Mwakyembe: Ukikutwa na Shamba la Bangi jela miaka 30.

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Kuanzia sasa, kwa mtu yeyote atakayekutwa na shamba la dawa za kulevya aina ya banngi, anaweza kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha kuanzia miaka 30 gerezani

bangi%202.JPG

Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Sheria Mpya ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya, ambayo imeanza kutekelezwa hivi karibuni.

Mbali na adhabu hiyo, sheria hiyo pia imeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu atakayebainika kusafirisha aina yoyote ya dawa za kulevya, pamoja na wale wanaoingiza dawa kutoka nje ya nchi.

Pia sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya shilingi milioni 200 na kifungo cha maisha kwa watakaokutwa na malighafi au maabara za kutengezea dawa za kulevya huku ikiweka adhabu ya kifungo cha miaka mitano na/au faini ya kuanzia shilingi milioni moja kwa mtu atakayekutwa na kiasi kidogo cha dawa cha dawa za kulevya.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe, akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, kwa ajili ya uchambuzi wa sheria hiyo mpya, ambapo pia ameelezea utofauti wa sheria hiyo ya mwaka 2015 na ile iliyokuwepo ya mwaka 1995.

6_5.JPG

Dkt Harrison Mwakyembe

Amesema lazima kutakuwa na ukosoaji kwa kuwa sheria hiyo ni mpya hsa katika suala la mashahidi, lakini kuna sheria nyingine ya kulinda mashahidi (Whistle Blowers Act), ambayo itasaidia kuwalinda watu wanaotoa taarifa kuhusu wahusika wa dawa za kulevya

Amesema pia serikali iko tayari kupokea maoni kutoka kwa wadau, juu ya nini kifanyike ili kuwadhibiti wahusika wa dawa za kulevya ambao wamekuwa wakiifanyia wema jamii inayowazunguka kwa kiasi kikubwa.

Huyu hapa Dkt Mwakyembe akifafanua

Huyu naye ana madudu mengi
 
Ukiwa fisadi kama Lugumi, wale wa Escrow, Wabunge wapiga madili, mnunuzi wa mv ufisadi ya billioni 8 etc Serikali HAITAKUGUSA!
Mbowe amekupa nini ndugu mbona unajitoa ufahamu.
 
Mkuu hapo kwenye hicho kifaa achana nacho....
 
Kwa akili yako fupi kwa sababu wewe unapewa buku 7 basi unadhani kila anayeaandika hapa ananufaika.
Kwa akili yako fupi nilichoandika unaona ni kujitoa ufahamu lakini ukweli unaujua pamoja na kujaribu kuukimbia. Tia akili kichwani achana na ujuha.

Mbowe amekupa nini ndugu mbona unajitoa ufahamu.
 
Kama kweli Sheria inatekelezeka mateja wote wataishia segerea, Muda wote hicho kiasi kidogo wanacho
 
Nahitaji kufahamu wale maafisa wa serikali waliokuwa wanakula mishahara ya wafanyakazi hewa adhabu yao ni miaka mingapi jela na hadi hivi sasa ni wangapi washatiwa hatiani? Then ndio tuje kwenye dawa za kulevya
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bangi olkokola haipandwi ukiotesha mahindi au maharangwe unaikuta imeota yenywe,wakulima wengine tuna kaa mjini unapanda unaondoka unarudi kipindi cha palizi.
 
The research team predicted that cannabinoid-based medications "will be the new breakout medicine treatments of the near future.” kama watafiti wanakubali kazi ya mmea huu ambao unatibu magonjwa chungu mbovu! kwa nini serikali isije na njia mbadala kuhakikisha mmea huu unatunzwa kwa matumizi mengine pindi mambo yanapowia magumu? Siungi mkono mmea huu kuteketezwa kabisa in 'msukuma voice' message sent hah hah hah
 
Hawa Jamaa wa ccm sijui akili zao zina kaa wapi ni mafundi wakuanzisha mambo mapya kila Leo.
 
Kwa akili yako fupi kwa sababu wewe unapewa buku 7 basi unadhani kila anayeaandika hapa ananufaika.
Kwa akili yako fupi nilichoandika unaona ni kujitoa ufahamu lakini ukweli unaujua pamoja na kujaribu kuukimbia. Tia akili kichwani achana na ujuha.
Basi yatosha
 
Back
Top Bottom