Mwalimu amzalia mtoto mwanafunzi wake

Mwalimu amzalia mtoto mwanafunzi wake

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
Naona Dunia imegeuka sasa ni zamu ya waalimu kutembea na Wanafunzi na nadhani hata humu mmo



MWALIMU AMZALIA MTOTO MWANAFUNZI WAKE

Wakati ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kwa kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa kidato cha pili amemzalisha mwalimu wake.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 17 amemzalisha mwalimu wake mwenye umri wa miaka 25 katika shule ya sekondary ya umma ya Nkasi iliyopo katika mwambao wa ziwa Tanganyiaka.

Wanafunzi katika shule hiyo wamekuwa wakiendelea kumpongeza mwanafunzi mwenzao kwa kufanikiwakiwa kupata mtoto katika umri mdogo huku mzazi mwenzie akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa mwajiriwa wa serikali.

Imeeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado anaendelea na kazi shuleni hapo huku darasani kukiwa na mzazi mwenzie. Akizungumza na mwandishi wa haabari hizi mjini Namanyere hivi karibuni mkuu wa sekondary ya Nkasi ndugu Amiamie Nanga alisema, Mwalimu huyo aliyezalishwa na mwanafunzi ameanza kazi shuleni hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha tangu atoke chuoni.

"Yameshatokea lakini haileti picha nzuri sana, lakini mimi nina uzoefu mkubwa sana na wakazi wa ukanda wa pwani wa ziwa Tanganyika kwao sio ajabu kabisa kuwa na uhusiano na mtu aliye kuzidi umri, iwe kwa mtoto wa kike au wa kiume wote ni sawa tu..."

Chanzo: Habari Leo
 
HAPO CHILD Act HAIMUACHI HUYO MWALIMU
 
haiumizi sana hiyo angekuwa mtoto wa kike kweli...afu istoshe mwalimu basi hapo hakuna tatizo safi kabisa
 
Nae mwalimu awajibishwe kama wanavyo wajibishwa wanaume
 
Huyu mwalimu kifungo cha maisha au miaka 30 inamuhusu.
 
Kimaadili hili ni jambo la ajabu mno.. Ipa kwa kuwa maadili yameporomoka hamna jinsi... Yani hapo sifa ya ualimu haipo kabisaaa

ila utandawaz ndo umeharibu bhana ukizingatia mtoto wa kike katoka chuo tu.........
 
Mwalimu wa kiume akimzalisha mwanafunzi wa kike eti AMEBAKA,lakini mwalimu wa kike akizalishwa na mwanafunzi eti ni BAHATI!

Hizi sheria zetu tunaomba zifanye kazi sawa,kama tumependekeza 50/50 iwe ya kweli!Isiwe tu kutafutia kura za wanawake kwenye chaguzi zijazo!
 
Mwalimu apigwe 30 kwani simlisema ni haki sawa?
 
Back
Top Bottom