William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Wakuu ninaomba kutoa heshima kwa wananchi wote hapa forum, in the wake ya yanayotutokea sasa hivi kisiasa nchini, kwa unyeyekevu mkubwa ninaomba tumkumbuke Rais wetu wa kwanza Baba wa taifa Mwalimu Nyerere(RIP).
Ninaomba kuyafikisha kwenu matukio muhimu yaliyotokea katika kuelekea kwenye kututoka kwake, nilikuwa ninapitia maktaba yangu nikayakuta haya magazeti ya mwaka October, 1999, ya wiki ambazo zilielekeza mwisho wa Mwalimu, baba wa taifa, mwisho ambao wengi wetu tunaamini kuwa ndio uliokuwa mwanzo wa yanayotukuta sasa hivi katika taifa letu kisisasa.
Tumefikia mahali as taifa hatuelewani tena, kuna wanaonekana kuwa ni wamiliki wa nchi yetu, na sisi wananchi kuwa kama wageni, umoja wetu upo mashakani, mshikamano wetu upo njia panda, Mungu atunusuru na hili balaa tunalotaka kuletewa na wenzetu wachache wenye tamaa za utajiri wa haraka na madaraka yasiyokuwa na mipaka.
Reconciliation inaweza kuwa ni pamoja na kumkumbuka Mwalimu
Baba yetu alivyotutoka.
Ahsanteni Wakuu!