowatuhumu na kuwatukana ukaomba msamaha kuliko chama kingine maana huaminiki tena.
3. Maandishi (documentation) ni muhimu tena zenye rejea inayoweza kuwa accessed na watu wote na si za kughushi. All said by you and your compatriots are short of documenation hence they lack good trck records and remin to be outdate lies and fabrications.
 
Back
Top Bottom