Mwalimu Nyerere na siasa za Ujamaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu Nyerere na siasa za Ujamaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by daniel_mollel, Oct 14, 2011.

 1. d

  daniel_mollel Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huu ni wakati muafaka wa kuzungumza au kumkumbuka mwalimu J. K. Nyerere. Mwalimu ni mtu wa pekee sana kuwahi kutokea. Ninasema hivyo kwa sababu ukweli wa maisha yake unadhihirisha upekee alionao. Binadamu huumbwa na hulka moja ambayo mara nyingi sana huwa vigumu kuificha. Wazungu hukuza watoto wao kwa misingi ya kujaribu kuificha lakini kwenye baadhi ya mambo hudhihirika. Hulka hii siyo nyingine bali ni 'ubinafsi' umimi. Jambo hili ni gumu sana kulificha hata ukijaribu, kwa kiasi kikubwa sana wagunduzi wa mambo wakikufuatilia watalibaini. Mwalimu alifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kutawala jambo hilo katika maisha yake. Katika mazungumzo yake mara kwa mara aliepuka sana kutumia maneno 'mimi', 'nasema', 'nataka', n.k. Alitumia zaidi maneno ya majumuisho kwa mfano; watanzania wanataka, tungependa, n.k. Ni nadra sana kwa viongozi hasa wa Afrika kusahau kujineemesha wao na jamaa zao pindi wanapopata nafasi za kuongoza. Mwalimu aliongoza kwa kipindi kisichozidi miaka 25, ingemtosha sana yeye kujitengenezea maisha ya kifahari baada ya uongozi wake, lakini hakufanya hivyo. Hayo yote ni matunda ya jambo aliloliamini ambalo ndilo msingi wa siasa za ujamaa, 'usawa' hakuona haja ya kuwa kwenye daraja tofauti la maisha, badala yake alitaka kuwa kama mtanzania mwingine yeyote. Mwalimu Nyerere hakuwahi kuwa na nyumba aliyoijenga sina kumbukumbu ya gari alilolinunua, Mwalimu alipewa nyumba mbali mbali katika maeneo mbali mbali. Sasa baada yakusema hivyo nafikia uamuzi wa kukubali kwamba mwalimu alikuwa mjamaa, tena mzalendo. Mwalimu kwa bidii kabisa na moyo wakujitoa alisimamia jambo aliloliamini, bila woga wowote. Alifikia mahali pa kuridhia Waziri wake afungwe jela kwa makosa ya ufisadi, tena na viboko akachapwa kwa sababu mwalimu hakuwa mnafiki. Siasa za Ujamaa zilishindwa kwa sababu waliomzunguka Mwalimu kama wasaidizi wake hawakuwa wajamaa wa kweli. Nathubutu kusema waliokuwa wajamaa wa dhati ukimtoa Mwalimu ni watatu tu. Falsafa ya ujamaa ingefuatwa kwa uaminifu na wote kwa wakati huo, tungefika mbali sana.
   
Loading...