Mwambie dereva asimamishe kwanza!

Mwambie dereva asimamishe kwanza!

Magnificient

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,177
Reaction score
734
Mwanasaikolojia aliingia ndani ya chumba cha vichaa wenye afadhali kwa ajili ya kuwafanyia counselling ikiwezekana wapandishwe mabasi na warudishwe makwao. Wakati anaendelea akawataka kila mtu aigize kama yupo ndani ya basi; wengine wakaanza kulala, wengine kama wanasoma magazeti, wengine kama wanachati na wengine wanapiga story safarini. Muda kidogo mara kichaa mmoja akaanza kutapika, na kutapika na kutapika! Kuona vile mwanasaikolojia akaona akatishe igizo na kuwaambia vichaa wengine-
Mwanasaikolojia: Samahani, naomba mumsaidie kumpeleka mwenzenu nje.
Vichaa wakamjibu: Mwambie dereva asimamishe gari kwanza!
 
Back
Top Bottom