Mwalimu Nyerere College Inahujumiwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu Nyerere College Inahujumiwa!

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Mizizi, Sep 9, 2011.

 1. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa taarifa nilizozipata leo hii kutoka kwa wadau wa Mwalimu nyerere Memorial Academy ni za kusikitisha sana. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba, mambo haya yanafanywa na vijana, ambao tulitegemea wangeleta mabadiliko na kusahau ile kasumba iliyokuwa ikishusha hadhi ya baadhi ya vyuo mbali mbali hapa nchini! Kinachotokea Mwalimu Nyerere ni kwamba kuna baadhi ya walimu wamesahau wajibu wao wa kuwasimamia wanafunzi wao ili kufikia malengo yao ya kitaaluma na badala yake wamejigeuza miungu watu.

  Haya yametokea hivi karibuni pale wanafunzi wa kada mbalimbali walipohitajika kuandika ripoti zao za tafiti mbalimbali kama utaratibu unavyoeleza. Kinyume na matarajio, baadhi ya wanafunzi hasa wa kike ambao wasimamizi wao ni wanaume vijana kukutana na vikwazo mbalimbali. Wengine walitakiwa kupeleka ripoti hizo nyumbani kwa walimu nyakati za usiku. Waliokataa kufanya hivyo wamefikia hatua mbaya, hata kukataliwa kupokelewa ripoti zao na hivyo kuwepo uwezekano wa kurudia mwaka! Cha kushangaza, ni kwamba, hawa wanaofanya haya wengine wamesoma ndani na nje ya nchi, na wameona ni jinsi gani huko walimu walivyo committed na helpful kwa wanafunzi wao kama wao walivyosaidiwa kwa hali ya juu. Cha ajabu ni kwanini wanaamua kuwafanyia ushenzi kama huu watanzania wenzao.

  Kuna mwalimu mmoja baada ya kufanya upumbavu kwa mwanafunzi mke wa mtu, mumewe akaamua kutia timu chuoni, mwalimu alipolazimishwa kuipokea ripoti ya mwanafunzi na mkuu wake akamwambia yule mwanafunzi amwite mumewe wasaishe wote,mwanafunzi alipoambiwa vile akaamua kufikisha malalamiko kwa mkuu wa yule mwalimu, ndipo akabadilishiwa msimamizi, ndipo yule mwalimu wa awali akamfuata huyu mwalimu na kumpa maelekezo kwamba, ahakikishe yule mwanafunzi anarudia mwaka ama yeye anaunja urafiki nae.
  Majina ya hawa walimu wote ninayo, na kuna mengi yaliyofanywa hapo chuoni, ikihitajika tutayaweka hapa.

  Sasa najiuliza, haya mambo mbona hayafanani na falsafa ya Mwalimu kama chuo kilivyobeba jina lake? Ama ndio hujuma za makusudi kukihujumu chuo hiki kwa malengo maalumu?
   
 2. fikirini

  fikirini Senior Member

  #2
  Sep 9, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hao walimu kweli au ndo waliobebwa wakati wa taaluma zao vyuoni? hao wana tabia za kinyama kabisa hawafai ktk maendeleo ya taifa letu, hebu ifikie kipindi vyuo viwe katka hali ya upekee kama ngazi ya juu ya elimu kwa kutoa elimu bora bila ya unyanyasaji wa wale wanaosoma sasa, kweli hao walimu ni educated au schooled people?
   
 3. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Cha kushangaza wanapoomba kazi, ukisoma barua zao na CV zao wanavyojieleza kwa ethics utapenda! Wanapopewa ofisi za umma wanafanya "uswahili" wao wa kijinga!
   
 4. Baba Erick

  Baba Erick JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hayo malalamiko mtumie rais kwenye account yake facebook watashughulikiwa haraka iwezekanavyo.
   
 5. S

  Sanga n. Member

  #5
  Sep 10, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli inashangaza sana. Halafu 2nasema 2nataka kuwafikia Westeners. Kwa mtindo huu wa kukabidhiana degree za kitandani tutafika?
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh kweli kazi ipo
   
 7. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapo sina neno, hao ndiyo watanzania
   
 8. s

  siwalaze Senior Member

  #8
  Sep 10, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Mie nadhani inahitajika!! hebu mwaga hapa hayo majina mkuu! u r a great thinker mkuu,ain't u?
   
 9. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  duh wataje hao wahujumu,hawana haya?
   
 10. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mtoa mada uliyosema ni kweli. Yupo mwalimu mmoja anapenda kuwakomalia sana wake za watu, haswa wanaotoka mikoani. Na yeyote hata kama hajaolewa. Anawabana sana ktk research work, jina limenitoka, nilikuonyeshwa akiwa ndani ya gari ya jamaa yake maeneo ya Posta.

  Wanatumia Mkendo Motel, halafu kuna mmoja anatajwa kuwapeleka kwenye Hotel moja ipo maeneo ya Kariakoo karibu na Mtaa wa Lumumba.
   
 11. Baba Erick

  Baba Erick JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni dhambi jamani matumizi ya kitu ya watu ni hatari sana ila mungu anaona hayo
   
 12. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Inabidi muweke majina yao hadharani ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao. Kwanini watanzania mnapenda kuficha ficha mambo? Hao wataendelea kudidimiza elimu pamoja na kuchafua sifa nzuri za chuo.
   
 13. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hili ni tatizo kubwa.Walimu wa vyuo hawana ethics za ualimu.Wanapata kazi kwa sababu wana GPA kubwa.Hakuna kozi wanazopelekwa kusomea ualimu pamoja na ethics zake ndiyo maana mambo kama haya yanajitokeza.
   
 14. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Hivi hapo Chuoni hakuna Serikali ya Wanafunzi? Kwa nini watu wawakubalie hao mafisadi badala ya kutumia vyombo vya kutafuta haki? Hakuna regulations dhidi ya sexual harassment? Kuwataja hapa JF yatakuwa kama majungu tu. Kama wahusika ni serious wafanye mipango ili hao watu wakamatwe ready-handed in action. Hili linawezekana. Lakini vile vile kuna wanawake wavivu au wasiojiweza (darasani) wakifeli wanasingizia eti walimu waliwataka kimapenzi wakawakatalia. Chunguzeni pande zote mbili.
   
 15. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  wataje kwa majina yao au ni umbeya wa kuwachafua tu?
   
 16. m

  maguu Member

  #16
  Sep 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kama ni kweli waachishwe kazi mar moja, si wazalendo hao, wana tamaa mbaya.
   
 17. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  orodhesha majina yao
   
 18. D

  Dotori JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mhusiika atoe data ambazo zitasaidia kulifanyia jambo hili. Kuongea kwa mafumbo hakusaidii
   
 19. Mashamba

  Mashamba JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ainisha majina yao jamvin humu, hawafai kwa lolote hata jina la kuwapa sina.Majina tu
   
 20. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu ingekuwa hivyo ulivyofikiria endapo matokeo yangekuwa yametoka na wahusika wamefeli mitihani yao!
  Nilichokielezea hapa, hata matokeo hayajatoka, kwa hiyo sidhani kama inaweza kuwa ni uvivu wa akina dada kutokamilisha repoti ndio wamesingizia hivyo kwa hili, japokuwa siwezi pingana moja kwa moja kwamba baadhi ya wanawake wanatumia njia za kujirahisisha kupata wepesi kwenye mambo ya elimu. Ila haimaanishi pia kwamba hakuna walimu wenye tabia chafu kama hizi
   
Loading...