Mwalimu anyanyaswa Tanga

UMASIKINI BWANA

JF-Expert Member
Oct 17, 2013
942
567
Hbr wana jf kuna mwalimu huko mkoa wa Tanga kanilalamikia mpaka anasema anafikiria mengi huku akisema anaanza kuichukia kazi baada ya kutendewa manyanyaso na watu flani wenye nguvu ya madaraka.Anasema mkubwa flani anamnyima fursa kadhaa huku akiwapa watu wengine kiupendeleo hajawahi kwenda semina kubwa hata siku wanajirudia wale wale huku akiahidiwa kukiona na kutopata nafasi mpaka mwisho wa kazi yake au mkubwa huyo atakapo hama wilaya hiyo iliyopo karibu na mkoa wa manyara.Nashindwa nimsaidie nini mana kafanya kunililia na kupiga magoti mbele ya familia yangu hapa dodoma juzi jumamosi.Jamani tumsaidie kivipi anaonekana ku be frustrated kabisa anapata vitisho kadhaa ktk ajira yake fanyeni jambo kabla sijaenda mvaa huyo mnyanyasaji huyu ni mwanangu na ni yatima anaetegemewa nimemhoji vya kutosha yameniingia akilini.
 
Wambie atumie Fulsa zilizopo eneo husika kujiingezea kipato, hizi mambo ya semina, kusimamia mitihani Sijui kwenda kusahisha kuamini ni sehemu ya kuongeza kipato kwa mwalimu ilikuwa zamani,

Ni ujinga sana kukuta mwalimu wa leo anasema eti ananyanyasika kisa haendi semina haaa haaa, mwalimu funguka tafuta shughuli ya kufanya baada ya kazi uongeze kipato hayo masemina Sijui nini utaona yanakupotezea mda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom