Mwaliko wa Kuhudhuria Kongamano kuhusu hali ya Elimu nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaliko wa Kuhudhuria Kongamano kuhusu hali ya Elimu nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by neemarug, Nov 21, 2011.

 1. n

  neemarug New Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Katika kuadhimisha miaka hamsini (50) ya Uhuru wa Tanzania Bara, Umoja wa Wanafunzi Walimu (UDSTA) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la HakiElimu wameandaa kongamano kuhusu hali ya elimu nchini. Kongamano hili litajadili maendeleo na changamoto katika Sekta ya Elimu tangu nchi yetu ilipopata uhuru. Kongamano hili litafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 26 Novemba 2011 kuanzia saa 4.00 asubuhi katika Ukumbi wa Yombo 4, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wazungumzaji wakuu katika Kongamano hili watakuwa Ndugu Jackson Makweta, Waziri wa zamani wa Elimu, na Profesa Justinian Galabawa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Ukiwa mdau muhimu wa maendeleo ya elimu na ya kijamii hapa nchini, unaombwa kuhudhuria kongamano hili wewe mwenyewe pamoja na viongozi wenzako. Aidha, unaombwa kwa nafasi yako uhamasishe wadau wengine katika taasisi yako, taasisi zingine, pamoja na wananchi kwa ujumla kuhudhuria kongamano hili muhimu.Tafadhali wasiliana nasi kwa ufafanuzi zaidi.
  Simu ya mezani; 255 22 2151892/3, simu za mkononi: +255 655/784 283 163 Barua pepe: media@hakielimu.org

  Tunatanguliza shukrani zetu kwa kukubali mwaliko huu.

  Wasalaam,


  Annastazia Rugaba
  Idara ya Habari
   
 2. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sawa ni muda mwingine watanzania kulalamika maana kila mtu ni kulalamika mpaka rais analalamika kila kukicha ni malalamiko,haya ndugu tutakuja tulalamike na tunashukuru kwa kuandaa jikwaa la kulalamika
   
 3. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kongamano muhimu ambalo limekuja ktk wakati muafaka kwa kuzingatia mabadiliko makubwa ya kieleimu tokea wakati wa tunaikomboa hadi leo.

  Muanzisha thread hakutaja agenda zitakazo jadiliwa ktk kongamano ispokua kwa kukumbushan tu ni vyema kama nguvu zitaelkezwa zaidi ktk uwezekano wa kubadilisha mitaala iliyopo ili kupambana na changamoto tulizonazo. Hili linaweza kwenda sambamba na kubadilisha mentality za waalimu wetu kua kila anapotunga mtihani mgumu ndio anaonekana mwalimu mzuri.

  Kwa ufupi inatakikana proposal ambayo italenga kufanya mabadiliko makubwa ktk secta ya elimu kuanzia vifaa, walimu, wanafunzi na pengine hata idara ya elimu na insi inavyofanya kazi zake.
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  sintoweza kufika.lakini nawasilisha maoni yangu hapa hapa."Teach the Farmer's son how to Farm"Kuanzia elimu ya msingi, watoto wanafundishwa mashuleni mamboambayo hawafundishwi nyumbani hivyo kuwaacha njia panda juu yamustakabali wa maisha yao ya baadae.Kwa mfano, angalia umasahini, watoto wakimasahi ufundishwa nawazazi wao practically namna ya kufanya ufugaji, lakini wakienda shuleni, wanafundishwa namna ya kulima pamba, korosho, karafuun.k then wanafundishwa juu ya ufugaji wa ng'ombe kidogo, thenufugaji wa kuku, kupiga pasi, kutengenesa Pizza, uvuvi, ushonaji,computer nk. mbaya zaidi yote haya yanafundishwa kinadharia.Hii haizisaidii jamii zetu kuendeleza na kuboresha shughuli za kiuchumikatika maeneo yao kiuendelevu. na ndio maana baada ya masomo hayahasa ya msingi ambako ndio kikomo cha masomo kwa watanzania wengi,tunakuwa na wasomi ambao sio expertise wa kitu chochote, ambao baada ya kugundua kwamba elimu waliyopata hawasaidii kuishi vizuri zaidikwenye jamii zao wanalazimika kukimbilia mijini.PendekezoWatoto wa wavuvi wafundidhwe uvuviwatoto wa wakulima wa pamba, wafundishwe kilimo cha pambawatoto wa wakulipa wa karafuu wafundishwe kilimo cha karafuuwatoto wa wakulima wa maharage, wafundishwe kilimo cha maharagewatoto wa wafugaji wafundishwe ufugaji.specialization hii itasaidia kuwafundisha kwa vitendo, sababu wanafundishwakitu ambacho wakiwa nyumbani wanakifanya kwa vitendo, kuanzia hapo evaluation inaweza kupatikana kutoka hata nyumbani, yes, wazazi wawezekutoa comment za ufanisi wa watoto wao katika shuguli za kiuchumi zakifamilia.Hapa ndio tutakuwa tunatengeneza an educated and responsible nation.Nwatakia kila la kheri.
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Nyie walimu mnaonekana ni VILAZA tu, miaka 50 ya Tanzania bara ipi? Miaka ya 50 iliyopita hakukuwa na nchi inaitwa Tanzania bara. Uhuru unaosherehewa ni wa nchi nzuri ya Tanganyika na sio hii Tanganyikazanzibaria. Acheni upotoshaji na dhuluma dhidi ya Tanganyika, hata kama CCM mmeamua kufukia historia, lakini acheni ukweli uwe ukweli. Profesa mzima anakubali kuhudhuria uhuru wa nchi ya bandia...
   
Loading...