Mwamke aliye kwenye ndoa ya Kiislam akabadili dini anaweza kudai talaka?

mlaki mlaki

New Member
Dec 23, 2022
4
2
Naomba msaada juu ya hili.

Je, mwanamke aliyeolewa Kiislam akaja kutengana na mumewe na kubadili dini je ndoa itakuwepo paka atakapodai talaka au ndoa itafika mwisho.
 
Naomba msaha juu ya hili je mwanamke alie olewa kiislam akaja kutengana na mumewe na kubadili dini je ndoa itakuwepo paka atakapodai talaka au ndoa itafika mwisho
Ndoa ni mkataba wa kisheria kati ya mwanaume.na mwanamke ili waishi kama mume na mke, sheria ya mkataba huo inaweza kuwa ya kidini, kimila au ya kiserikali.

Talaka ni hati inayotolewa na mume au chombo husika kama taarifa ya kusitisha ndoa na hati hiyo anapewa mwanamke aliyeachwa.

Ndoa inapovunjika talaka ndio Uthibitisho kwamba ndoa imevunjika, talaka ni kama risiti ya kuthibitisha kwamba umenunua bidhaa ya aina fulani kwa gharama fulani kutoka duka fulani.
 
Na je mwanamke akidai talaka na mume akagoma kuitoa ingali mwanamke sidini yake tena ndoa itaendelea
 
Kwani kubadili dini ndio kigezo cha kuvunjika kwa ndoa??

Hata kama kabadili dini huyo kisheria bado ni mkeo na ili asiwe tena mkeo yakupasa uumpe talaka.

Talaka ndio cheti cha kuthibitisha kwamba huyo sio tena mkeo na mambo ya kubadilisha dini hayahusiani na talaka kwani hata kama kabadili dini kisheria huyo bado ni mkeo na itaonekana bado hujamuacha kwakuwa hujampa talaka.

Hebu geuza picha hiyo kwa upande wa pili; kwa mfano wewe ndio umebadili dini je huyo mkeo moja kwa moja anakuwa sio mkeo?? hapana hawezi kukoma kuwa mkeo ni hadi adai talaka na wewe uumpe talaka hapo ndio ndoa inakoma.

Narudia tena kama kuna cheti cha ndoa kinachothibitisha ndoa hivyohivyo talaka ndio cheti cha kuthibitisha kuvunjika kwa ndoa, kwa maneno mengine talaka ni cheti cha kubatilisha cheti cha ndoa, kama yeye anadai talaka na wewe UMERIDHIA kumuacha huyo mwanamke basi mpe talaka yake.

Au mwambie yeye ndiye akupe talaka (inaitwa khula) ambayo katika sheria ya kiisilamu yeye itabidi akurudishie mahari uliyompa.
 
Naomba msaha juu ya hili je mwanamke alie olewa kiislam akaja kutengana na mumewe na kubadili dini je ndoa itakuwepo paka atakapodai talaka au ndoa itafika mwisho
Kuna Dada mmoja Mkoa wa kusini aliolewa na Me Muislam akazaa naye Mtoto, baada ya miaka miwili tu ndoa chali na mwaka wa 3 akakacha ndoa.

Baada ya miezi 9 akiwa home kwao akapata Me Mkristo akaolewa naye na sasa wana mwaka wa 5 wakiwa wana Mtoto mmoja wa kiume.

PICHA KAMILI:

Ke anapitia changamoto ya kubaguliwa na Wazazi, Ndugu zake na ametengwa kabisa kwenye ukoo sababu tu ya kuolewa na Mkristo lakini Ke kakaza kuwa liwalo na liwe ataenda kujibu kwa Mungu ila amani ya roho ina nafasi kubwa sana kwake kimaisha katika ndoa kuliko kuendekeza dini na Ndugu.
 
Je alipewa talaka?
 
Kwani kubadili dini ndio kigezo cha kuvunjika kwa ndoa??

Hata kama kabadili dini huyo kisheria bado ni mkeo na ili asiwe tena mkeo yakupasa uumpe talaka.

Talaka ndio cheti cha kuthibitisha kwamba huyo sio tena mkeo na mambo ya kubadilisha dini hayahusiani na talaka kwani hata kama kabadili dini kisheria huyo bado ni mkeo na itaonekana bado hujamuacha kwakuwa hujampa talaka.

Hebu geuza picha hiyo kwa upande wa pili; kwa mfano wewe ndio umebadili dini je huyo mkeo moja kwa moja anakuwa sio mkeo?? hapana hawezi kukoma kuwa mkeo ni hadi adai talaka na wewe uumpe talaka hapo ndio ndoa inakoma.

Narudia tena kama kuna cheti cha ndoa kinachothibitisha ndoa hivyohivyo talaka ndio cheti cha kuthibitisha kuvunjika kwa ndoa, kwa maneno mengine talaka ni cheti cha kubatilisha cheti cha ndoa, kama yeye anadai talaka na wewe UMERIDHIA kumuacha huyo mwanamke basi mpe talaka yake.

Au mwambie yeye ndiye akupe talaka (inaitwa khula) ambayo katika sheria ya kiisilamu yeye itabidi akurudishie mahari uliyompa.
Na je kama mwanaume alitoa Mali kwa wazazi na hakulipa Mahali kwa mke inawezekana mwanamke akimpa talaka kumlipa ingali mwanamke hakupokea Mahali yake
 
Hapa mimi sijakuelewa.

Hata hivyo; kwa mujibu wa sheria ya.ndoa ya kiisilamu mahari inayotolewa na muoaji huwa ni mali ya muolewaji (mali ya mke) na wala sio mali ya Baba au mama au hata mtu yeyote mwingine, sasa kama mahari walipokea watu wengine na wakaila hiyo wewe sio juu yako.

Kwakuwa mke ndiye aliyebadili dini na ndiye anayetaka umpe talaka basi wewe kwa maoni yangu inatakiwa umdai khula (yaani talaka anayotakiwa akupe wewe kuonyesha kwamba wewe sio mume wake) na aambatanishe na mahari uliyomtolea kipindi unamuoa ili hiyo mahari kama unataka uweze kwenda kuoa mke mwingine.

Yeye si ndio kabadili dini halafu tena anadai umpe talaka!!!?--- vipi mahari uliyomtolea iende na maji ??!, kama utaamua umpe talaka ni sawa kwani hayo ni maamuzi yako lakini kama ukimlazimisha yeye ndiye aandike khula na akaandika hapo ndoa itakuwa imevunjika na itambidii akulipe mahari yako uliyomtolea.
 
Naomba msaha juu ya hili je mwanamke alie olewa kiislam akaja kutengana na mumewe na kubadili dini je ndoa itakuwepo paka atakapodai talaka au ndoa itafika mwisho
hakuna Ndoa hapo,hivyo Muhanga (victim) hapo itabidi afunge kesi mahakamani kwa ajili ya kupata talaka sababu ya mwenza kubadilisha lini ambayo siyo dini aliyokuwanayo/waliokuwa nayo kipindi cha kufunga ndoa,hii ni kwa mujibu wa Kifungu 107(2)(i) ya Sheria ya Ndoa ya Sura ya 29 Iliyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2019,karibu PM kwa msaada zaidi
 
Naomba msaada juu ya hili.

Je, mwanamke aliyeolewa Kiislam akaja kutengana na mumewe na kubadili dini je ndoa itakuwepo paka atakapodai talaka au ndoa itafika mwisho.
Ndio. Kubadili dini kwa mmoja wa wanandoa ni kigezo kimojawapo kisheria kinachopelekea mahakama kuvunja ndoa.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom