Abramovicha amualika Mourinho dinner baada ya mechi ya leo Man U vs Chelsea pale Darajani.

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
2,326
1,314
Leo majira ya jioni kwa saa za Nairobi, kutakuwa na kipute kikali cha soka baina ya Man United na Chelsea.

Lkn mbali na hicho mmiliki wa Chelsea amemualika boss wa Man United Mourinho kwa ajili ya dinner baada ya mechi ya leo.

Ikumbukwe Mou aliwahi kusema Mmiliki wa Chelsea sio rafiki yake wa karibu bali walikuwa na mahusiano wa mmiliki - meneja na wala si zaidi. Mmiliki huyo alishawahi kumuajiri Mou mara mbili na kumfukuza mara mbili, mara ya mwisho ilikuwa Oct 2015. Hata hivyo Mou ndio kocha mwenye mafanikio makubwa kwenye club ya Chelsea na ndiko alikopatia jina la 'The Special One'.

Antonio Conte boss wa sasa wa Chelsea yupo kwenye wakati mgumu baada ya kugongwa 3 kwa 0 na club ya Italy AS Roma kwenye champions league. Mbali na hilo Chelsea ipo nafasi ya 4 na Man U nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza huku Man U wakiwa nafasi ya 1 kwenye champions league.
 
conte kosa lake ni moja tu kumtimua DIEGO COSTA kipenzi cha tajiri sababu nyingiiii na ngonjeraaa zitaletwa lakini tajiri hakutaka costa aondoke
 
Conte leo ndo mwisho wa kibarua,nasubiri jinsi Rashiford atakavyowagalaza hawa Chelsea.
34760af6ff7bd7d45ab657825f18cc36.jpg
 
Back
Top Bottom