Mwalimu Nyerere ametukanwaje hasa?

Tatizo ni lisu na sio matukano, kwani yapo matusi mengi sana yaliyotumiwa na wale wa mipasho/ccm na kwa nini lisu tu. mbona hamkusema kwa mtikila kipindi cha kifo cha nyerere 1999
 
Nitakujibu nikishakuwa na uhakika kuwa unajua maana ya "kutukana". Iwapo hujui maana ya matusi basi hakuna utakaloona tusi na itarudi tena kwenye "maneno na matumizi yake"'

Ulisikia aliyo sema Bi Asha? Mtoto wa marehemu Kawawa Bi Zainabu Kawawa?
 
I hate the unreasonable glorification of Nyerere.
 
Mkuu, nukuu hayo matusi aliyotukanwa Nyerere. weka bra bra pembeni.

Matusi ni maneno ya kawaida. Yanakuwa matusi tu pale yanapotumika kudhalilisha (discredit) watu wengine, vinginveyo siyo matusi. Nimeuliza iwapo muuliza swali ana threshold yoyote inayotofuatisha matusi na maneno mengine, hajanijibu ila wewe umeingia kumsaidia. Msioona matusi katika maneno ya Lissu ina maana kuwa hamuoni udhalilishaji katika maneno yake, na inakuwa ni vigumu kuwaridhisha. Nyie wanasheria nadhani mnajua sheria za Defamation of Character ambazo kwa lugha rahisi ni sheria dhidi ya kutukana. Ni mnajua ni mambo gani yanayotumika kutukana na ni yapi; na vile vile mnajua kuwa kuna hata sheria dhidi ya kutukana mtu aliyekiwsha fariki?
 
Tatizo ni lisu na sio matukano, kwani yapo matusi mengi sana yaliyotumiwa na wale wa mipasho/ccm na kwa nini lisu tu. mbona hamkusema kwa mtikila kipindi cha kifo cha nyerere 1999

Ndipo tunapokosa direction kama taifa iwapo sifa ya kisiasa ni kumwaga matusi tu.
 
........MANENO yote yaliyowahi kutoka mdomoni mwa Lissu yanatakiwa yaangaliwa kwa makini, mfano yakiwa yale maneno yake dhidi ya Zitto na Kitila.........

......Lissu aliwahi kuzungumzia issue za majaji walioteuliwa na JK......ukisoma kw amakini utaona uchambuzi wake ulikuwa una walakini fulani.......washabiki wa siasa wakabaki kushangilia!!........nakubaliana na wewe kuwa ni muhimu tuwe makini na maneno yatolewayo na watu mbali mbali..........

Moja ya jambo ambalo limeijengea Sifa sana JF ni kutokana na baadhi ya wanachama wake kuwa na uchambuzi mahiri........Umaarufu wa JF....Ni utamaduni wa kuchambua.......siku hizi kumetokea wanasiasa wengi wanataka kuivuruga JF yetu hapa....i.e. hapa pumba zinawekwa mchana kweupe na mchele vivyo hivyo.....
 
ukweli nyerere walikuwa muongo na mnafiki, amedhulumu sana, sasa mkiambiwa mnaona katukanwa, mbona wengine mnawatukana kwa kukashifu .....?
 
Swali langu unatakiwa ulijibu wewe uliyeshikwa na kisebusebu na n..ge cha kuwasilisha hayo ya MTEI kwani wewe siku hizi umekuwa msaidizi wa MTEI hadi uwasilishe hoja zake?

Edwin Mtei ni member humu. Isije ikawa haya maandishi yameghushiwa, kama ccm walivyozoea kughushi hasa hiyo ya kuteuliwa IMF 1972. Ajitokeze mwenyewe kueleza madhara aliyopata kwa matamshi ya Lissu.

Petro kwa nihakikishie kuwa huo ni uzi wa Mtei,ktk uzi huo hizi ni post za mwanzo zikionyesha Uvccm walitunga na kubandika jukwaani kwa id zao,tatizo baadae Mods wakaunganisha na id ya Mtei,haya sio maneno ya Mtei
 
hyo nyerere ni mungu mpaka wasimkosoe embu badilikeni....asiyekoselew ni moja tu allah.
 
Wanao mtukana nyerere ni ccm kupitia matamshi ya lissu ambayo hayana mantic hata moja ya matusi ni propaganda tu.naungana na lissu hatamtukana mwalimu nyerere ccm wazushi tu wanatafuta pa kupumulia hoja hawana wamebaki kuvizia vizia tu ili kuvuruga mchakato.
 

Nyerere alikua kiongozi mzuri, Lakini alikuwa na mapungufu jamani hakuwa Mungu alikuwa na mapungufu mengi tu ukiachana na huo uwongo,
 

kama kukosoa mawazo ya nyerere ni matusi basi walianza ccm kwa kulipuuza azimio la arusha,je si kweli kuwa wamelipuuza?.
 

Naona huna jibu ila kama kama ndiyo hivyo basis yamemtolea lissu tuhuma
 

ndugu mmeombwa mtaje hayo maneno aliyotumia lissu kumtusi mzee nyerere, wewe unatoa maelezo kumbuka si wote wasikiao habari hii walisikiza radio au kutazama runinga,nukuu hata maneno machache la sivyo tutaona ni propaganda za walioshindwa.
 
Sasa si uitafute ile link usikie mwenyewe na wewe na wenzako hamna ubavu wa kumuonya Lissu kama hata babu yako mtei kasikia unataka nini tena si ukamuulize mtei au Tundu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…