Tatizo siyo kumsikiliza Mwampamba tatizo kwa nini Dr Slaa akope pesa za ruzuku katibu ya Chadema inasemaje.
acheni ----- wenu nchi ina mambo mengi ya maana ya kujadili au ndo mnatumika!!!
Sidhani kama Kukopa tafsiri yake ni kuiba. Kukopa maana yake urudishe kwa wenyewe na kupora maana yake kiwiziwizi.
mkuu upo? habari ya leo?
katiba ya chama chochote inataratibu zake, kuhusu hili
1. Katiba inasemaje ya chadema? maana sisi wengine mtufumbue macho.
2. Kutokana na jibu la 1 utaratibu umefutwa kuwakilisha malalamiko panapohusika kama upo na nani kawasilisha, kama haujafuatwa nini mtazamo wako, tuite haya majungu au uzushi? au malalamiko yasiyo rasmi
Kukopa sio kuiba ndugu yangu ila kama utaratibu haukufuatwa hapo ndipo penye tatizo.
Nipo kama unavyoona. Hebu nirushie katiba na financial policies za CHADEMA kama zipo karibu hapo tuangalie taratibu za kukopa kama zilifuatwa.
Mkuu Freshthinking.
Kwanza hongera kwa kuona kuwa matusi haya kubaliki hasa kwa kijana kumuita mtu aliye kuzidi umri majina yasio faa! Hii ni kinyume na mila na desturi za kijana wa kitanzania.
1. Katiba za vyama vingi hazina kanuni au sheria za kukopesha au kukopeshana, cha msingi tambua kuwa kutokuwepo kwa kanuni au sheria za kukopeshana hakuondoi uhalali wa mhusika kuomba mkopa au kukopeshwa kama kuna makubaliano ya kimaandishi au yaki ofisi na utayari wa kutoa mkopo huo kwa mhusika.
Ndio maana nikasema aachwe apige kelele na kutukana akichoka ataenda kulala.
Mwampamba kweli wewe ni kijana makini majibu yako ni kisu kwa Dr Slaa na wafuasi wake wote.
Utaratibu upi haukufuatwa. Mwampambaism? Umeambiwa kwenye katiba kama mpaka kukopa na kukopeshana kutakuwepo basi hiyo siyo katiba maana itakuwa inabeba kila kitu. Sasa kama unafikiri kuna utaratibu ulikiukwa mbona husemi au mbona mtoa tuhuma hasemi. Katiba iko silent na labda utaratibu haukuwepo wa kukopeshana. Sasa kwakuwa haukuwepo mwenye shida asipate mkopo. Kila kitu kina mwanzo kama haukuwepo basi ulianza na Dr. Slaa na mweingine akitaka mkopo kama pesa ipo ni kuwekeana makubaliano ya kurudisha katika wakati mwafaka.
Ritz, hatujui yanayoendelea CCM na vyama vingine kwakuwa wao mambo yao wanayafanya kwa usiri mkubwa sana. Hivi unafikiri mabilioni kwa mabilioni wanayokusanya CCM kutokana na miradi waliyopora kwa wananchi (viwanja, ofisi, na kumbi) wanayatumiaje? Je unajua CCM wanapokea kiasi gani cha ruzuku kila mwezi? Je wanafanyia nini? Kinachowasaidia hawa wenzetu, ni kwamba mambo yao hufanywa kwa usiri mkubwa. Mtu mpuuzi kama Mwampamba hapati nafasi ya kujua kinachoendelea humo ndani. Uwazi wa CHADEMA katika utendaji wa mambo yao ndiyo unaowafanya wafike mahali wasakamwe kiasi na wachumia tumbo kama akina Mwampamba.Jibu hoja ya msingi katiba ya cha inasemaje kuhusu pesa za chama.
Endelea kuwadharau vijana wa vijiweni lakini kumbuka hao ndiyo wapiga kura.
hauna hoja! labda chuki unayo .kwa jinsi ambavyo dokta amejitolea kujenga chama na kwa status yake(rais wa mioyo ya watanzania) kumkopesha m 20 ni kumuonea ingefaa wampe tu mzee wetu amalize yaliyokuwa yanamkabili basi.You are shootingi in the dark boss!