yamungu joshua
Member
- Nov 17, 2016
- 29
- 14
Ukosahihi kaka
Kamwambie ataje kifungu kinachozuia kufanya siasa/kusema.Mnapoandika upuuzi wenu, mue pia mnataja na vifungu vya sheria anavyovunja, kwa maana ya ibara. Na sio mtindo wenu wa kipuuzi wa ku generalise habari
Sent using Jamii Forums mobile app
Naamini hujaandika kwa niaba ya Watanzania. Ni kwa niaba ya familia na chama chako.Kibarua hiki mnacholipwa kuandika upuuzi na propaganda dhaifu kama hizi mmeshafeli na mnazidi kukididimiza Chama Chenu. Watanzania wa sasa sio wale mliokuwa mnawahadaa kwa Operation na movements zisizo na faida
Si mpaka awe na listening skills ndo aweze kusikiliza na àwe na Good communication skills ndo aweze jibu kwa hoja na kushawishi.Bàhati mbayà sàna amenyimwa uwezo wa kusikilizà,kushawishi na kujenga hoja zinazoeleweka si kwa kiingerezà wala kiswahiliMimi ni nani? Mimi ni raia wa kuzaliwa na mzalendo kwa nchi yangu Tanzania, Na ninakiri kwamba pamoja na kwamba sio "wa chama kile" lakini nilimpigia kura yangu yangu kwa kuamini kwamba misimamo yake ya kusimamia katiba ingeisaidia hii nchi, (Nilikosea). Nimekasirika maana sikumchagua kufanya haya anayoyafanya sasa hivi ya kufanya neno lake ndio liwe katiba, Tafadhali Mwambieni.
Nimekasirika, kuona kwa sababu ya chuki zake binafsi na "Wawekezaji Wale" Watanzania wenzangu maelfu kwa maelfu wameachishwa kazi na kila kukicha makampuni yanaendelea kutangaaza kupunguza wafanyakazi na hata ambao bado wapo makazini hawajui kesho itakuwaje, Mwambieni sikumchagua kwa ajili ya kufanya hayo. Nilimpigia kura yangu ili aweke mazingira ya hao wenye nacho watengeneze ajira zaidi kwa watoto wetu, Nilimchagua atengeneze mazingira walau maisha yangu nami yainuke kidogo walau yawakaribie hao wenye nacho.
Nimekasirika, Binti yangu aliyesoma na kuhitimu chuo kikuu ualimu wa masomo ya arts na ambae nilimsomesha kwa mshahara wangu mdogo wa kazi yangu niliyoipoteza ya ulinzi kwenye kampuni la "Yule Mhindi" hajapata kazi tangu mwaka 2015. Wamerundikana mtaani na vyuoni bado wanaendelea kutengenezwa wengine, Nilimsomesha nikijua akimaliza ajira yake ni moja kwa moja serikalini na hivyo ndivyo ilivyokuwa, Si mngesema tangu awali kwamba ajira kwa hawa watu hazitakuwepo akasoma kitu kingine?
Mwambieni nimekasirika yeye kujifanya ndio Mungu, kuona kwamba yeye anajua kila kitu, Mwambieni kiongozi husikiliza, Nchi yetu hii ambayo watu wengi hawajui wanataka nini inahtaji kiongozi anayesikiliza maoni hata ya wachache wenye akili. Muulizeni kwanini anawachukia upinzani? Kama wanampa mawazo ya kujenga kwa nini anawachukia? Kwanini kuwakamata kamata kila siku kama vile wamekuwa maadui kisa tu wanaikosoa serikali? Nilitegemea angewasikiliza, na ambayo yanafaa angeyafanyia kazi kama hayafai angetoa majibu kwa hoja kwa nini hakubaliani na mawazo yao. Sio hivyo anavyofanya kuwachulia kama ni maadui wa serikali.
Mwambieni nimekasirika na mtaani kwetu watu wengi wana hasira. Mwambieni asipofanya jambo hawa watu anaofikiri hawana akili mwaka 2020 watamkataa, na akilazimisha ataelewa "Panya akikasirika anakuwaje". Mwambieni hajachelewa, akae ajitafakari upya, aanze upya.
Okay wataka tukutajie Ibara za kwenye Katiba yetu anazovunja Mkulu?Mnapoandika upuuzi wenu, mue pia mnataja na vifungu vya sheria anavyovunja, kwa maana ya ibara. Na sio mtindo wenu wa kipuuzi wa ku generalise habari
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaaa kasome sheria ya manunuzi ya serikali halafu uje utuambie umeona nini na yeye kafanya nini, kasome sheria na kanuni za utumish wa umma halafu uje utuambie umeona nini na yeye anafanya jini, kasome katiba katika kipengere cha haki za binadamu ukirudi pia utoe jibu yeye na wateule wake wanafanya nini, kasome sheria ya vyama vya siasa halafu urudo utoe jibu mjinga na mpumbavu wewe sheria zipo halafu hamsomi mnataka tuje tuwaletee sisi huku matokeo yake mmekuwa wasifiaji wa kila kitu kwa sababu hamna shule na sheria hamzijui, TULIPE DENI LA WATU.Mnapoandika upuuzi wenu, mue pia mnataja na vifungu vya sheria anavyovunja, kwa maana ya ibara. Na sio mtindo wenu wa kipuuzi wa ku generalise habari
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakuu wa wilaya - MaDC - wamekuwa kama wa enzi za ukoloni - wanatembea na fimbo za kuchapa watu na kuwasweka rumande kwa jinsi watakavyo.Viwanda imekuwa kukamata wananchi na upinzani kuwaweka ndani
Thumb downUnamsomesha binti mpaka Chuo kikuu bado unamtafutia kazi? Huyo binti mayai hawezi kufanya la maana kama utaendelea kumdekeza. Ni bure kabisa na wewe kama mzazi kichwa nazi. Chuo kikuu halafu unalia hapa jukwaani kuwa hana kazi?
Ni nani aliyepanda jukwaani akawaita wenzake WAPUMBAVU/MALOFA?Mikutano hamfanyi, Uhuru wa kutoa maoni, Kila siku mnaitisha media na kueleza hisia zenu, Kuna siku ambapo Mmekatazwa kuongea na vyombo vya habari.
Tatizo Uhuru huo mnautumia kifala, kutukana wenzenu, kuzua, kukashifu, haikubaliki popote pale duniani
Sent using Jamii Forums mobile app
Utaambiwa hata hayo maandishi yako sijayasoma nenda kayaandike kitandani kwako ulalie na mkeo.
In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
fanya kazi acha kulialia
fanya kazi acha kulialia