Mwaliko kwa WanaJF

WaUru

New Member
Joined
Sep 3, 2011
Messages
4
Points
0

WaUru

New Member
Joined Sep 3, 2011
4 0
Heshima mbele wakubwa!

Mimi nimekuwa nikipita mara kwa mara na nimeguswa sana na moyo wa wengi hapa wa kufundishana na kusaidiana utaalamu wa biashara na ujasiriamali. Nimeona pia kuna ari ya kujiendeleza na kujikwamua kiuchumi na kimaisha. Nafikiri huu mwaliko hapa ndipo mahala pake.

Bila shaka wengi hapa mnaifahamu tovuti ya LinkedIn.com - basi kule kuna group moja linaitwa Tanzania Investors & Enterpreneurs ambayo kila mpitaji na mshiriki wa business & economic forum ya JF anaweza kuifurahia.

LinkedIn.com ni tovuti yenye kuunganisha watu (social networking) kama Facebook, lakini yenyewe ni ya "professionals" na mahusiano mengi huko ni ya kufahamiana aidha kibiashara na/au kikazi. Lengo la hilo kundi ni "... a networking platform for investors, entrepreneurs, explorers, friends and nationals with business interests in Tanzania." Ninachofurahia LinkedIn kwa maswala ya biashara ni uwazi wa wahusika... unabadilishana mawazo na watu ambao unaona walikosoma, kufanya kazi, wasifu wao kupitia picha na kadhalika. Sasa hivi hilo kundi lina wafanyabiashara wanaotaka kuzungumza na wajasiriamali wanohitaji msaada kuingiza bidhaa zao katika soko la Marekani, wajasiriamali wanaotafuta partner wa kufanya agribusiness Mwanza na wanaotafuta wawekezaji sekta ya safari za anga.

Ndugu, naamini wewe unastahili na mwaliko ndio huu! Tafadhali tuonane @ http://www.linkedin.com -> Groups -> Tanzania Investors & Enterpreneurs.

Shukurani kwa michango yenu hapa.

Mungu tubariki WaTanzania!
 

Remmy

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2009
Messages
4,712
Points
1,250

Remmy

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2009
4,712 1,250
Asante sana kwa taarifa, nafikiri nitajifunza mengi na nahisi sasa ni takuwa mfanyabishara mkubwa sana. Thanks to u pp.
 

WaUru

New Member
Joined
Sep 3, 2011
Messages
4
Points
0

WaUru

New Member
Joined Sep 3, 2011
4 0
Ni kweli... wengine wanapenda kulalamika na kusema hizo deal ni za mafisadi tu. Sio kweli... ulimwengu wa sasa unatupatia nafasi kukutana na watu wa mataifa mengine; tusilaze damu. Sio siri leo hii watu wa nje wana hamu ya kuingia katika soko la Tanzania kuliko nilivyowahi kuona maishani! Kama sio wewe, basi atapata mwingine . Haya ndio mambo ya siasa za kibepari. Sisemi uwe fisadi, lakini ni muhimu kutafuta masoko na miundo mbinu madhubuti kutoka katika nchi zilizoendelea.

Nafasi ndio hizi za kutupa ndoano kwa watu wa ndani na nje ya nchi. Kwani utapoteza nini? Ukiona unatangaza nafasi ya JV na hakuna anyejibu basi pengine hiyo biashara yako ina maswali zaidi ya majibu. Unajipanga na kuifanyia kazi tathmini yako halafu unaamua kifuatacho. Nawakilisha.

Mungu na atubariki WaTanzania.
 

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2009
Messages
2,479
Points
1,225

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2009
2,479 1,225
nimeiona... nadhani kuna kundi la watanzania wanaanza kuamka.. natamani kuona hata wale walioko vijijini wanafaidika na TEHAMA jamani...
 

Forum statistics

Threads 1,379,601
Members 525,469
Posts 33,750,267
Top