Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 745
- 1,504
Mwalimu aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi kuwa anataka kuwaonesha hatua tatu za hisia za binadamu..
Ya kwanza ikiwa ni sapraizi, ya pili kukereka na ya tatu kughadhibika..
Baada ya maelezo hayo akachukua simu yake na kuandika namba ya simu kwa kubahatisha tu kisha akaweka laudi spika na kuipiga. Ilivyo bahati iliita.
"Samahani. Naweza kuzungumza na Junia tafadhali," mwalimu alitamka punde tu baada ya simu kupokewa.
"Oh! Itakuwa umekosea namba. Simfahamu mtu anayeitwa Junia."
Mwalimu akakata simu na kuwaambia wanafunzi, "Hiyo ndiyo hatua ya kwanza. Sapraizi."
Kisha hapohapo akarejea tena kuipiga ileile namba.
"Hallo. Naomba uniitie Junia nahitaji kuzungumza naye." Mwalimu alizungumza punde tu baada ya simu kupokelewa.
"Hivi wewe si ndo umetoka kupiga nimekwambia umekosea namba. Jiheshimu basi."
Mwalimu akakata simu na kuwaambia wanafunzi, "Hiyo ndiyo hatua ya pili. Kukereka."

"Junia yuko hapo?" Mwalimu aliuliza punde tu baada ya simu kupokelewa.
"We mbwa kasoro mkia acha kujifanya hamnazo unasikia. Ukipiga tena nitakuja kuipasuapasua hiyo simu yako na kukuminya hizo kengele zako. Baradhuli wa kijivu wewe."
Mwalimu akakata simu na kuwaambia wanafunzi, "Hiyo ndiyo hatua ya tatu. Kughadhibika."
Hapohapo mwanafunzi mmoja akanyoosha mkono na kusema, "Mwalimu. Kuna hatua ya nne umeisahau."
"Ipi hiyo?" Mwalimu akauliza.
"Kuchanganyikiwa. Lete nikuoneshe." Mwanafunzi akachukua simu ya mwalimu na kuipiga namba ileile.
Ilipopokelewa akamwambia mpokeaji, "Hallo. Naitwa Junia. Kuna mtu alipiga kuniulizia hapo."
😁👨🦯
Jiunge na Chenrl yetu ya whatsApp