Mwambieni Millard Ayo hii timu haiitwi Man U

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
967
1,693
Kwa media ama Public figure ambayo ina fuatiliwa na kuamiwa na waTanzania wengi kama hii ya Millard ayo huwezi kutegemea kuona mambo ya ajabu kiasi hiki yanafanyika! hata kama kipaumbele chake sio soka sio hivi anaboa.

Na kama kipaumbele sio soka basi aachane na kuposti vitu ambavyo hajui au hana ufahamu navyo

Kui ita Manchester United MAN U ni sawa na Media kuposti ikiita clabu za Simba na Yanga UTO,MAKOLO,KIDIMBWI au MBUMBUMBU.

Inashangaza na inamaana haoni hata media kubwa za huko duniani wanatumia ufupisho wa MUFC ,MU, MAN UNITED haoni?

Sio sawa kabisa kuita MAN U ni fedhea kubwaaa

Moja kati ya kumbukumbu mbaya zaidi kwenye historia ya soka la England na jiji la Manchester ni ile ajari ya Munich iliyo poteza zaidi ya asilimia 90 ya wachezaji wa kikosi cha kwanza Wakiongozwa na alie kua kocha wakati huo Sir Mats Busby ...

Kila mwaka tarehe kama ile hufanyika maadhanisho ya kuwakumbuka mashujaa wale ..

Baada ya ajari Mechi ya kwanza iliyo ikutanisha Man united na mahasimu wao wa jadi Liverpool
Mashabiki wa Liverpool wali kua wakizomea na kuimba
"sir Matts Babies are gone and they shall never come back they have rotten and become Manure....man your manure man your manure ....""

Wakimaanisha watotowa sir Matt wameondoka na hawatorudi tena ameoza na wame kua mbolea....man ni mbolea man ni mbolea ""
Watotobwa Sitt Busby na wale wachezaji walio Poteza maisha kwenye ajari ya Munich

Baada ya muda wakaja wapinzani na mahasimu wengine Leeds united wao wakaiga huo wimbo na kuuboresha kidogo kwa namna yao
Waliimba
"man your manure man you manure ....man u man u ..man u ..."

Tangu hapo ikawa ndio wimbo MAN U ulitumika na vilabu kama kudhihaki timu ...ulitumika kudhihaki na kutonesha kidonda cha kumbukumbu hii mbaya kwa timu na soka kwa ujumla.....

Mamlaka ya nchi na chama cha soka cha Uingereza FA wakapiga marufuku matumizi ya Neno MAN U kwa vyombo vya habari na mashabiki ...

Ndio mana ufupisho unao tumika sasa ni MUFC ,MAN UNITED,MU...ila sio MAN U

ni jambo la ajabu sana na la fedhea kuona public figure kama millard ayo yupo tu ana fedhehesha.

FB_IMG_1633192059115.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom