Mwalimu wa MATHS

Hapo Mapambano Study Camp ndo kwenyewe, Binafsi nimepitia hapo kama Mwanafunzi, na pia nilishafanya kazi hapo ya kuwapigia shule vijana Wa A-level somo la Maths (nathubutu kujisifu kwani mwanafunzi wangu aliongoza A-level Maths Mock exam kwa dsm,miaka kadhaa iliyopita, na Matokeo ya wanafunzi wangu kwenye Necta yalikuwa mazuri.)

Kusema kweli, ile sehemu kwa sasa ni kama Wadau muhimu sana wa Elimu, kwa Dar-es-salaam, pale kuna Mwalimu Mussa mtaalamu sana wa Chemistry na Biology, kuna Mwalimu Magnus naye mtaalamu sana wa Biology, Chemistry na Physics.

Pia kila mwaka huwa kuna form six leavers ambao ni vipanga huenda pale kuwapigia shule watoto wa vidato vya chini.
Kiufupi nakushauri umpeleke kijana wako pale. kila likizo inapofika, kwani wana program pana zaidi na si somo moja pekee.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom