MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 850
huyu jamaa alikuwa kichwa sana, namheshimu.
Very true mkuu. Ninacho mpendea ni kwamba jamaa alikua na uwezo wa kuona mbali si hawa wa leo wanao ona urefu wa pua tu. Japo ali kuwa na mapungufu yake tunge chukua yale mazuri yake tunge kuwa mbali. He was a political genius and he is my political idol.
Mwanafalsafa1,
Kwa sababu leo ni Easter sitakuwa na muda mwingi wa kukaa kwenye mtandao. Lakini umeuliza tungechukua mazuri gani, hapa nitakupa mfano mmoja tu. Mwalimu alitaka Tanzania tuwe na viwanda vyetu, na alituwekea misingi ya viwanda hivyo. Licha ya kwamba viliendeshwa hohe-hahe (makosa) misingi ya kuwa na viwanda vyetu haikuwa kosa. Sasa wakaja wenye akili zaidi ( Mwinyi na Mkapa) na badala ya kuangalia ni wapi tulifanya makosa, tuyarekenishe, ili viwanda viendelee kuwa vyetu, wakaamua kubinafsisha, au kugeninasisha. Kuna wakati nilimwuuliza Mkapa kwa nini hawasaidii Watanzania wawekeze badala ya wageni, akanijibu kwa jeuri, "Watanzania ndio walioua viwanda. Afadhali tuwape Makaburu waviendeshe." Sasa tunavuna matunda ya mtazamo huo.
Ni hilo tu moja kwa leo. Happy Easter.
Huyu mzee mnamtukuza bure lakini ametawala nchi kibabe na kidikteta sana.
Baada ya kuona mambo yanamkalia vibaya na Watanzania wanaanza kuamka ndio akaanza kuzungumza lugha hizi za kujipendekeza kwa wananchi na kuwafanya waliokuja baada yake wabaya.
Chukua huo mfano wa Katiba unayosema Mkuu. Si Nyerere huyu huyu alieteua wajumbe wa CCM na Zanzibar kuandaa Katiba ya Chama chao na baadae akatumia Kamati hiio hio ya Chama chake kuunda Katiba ya Tanzania?
Si Nyerere huyu huyu aliekiuka Mkataba wa Muungano na kuligeuza Bunge letu la Kawaida na kulifanya kuwa Bunge la Katiba na kuipitisha?
Si Nyerere huyu huyu alievunja Mkataba wa Muungano na kiongezea madaraka SMT kwa kuifisidi Zanzibar?
Huyu Nyerere tutamkumbuka daima kwa chuki zake dhidi ya Zanzibar mpaka kwa kushindwa kujizuia akasema,
"If i could tow that island out into the middle of Indian Ocean, i could do it" - JK Nyerere
Huyu Nyerere ndio tutamkumbuka sana kwa mabaya yake na hakuna jema alotufanyia zaidi ya kutusaidia kumuondoa Mkoloni lakini kumbe kwa yeye kuifanya Zanzibar Koloni la Tanganyika.
Huyu ni mtu mbaya sana na hastahiki kusifiwa ila na wakoloni wenzake.
Hatutaki humu JF vijitu vyenye visa binafsi. Hata uwe so -ve, Nyerere will remain the Father of our Nation. Alikuwa na mapenzi ya dhati kwa nchi yake na alikuwa adui mkubwa kwa vijitu (nahisi na wewe ni miongoni mwao) vilivyotaka kutanguliza maslahi binafsi badala ya taifa. Misingi ya utaifa aliyoijenga ndiyo inayoifanya Tanzania angalau isurvive mpaka sasa katikati ya maadui wa ndani (kama wewe) na wa nje.
Taifa lipi are you reffering to Dume? Kijitu nadhani ni matusi au tuseme ni dharau na nikimuona mtu badala ya kujadili issue anajadili mtu, huanza kumdharau sana tu.
JF ni ukumbi huru wa mtu kutolea mawazo yake lakini wewe baada ya kujadili hoja, unanijadili mmi.
Wewe unamuona Nyerere hivyo, usinilazimishe na mimi kumuona hivyo.
Hapa si ubinafsi hata kidogo, ni hoja kwa hoja.
Hatutaki humu JF vijitu vyenye visa binafsi. Hata uwe so -ve, Nyerere will remain the Father of our Nation. Alikuwa na mapenzi ya dhati kwa nchi yake na alikuwa adui mkubwa kwa vijitu (nahisi na wewe ni miongoni mwao) vilivyotaka kutanguliza maslahi binafsi badala ya taifa. Misingi ya utaifa aliyoijenga ndiyo inayoifanya Tanzania angalau isurvive mpaka sasa katikati ya maadui wa ndani (kama wewe) na wa nje.
Kudadeki!brain washed...
Si hivyo tu bali pia hotuba zake zinavutia kusikiliza hata siku nzima kwani hazikuwa za kinafiki kama ilivyo kwa hawa wanaojichubua magamba kwa sasa.Kabisa Mkuu unaweza kusikiliza hotuba ya Mwalimu ya miaka 20 au 25 iliyopita lakini hotuba hiyo ingeweza kabisa kutolewa jana au juzi kutokana na mazingira tuliyonayo nchini mwetu kwa sasa