Mwambieni Magufuli, Nimekasirika!

Mwambieni Magufuli, Nimekasirika!

Kibarua hiki mnacholipwa kuandika upuuzi na propaganda dhaifu kama hizi mmeshafeli na mnazidi kukididimiza Chama Chenu. Watanzania wa sasa sio wale mliokuwa mnawahadaa kwa Operation na movements zisizo na faida

Ila kutuhadaa kwa makelele yenu na mitusi yenu majukwaani sema kafanya lipi
Ajira ziko wapi
Elimu iko wapi
Mikopo iko wapi
Sana sana kuna kesi kibao za madai
 
Mimi ni nani? Mimi ni raia wa kuzaliwa na mzalendo kwa nchi yangu Tanzania, Na ninakiri kwamba pamoja na kwamba sio "wa chama kile" lakini nilimpigia kura yangu yangu kwa kuamini kwamba misimamo yake ya kusimamia katiba ingeisaidia hii nchi, (Nilikosea). Nimekasirika maana sikumchagua kufanya haya anayoyafanya sasa hivi ya kufanya neno lake ndio liwe katiba, Tafadhali Mwambieni.

Nimekasirika, kuona kwa sababu ya chuki zake binafsi na "Wawekezaji Wale" Watanzania wenzangu maelfu kwa maelfu wameachishwa kazi na kila kukicha makampuni yanaendelea kutangaaza kupunguza wafanyakazi na hata ambao bado wapo makazini hawajui kesho itakuwaje, Mwambieni sikumchagua kwa ajili ya kufanya hayo. Nilimpigia kura yangu ili aweke mazingira ya hao wenye nacho watengeneze ajira zaidi kwa watoto wetu, Nilimchagua atengeneze mazingira walau maisha yangu nami yainuke kidogo walau yawakaribie hao wenye nacho.

Nimekasirika, Binti yangu aliyesoma na kuhitimu chuo kikuu ualimu wa masomo ya arts na ambae nilimsomesha kwa mshahara wangu mdogo wa kazi yangu niliyoipoteza ya ulinzi kwenye kampuni la "Yule Mhindi" hajapata kazi tangu mwaka 2015. Wamerundikana mtaani na vyuoni bado wanaendelea kutengenezwa wengine, Nilimsomesha nikijua akimaliza ajira yake ni moja kwa moja serikalini na hivyo ndivyo ilivyokuwa, Si mngesema tangu awali kwamba ajira kwa hawa watu hazitakuwepo akasoma kitu kingine?

Mwambieni nimekasirika yeye kujifanya ndio Mungu, kuona kwamba yeye anajua kila kitu, Mwambieni kiongozi husikiliza, Nchi yetu hii ambayo watu wengi hawajui wanataka nini inahtaji kiongozi anayesikiliza maoni hata ya wachache wenye akili. Muulizeni kwanini anawachukia upinzani? Kama wanampa mawazo ya kujenga kwa nini anawachukia? Kwanini kuwakamata kamata kila siku kama vile wamekuwa maadui kisa tu wanaikosoa serikali? Nilitegemea angewasikiliza, na ambayo yanafaa angeyafanyia kazi kama hayafai angetoa majibu kwa hoja kwa nini hakubaliani na mawazo yao. Sio hivyo anavyofanya kuwachulia kama ni maadui wa serikali.

Mwambieni nimekasirika na mtaani kwetu watu wengi wana hasira. Mwambieni asipofanya jambo hawa watu anaofikiri hawana akili mwaka 2020 watamkataa, na akilazimisha ataelewa "Panya akikasirika anakuwaje". Mwambieni hajachelewa, akae ajitafakari upya, aanze upya.

Kama ulimpigia kura, endelea tu kuisoma namba, si afadhali ungempigia hiyo kura hata Kingwendu?
 
Mnapoandika upuuzi wenu, mue pia mnataja na vifungu vya sheria anavyovunja, kwa maana ya ibara. Na sio mtindo wenu wa kipuuzi wa ku generalise habari

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni nafuu dunia ingekuwa na ma-Lucifer wengi kuliko nyie idiots wa Lumumba! Mmemfanya huyo mtukufu Sizonje/Pogba kuwa mungu wenu!
 
Kibarua hiki mnacholipwa kuandika upuuzi na propaganda dhaifu kama hizi mmeshafeli na mnazidi kukididimiza Chama Chenu. Watanzania wa sasa sio wale mliokuwa mnawahadaa kwa Operation na movements zisizo na faida
Unafikiri wewe unapolipwa kwa kushangilia kila aina ya upuuzi hata ule unaoathiri maisha yako mwenyewe, na wengine nao wanalipwa kulaani huo upuuzi?
 
Waliomchagua wanalaana ya kwanza kupita Magufuli mwenyewe.
 
Back
Top Bottom