Nasikia harufu ya damu Man United vs Real Madrid

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
NANUSA HARUFU YA DAMU.... MAN U vs REAL MADRID
maxresdefault.jpg

Baada ya Manchester United kupata matatizo ya "Munich Air Disaster", Real Madrid ilikua timu ya kwanza kujitoa kujaribu kuisaidia kifedha na kutaka kuwatoa wachezaji wake wa tano akiwamo gwiji ALFREDO DI STEPHANO, Do Stephani alikua ndo Mchezaji bora kwa wakati huo huenda ukilinganisha na wakati huu labda wangemtoa Cristiano Ronaldo. Kwa Miaka kadhaa kumekua na urafiki chanya baada ya tukio lile kiasi Man United waliwauzia Real Madrid wachezaji wake Wengi tu kwa Mfano beki Gabriel Heinze kwa ada ya Paundi 6M tu, Huku Liverpool walikua wanataka kutoa Zaidi ya Paundi 9M, David Beckham alipelekwa Real Madrid ilihali alishafanya mazungumzo binafsi na Barcelona, Ruud Van Nisterlooy tena aliondoka akiwa Mchezaji Muhimu kabisa ndani ya Manchester United, Javier Hernández "Chicharito" aliyepelekwa kwa Mkopo mwaka 2014 baada ya Forward line ya Real Madrid kuhitaji mtu wa kum-back up Karim Benzema, No ule Usajili Mkubwa wa Cristiano Ronaldo licha ya kwamba Uligharimu pesa ndefu lakini United ilimuachia kwa Roho safi kabisa

Maisha yalianza Kubadilika mara baada ya Real Madrid kumtaka Moja kati ya Makipa bora kabisa Duniani anayecheza Manchester United, I Mean David De Gea, Man United hawakutaka kumuuza na waliliweka hilo wazi, Ingawaje kulikua na Ushawishi mkubwa na pressure kubwa kutoka kwa De Gea mwenyewe lakini iko wazi kwamba Real Madrid Waliforce sana dili la De Gea. Kuna kipindi ililipotiwa kwamba waliongea na wazazi wa De Gea waweze kumshawishi mwanao, wakamtumia hadi Mchumba wa De Gea mrembo Edurne ambae ni Mwanamuziki anayefanyia kazi zake pale kwenye Jiji la Madrid, hili lilifanikiwa kwa namna flani ingawaje De Gea alishaanza taratibu ku-develop Mapenzi yake kwa Man United tukasikie kuna kipindi alijaribu kuondoka, Ingawaje mambo yalienda sawa na Man United wakendelea kusisitiza Msimamo wao wa kutomuachia David kuna kipindi ilikaririwa kwamba Usasajili wa De Gea umekamilika Ila United wamecheelewesha kwa makusudi Fax ya De Gea kwenda Real Madrid na usajili ukashindwa kukamilika, kitu kilichoonekana ni ushindi kwa Man United na ni Loss s kwa Real Madrid. Baada ya Porojo zote kupita David De Gea alisign mkataba mpya Ndani ya Manchester United, Mkataba wa Miaka 5

Maisha yakaendelea kwa Real Madrid kua kinara wa Club zote ndani ya Uwanja huku Manchester United ikipata mafanikio makubwa na kua kinara wa Club zote nje ya uwanja hasa kwenye swala la Promotion na Biashara na waka wapiku Real Madrid kama Club yenye thamani kubwa duniani kwa sasa.
Kuna kipindi Man United ilikosa mvuto kabisa hasa baada ya kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, Hivyo ilihitaji Baadhi ya World class players kitendo kilichowafanya kugonga kwa Ndugu zao Real Madrid kuhitaji huduma ya Angel Di Maria, huyu Madrid walitaka Paundi 60M huku man u wakitaka kutoa 50M mazungumzo yalienda vizuri na Man U walikubali yaishe wakatoa Paundi 59.7M.

Baada ya miaka kadhaa Man United wakagonga hodi tena kwa Ndugu zao Real Madrid sasa hvi wakihitaji huduma ya Alvaro Morata na james Rodriguez ingawaje Jose Mourinho hakuthibitisha bid ya James. Kwa Morata Madrid walitaka Paundi 70M kwanza Man United wakatoa Paundi 60M, ikakataliwa na huku mazungumzo yakiendelea Madrid walipandisha na kutaka Paundi 79M huku man u wakiishia Paundi 65M dili ikagoma kwani Real Madrid na Frolentino Perez wao walikua na kisasi kwenye Ishu ya De Gea. Man United kuamua kumgeukia Lukaku waliemnunua kwa £75M ambayo United walikua radhi kuipa Madrid kwenye Usajili wa Morata.
Kwa James Rodriguez, Real Madrid hawakuonesha nia ya kumuuza moja kwa moja kama United walivokua wanataka na wakampeleka kwa mkopo Bayern Munich na wanauwezo wa kumnunua Paundi 35M tu ila sidhani kama hii ndo bei ambayo Man United wangeambiwa. No ni jana tu Iliripotiwa Club ya Chelsea imefikia makubaliano na Real Madrid kwenye usajili wa Alvaro Morata kwa £75M, bei ambayo Man United walikua radhi kulipa kabla hawajapandishiwa.

Baada ya drama hizo zote wiki iliyopita niliskia kumetokea Movie nyingine tena, Hii ni ya kugombea Uwanja wa mazoezi timu zote zikiwa kwenye Pre Season i nchini Marekani.
Huu ni muendelezo wa Ushindani, Ujeuri na Kukomoana unaoendelea baina ya timu hizi huenda De Gea alitaka ah anataka kwenda Real Madrid, ah Morata alikua anataka kwenda Man United ila kutokana na Ujeuri unaoendelea baina ya timu hizi Mbili Uhamisho wao Ulikwama.

Kabla ya Msimu huu wa 2017/2018 kuanza kuna mechi mbili zitapigwa kati yao, Ile ya Kirafiki kule Marekani iliyopigwa 24 July, na ile kubwa ya UEFA Super Cup.

Sipati picha huo Ushindani utakaokuwepo hasa kwenye Super Cup. Nachokiona Ni Harufu ya Damu Tu.
14965608581405.jpg


VS

129892118_Getty-Images-Europe_Ajax-v-Manchester-United-UEFA-Europa-League-Final-xlarge_trans_NvBQzQNjv4BqM37qcIWR9CtrqmiMdQVx7D-C4Ci08c-Zomr4p6x2cCw.jpg


Leo nampa man united ushindi wa 4 kwa 0
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom