Mwalimu wa Kike apigwa na Mwalimu Mkuu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
MWALIMU WA KIKE APIGWA NA MWALIMU MKUU NA KUVUNJWA JINO MOROGORO VIJIJINI. WENZAKE WAMUOMBA ASKOFU MWAMAKULA ASAIDIE KUPAZA SAUTI ILI MAWAZIRI WENYE DHAMANA WASIKIE NA KUINGILIA KATI

Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Tunapenda kukujulisha tukio la kusikitisha lililomkuta mwalimu mwenzetu aitwaye Witness Makoti wa Shule ya Msingi Mkuyuni iliyopo Tarafa ya Mkuyuni katika Wilaya ya Morogoro Vijijini Mkoani Morogoro.

Siku ya Ijumaa, tarehe 15 Oktoba 2021 muda wa Saa 6 mchana, Mwalimu Witness Makoti ambaye ni mwanamke alikuwa akiongea na wanafunzi watatu darasani. Wakati akiongea na watoto wake, ghafla alishambuliwa na kuanza kupigwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ambaye ni mwanaume aitwaye Mussa Hasira. Alipigwa sana lakini aliokolewa na mwalimu mmoja.

Baada ya kushambuliwa na kupigwa, Witness alikwenda kuripoti katika Kituo cha Polisi cha Mkuyuni na kupewa PF3 ya kwenda Zahanati ya Mkuyuni na kupata matibabu ya awali. Baada ya hali kuendelea kuwa mbaya, leo Jumapili alikwenda Hospitali ya Nunge kwa matibabu zaidi ambapo imegundulika kuwa Witness ana vidonda mdomoni na pia amevunjwa jino.

Hali yake ya kiafya mpaka sasa siyo nzuri sana na inazidi sana na ameleza pia kuwa pressure imempanda. Hadi muda huu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini na Mkuu wa Wilaya hawana taarifa.

Mwalimu Witness Makoti anahofia usalama wa maisha yake kwani ameelezwa kuwa Mwalimu Mkuu alimfuata mwalimu aliyemgombelezea Witness akaanza kumlaumu na kusema kuwa angelimuacha bila kumgombelezea ili amuue kabisa.

Mwalimu Witness Makoti ameomba asaidiwe katika kulipazia sauti jambo hili aweze kupata msaada kusudi haki iweze kutendeka lakini pia ili kuokoa maisha yake.

Tunaambatanisha picha ya Mwalimu Witness Makoti hapa chini.

Tunakushuru sana Baba Askofu Mwamakula kwa kutupokea na tunaamini kuwa kupitia sauti yako, Witness atapata msaada anaouhitaji.

8E4138A6-A3B0-4C32-9BDB-5FC73EBB8E2A.jpeg
 
Huyo Mussa Hasira ana ubini na jamaa mmoja huko Dar anayeitwa Hamisi Hasira ambaye naye ni mwenyeji wa Morogoro ambaye muda huu yupo mahabusu mwaka wa tatu kwa kosa la mauaji ya Bodaboda.

Isije ikawa ni ndugu maana hii hamu ya kuua seems ni insticts za kurithi
 
Hiyo taarifa haijaeleza kinaga ubaga nini hasa kisa na mkasa mpaka huyu mwalimu mkuu akaamua kumpika huyu mwalimu mwenzie mwalimu Witness?au huyu mwalimu mkuu amepandwa na kichaa cha ghafla?

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Kama ameshaenda polisi ilitakiwa polisi wafuatilie na wamkamate huyo mwl mkuu. Kwanini polisi hawajafanya kazi yao ,hiyo inaleta mashaka.
 
Kama ameshaenda polisi ilitakiwa polisi wafuatilie na wamkamate huyo mwl mkuu. Kwanini polisi hawajafanya kazi yao ,hiyo inaleta mashaka.
Hakuna taarifa kama hajakamatwa, pengine amekamatwa na kukamatwa siyo lazima awe ndani
 
Back
Top Bottom