Mwalimu Nyerere My Role Model Daima Nitakukumbuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu Nyerere My Role Model Daima Nitakukumbuka

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by NdasheneMbandu, Oct 4, 2012.

 1. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Wakati tukijiandaa na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere tarehe 14 Oktoba 2012 nimewiwa kuanzisha uzi huu. Serikali yetu iliamua kwamba tarehe ya kuadhimisha kifo cha Baba wa Taifa iwe ndiyo tarehe ya kuzima Mwenge wa Uhuru na ndivyo ilivyo hivi sasa. Katika mwaka huu wa 2012 Mwenge wa Uhuru utazimwa Mjini Shinyanga kwenye sherehe zitakazohudhuriwa na Rais Jakaya M. Kikwete. Nimeambiwa na rafiki zangu waliopo Shinyanga kwamba maandalizi ya sherehe yamepamba moto.

  Wakati tukielekea kuifikia siku hiyo, siyo vibaya tukijikumbusha mambo kadhaa ambayo Mwl. Nyerere aliyapigania enzi za uhai wake akiwa kiongozi wa kitaifa na hata baada ya kung'atuka kabisa kwenye masuala ya uongozi iwe wa kisiasa au wa kiserikali na kubaki kuwa raia kama mimi NdasheneMbandu.

  Kwanza nianze kwa kutoa tahadhari mapema kwamba Mwl. Nyerere hakuwa malaika. Alikuwa binadamu kama mimi na wewe msomaji wa uzi huu. Hivyo, lazima yapo mapungufu na yanaweza kuwa mengi tu aliyofanya katika uhai wake na hasa alipokuwa kiongozi. Jambo hili naye aliwahi kukiri tena waziwazi; mbele ya waandishi wa habari kwamba yeye kama binadamu lazima alifanya makosa. Makosa hayo, yanaweza kuwa ni fundisho kubwa kwa viongozi wetu wa sasa kwani mengi ni ya kiutendaji kama alivyoeleza Mwl. Nyerere. Wenye kumbukumbu na makosa hayo, watayaweka kwenye uzi huu kama nami nitakavyochangia.

  Binafsi namchukulia Mwl. Nyerere kama ROLE MODEL yangu kiuongozi. Mpaka sasa, Mwalimu Nyerere anabaki kuwa ndiye kiongozi pekee machoni mwangu ambaye alikuwa ANATENDA ANACHOSEMA na siyo kinyume chake. Alikemea sana ulimbikizaji wa mali ya umma kwa manufaa binafsi na yeye aliishi kama mtu wa kawaida kabisa. Ni kiongozi pekee ambaye ilikuwa ni alama ya taifa popote aendapo ndani na nje ya nchi. Ni kiongozi pekee ambaye matumaini ya wananchi yalikuwa mabegani mwake iwe wakati wa shida au wa raha. Hata baada ya kuacha uongozi katika nyanja zote, wananchi waliendelea kumwamini na kumtumaini. Ni kiongozi ambaye alikemea hadharani maadui wakubwa wa utulivu na amani yaani UKABILA na UDINI na wananchi wakamwelewa na kumwamini hivyo tofauti na ilivyo sasa ambapo kiongozi anayekemea ndiye mkiukaji mkuu wa misingi hiyo.

  Kwa upande wa uchumi, Mwl. Nyerere ndiye kiongozi pekee aliyeimba wakati wote na kuhimiza wananchi kujiletea maendeleo yao wenyewe kwa kutegemea rasilimali zao badala ya kutegemea misaada kutoka nchi zingine. Alijua kuwa kujitawala maana yake ni kujitegemea na katika hili naweza hata kunukuu maneno yake mwenyewe aliposema "KAZI NDIYO MSINGI WA MAENDELEO. NCHI MASKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MSINGI WA FEDHA. NCHI MASKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MISAADA KUTOKA NCHI ZA NJE", mwisho wa kunukuu. Leo hii, tunalaumu viongozi wetu kwamba wanatekelza sera kandamizi zisizolenga kuwaletea wananchi maendeleo lakini yote hayo ni kwasababu moja tu nayo ni kuendekeza misaada kutoka nje inayotufunga midomo hata ya kuuliza practicability ya sera zinazoletwa nchini.

  Sera ya Mwl. Nyerere ya kujitegema ndiyo iliyozikomboa nchi za China na India na nchi zinazoitwa tigger nations za Malasia, Indonesia, Taiwan, Singapore. Nchi zote hizo zilikataa masharti ya WORLD BANK na IMF and yet zimeweza kujenga uchumi imara. Kagame wa Rwanda ndiyo mwelekeo aliochukua na hata Marehemu Zenawi wa Ethiopia ndiko alikokuwa akielekea. Lakini kiongozi wetu wa sasa, kama kawaida yake, yupo New york akifuatilia msaada wa USD 15.5 na nasikia akitoka hapo ataelekea Canada inawezekana kwa lengo hilohilo; la kuomba. Sijui kwa wenzetu waislam kitabu chao kitakatifu kinasemaje lakini kwa wakristo Biblia ipo wazi kwamba ANAYETOA SIKU ZOTE HUBARIKIWA na kwenye baadhi ya aya za Agano la Kale Mungu anapomtamkia laana mwanadamu ameonesha waziwazi kwamba ATAKUWA ANAKOPA TU NA KAMWE HATAKOPESHA. Kwa kupitia viongozi wetu, watanzania tumechagua laana.

  Daima Nitakukumbuka Mwl. Nyerere na Siku Zote Utaendelea kuwa Role Model Yangu.
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Bado naamini kwamba nchi hii itapata kiongozi atakayeturejesha katika misingi iliyopiganiwa na Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Huyu wa sasa, ameamua kujenga uchumi kwa KUTEMBEZA BAKULI UGHAIBUNI. Hivi sasa yupo New York na ataelekea Canada.
   
 3. Mango833

  Mango833 JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,560
  Likes Received: 17,796
  Trophy Points: 280
  hakuwa na mawazo constructive zaid ya destructive kuijenga nchi katika misingi ya kidini kwa lipi nitamuenzi zaid ya kukumbuka uovu wake
   
 4. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Okay...Wamaanisha JK siyo....sawa tumeelewa.
   
Loading...