Kwani nchi inaongozwa na kabila au mtu?!Wakati Ule Nchi Maendeleo yalikuwa ya Upande Mmoja na Siasa zetu ziliashiria wananchi kuendelea kimpango MfanoWachagga na Wahaya sisi tulikuwe tumepata Elimu na wakati wa Mkoloni tulishika Madaraka sasa kama Nyerere asinge fuatilia hiyo nchi ingekuwa inatawaliwa na makabila makubwa au makabila yaliyokuwa na Elimu
Kwani nchi inaongozwa na kabila au mtu?!
Habari zenu jamani?!
Naomba nianze kwa kusema ukweli kwamba mimi sikuwepo kipindi cha utawala wa Mwl na hata alipofariki nilikua mdogo sana hivyo sikuwahi kujua kwanini watu wengi walikua wanampenda sana huku bado kukiwa na mambo mengi hasi yanayosemwa juu yake.Nafurahi kwamba mwaka huu nimeweza kutumia muda wangu kiasi nikasoma vitabu kadhaa kumhusu...makusanyo ya hotuba zake pamoja na vitabu alivyoandika mwenyewe.Kutokana na niliyoyasoma niliridhika kwamba sifa zote anastahili...pia kukosolewa maana yeye kama mtu mwingine yeyote yule makosa hatuwezi tuyakwepa.
Katika vitu ambavyo Mwl alivisimamia haswa ni usawa.Hakutaka kabila moja lijione/jisikie liko juu ya jingine na kutengeneza matabaka.Sasa swali langu nnaloomba mnisaidie ni hili....ule msemo au sijui niyaite madai ya kwamba Mwl aliwahi kusema makabila fulani hayafai kupewa uongozi wa juu wa nchi ni wa kweli au ni propaganda za waliomchukia?!Nauliza hivi kwasababu niliyoyasoma juu yake hayaendani kabisa na madai haya...na wala haileti maana kusikia kwamba aliyepigania usawa ndie aliyekua wa kwanza kutengeneza matabaka lilipokuja swala la uongozi!!!
Naomba majibu kama yapo yawe na vielelezo na yasiwe maneno ya kusikika na kufikirika tu ili tusiojua tujifunze kitu.
Asanteni!
Kwanza unakosea unaposema watu wengi walimpenda sana. Naomba kukufahamisha kuwa mimi nilikuwepo kabla, alipokuwepo, na baada yake. Nyerere hakupendwa na wengi kama unavyotakiwa kufikiria, Nyerere alilazimisha kupendwa, ukionesha kumpinga unapotezwa au unaswekwa ndani. Nyerere kisha koswa kupinduliwa mara nyingi tu kuliko Rais mwingine yoyote wa Tanzania.
Mengine hayo utajaza mwenyewe.
Hayo ni mawazo yakufikirika tu...hamna mwenye uhakika kwamba kama hilo lingetokea nchi ingeenda kombo(zaidi ya ilivyo) au pengine tungekua mbali sana kimaendeleo!Kama kweli alijitahidi kuzuia/kushawishi mkabila haya yasipate uongozi wa juu ina maana kwamba alikua mbinafsi sana kwa kuinyima Tanzania nafasi ambayo ingeweza kutufikisha mbali!Swala la kupeana madaraka hata kama sio ndani ya makabila hata sasa hivi lipo...kama hili hakuliona inawezekana hakuweza kuona faida ya kuifanya Tanzania nchi yenye demokrasia ya kweli na sio danganya toto!!Sio kuongozwa tu Madaraka Mbalimbali Nchini yangeegemea hayo Makabila na Usawa usingekuwepo Mfano Mzuri angalia Jirani zetu Kenya na Kabila la Kikikuyu wao walipendwa na wakoloni; wana Elimu zaidi ya wengine; Ardhi Zaidi ya Wengine; Mji bora zaidi ya wengine (NAIROBI) Wengi wana Madaraka na ni Mabwanyenye
Hakusema kabisa au hakusema kwa uwazi?!Nyerere hajawahi kusema makabila fulani Tanzania hayastahili uongozi wa aina fulani. Umeona vyema kwani angefanya hivyo ingekuwa ni kwenda kinyume kabisa na yote aliyoyasimamia na kuyaamini. Hii ni mojawapo ya myths ambazo zimetengenezwa.
Asante kwa kunirekebisha ila bado naamini waliompenda wanazidi walio/wanaomchukua...au labda tuseme hawakumtambua sawasawa kiasi cha kuamini aliwatakia mema hivyo hawana malalamiko juu yake. Binafsi naamini alikua dikteta wa kichinichini..wale waliokua karibu yake tu ndo wanaojua ni kwa jinsi gani hakupenda upinzani!!Kwanza unakosea unaposema watu wengi walimpenda sana. Naomba kukufahamisha kuwa mimi nilikuwepo kabla, alipokuwepo, na baada yake. Nyerere hakupendwa na wengi kama unavyotakiwa kufikiria, Nyerere alilazimisha kupendwa, ukionesha kumpinga unapotezwa au unaswekwa ndani. Nyerere kisha koswa kupinduliwa mara nyingi tu kuliko Rais mwingine yoyote wa Tanzania.Mengine hayo utajaza mwenyewe.
Asante kwa kunirekebisha ila bado naamini waliompenda wanazidi walio/wanaomchukua...au labda tuseme hawakumtambua sawasawa kiasi cha kuamini aliwatakia mema hivyo hawana malalamiko juu yake. Binafsi naamini alikua dikteta wa kichinichini..wale waliokua karibu yake tu ndo wanaojua ni kwa jinsi gani hakupenda upinzani!!
Well kwa hayo uliyoyasema hapo juu nadhani mwl alichangia sana kutusimamisha sehemu moja tu kwenye mstari wa maendeleo!Kama angetoa uhuru kwa wote wenye mawazo mazuri kusikika hata kama yalipingana na yake tungekua tumeendelea sana kisiasa!Kila aliempinga alionja joto yajiwewaulize kina bibi titi,kambona,edwin mtei na wengine weengi
Basi hakua mshindani hata kidogo....inawezekana alikua anaogopa sana upinzani!Ukweli ni kwamba Nyerere alikuwa dikteta kwa definition ya udikteta ya Ulaya Magharibi (by then). Ila kwa viwango vya Africa kwa wakati huo Nyerere alikuwa nafuu sana kulinganisha na viongozi wengine Madkiteta wa Africa ambao walikuwa wakiwaua wapinzani wao kwa maelfu. Nyerere alikuwa akiwanyima uhuru wapinzani wake kwa kuwapeleka huko vijijini na hawakutakiwa kufika mjini kujua nini kinaendelea. Mfano Kasanga Tumbo na Mzee Mapalala! Alikuwa Dikteta ila alikuwa si muuaji kama madikteta wengine wa Afrika wa enzi zake.
Well kwa hayo uliyoyasema hapo juu nadhani mwl alichangia sana kutusimamisha sehemu moja tu kwenye mstari wa maendeleo!Kama angetoa uhuru kwa wote wenye mawazo mazuri kusikika hata kama yalipingana na yake tungekua tumeendelea sana kisiasa!