Mwalimu mkuu abaka mjukuu, baba abaka mtoto

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,902
2,000
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwaselela iliyopo katika Kata ya Iwindi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Alinani Mwakifuna (59) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 15.

Kamanda Ulrich Matei
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema mwalimu huyo alimbaka mjukuu wake ambaye jina limehifadhiwa Februari 16 mwaka huu akiwa naye shambani.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda Mtei amepinga kuhusisha tukio hilo na masuala ya kishirikina.

Katika tukio lingine Kamanda Matei amesema kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Samwel Msukila (22) mkazi wa Mbeya, anashikiliwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka tisa.

Kamanda Matei alisisitiza kuwa matukio yote mawili na mengine ambayo yamekuwa yakitokea mkoani humo hayahusiani na imani za kishirikina na badala yake ni tamaa za kimwili za wahusika.

Itv
 
NnyaMbwate

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,665
2,000
Katika tukio lingine Kamanda Matei amesema kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Samwel Msukila (22) mkazi wa Mbeya, anashikiliwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka tisa.

Itv
Hapa kuna tatizo la umri. Baba mzazi miaka 22, mtoto miaka 9. Kwa hiyo baba alipata mtoto akiwa na miaka 12 ama 13. Naona haijakaa sawa hii!
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300

Kwa umri wa huyo aliyembaka mwanawe uliwekwa hapo inaonesha kuwa hata yeye alimpata huyo mtoto akiwa bado ni mdogo sana (miaka 13). Huko inaonesha watu wanafyatuana wakiwa wadogo sana. Baridi.
 
BAFA

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
3,071
2,000
Mapedophile ni cult na michezo ya hatari sana na michezo imeenea kwa kasi wengi walijificha kwa kichaka cha ushirikina kumbe sio
 
clinical pharmacology2

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
1,128
2,000
inamaana huyu baba alipata mtoto wakati ana miaka 12 akiwa darasa la tano hii si rahisi kuamini.
Maana mvulana wa miaka 12 anakua hajafikia bado ile sexual maturity .
Hapa kuna tatizo la umri. Baba mzazi miaka 22, mtoto miaka 9. Kwa hiyo baba alipata mtoto akiwa na miaka 12 ama 13. Naona haijakaa sawa hii!
Sent using iPhone x
 
Mgugu

JF-Expert Member
Jul 1, 2015
2,154
2,000
Hapa mzee kabikisa mwaka mmoja apate mafao kala n'gombe mzima kasoro mkia hizi tamaa za mwili zinatupeleka pabaya
kastarehe ka dakika 3 na sekunde 47 kamemkosesha babu kikokotoo chake inawezekana pia na ka umri kake kaliko salia anakakamalizia kwa nguo za rangi ya machungwa.
Ila we miss zomboko kila siku habari unazotuletea humu ni za majanga tu, hivi kweli unakosa hata habari nzuri za wakulima wa korosho kuwanywisha soda mbuzi wao jamani?

Maendeleo hayana chama
 
son of a teacher

JF-Expert Member
Jul 30, 2017
401
1,000
labda mvulana wa mkoani huku dar wa miaka 12 wana pasuana balaa ..nenda shule za msingi uone madogo wana bf n gf
inamaana huyu baba alipata mtoto wakati ana miaka 12 akiwa darasa la tano hii si rahisi kuamini.
Maana mvulana wa miaka 12 anakua hajafikia bado ile sexual maturity .

Sent using iPhone x
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom