Kutokana na walimu wengi wapya kuuliza mazingira na taarifa za msingi za mahali walipopangiwa kama kituo cha kazi, ningependa uzi huu utumike maalumu kwa ajili ya maswali na majibu yote yanayohusu taarifa vituo vipya.
Vile vile mnaweza kutumia ukumbi huu kukutana na walimu wenzako ambao mmepangiwa kituo kimoja, mkoa mmoja au maeneo ya jirani.
Kwa wale ambao wanataka ubadilishana vituo vya kazi, rejea maelezo ya msingi katika uzi HUU HAPA!
Karibuni na kila la heri walimu wapya!
waliopangiwa geita wilaya ya bukombe . au mtu yeyote yule anayeifahamu vizuri iyo wilaya aniisaidie
Tandahimba mkoa wa Gesi Zone(Mtwara/southern of Tanzania)
DC=District Counciljamani eti dc na tc tofauti nini?
DC=District Council
TC=Teaching College
Tandahimba ni wilaya inayopatikana Mkoa wa Mtwara, unapotaka kwenda waweza panda mabasi ya Dar-Tandahimba mfano wa basi ni TANDAHIMBA XPRESS (Bovubovu hivi) au upande basi linaloenda Masasi kutokea Dar then shuka Mtama (Kwa Bwana Mkubwa) hapo utapata mabasi ya huko, changamoto ya huko ni barabara mbovu tu ndo maana hata mabasi yanayokwenda huko ni yale ya tripu moja Dar Tripu gereji.
Tandahimba Express anaweza akalala njiani,sijui hilo lingine (TEMBO EXPRESS)Kuna mabasi yanaanzia pale Mbagara 3rangi yanaenda mpaka huko, mojawapo ni Tandaimba express na lingine ni Tembo express kama sikosei.
Halafu,changamoto kubwa ya Tandahimba ni Barabara tu,ni wilaya Kongwe ila duuuuuh...................anaweza akaenda hadi mtwara na akifika mtwara apande vicosta vya kwenda newala coz vinapita tandahimba nauli yake sidhani km itazidi elfu tano. Ila barabara ni ya vumbia kuanzia mtwara hadi unafika tandahimba. Wale jamaa ni wakorofi sn usipeleke dharau kule utaiona kazi chungu!