Mwakyembe, Sitta waombe radhi watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe, Sitta waombe radhi watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwan mpambanaji, Feb 16, 2011.

 1. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanaJf
  nimetafakari hali ya giza na tanesco,na kutoka na uamuzi huu
  Sita na mwakyembe hawawezi kamwe kutoka kwenye hili zigo na daima watanzania na wapenda ukweli hatutawasamehe na histori itawahukumu,mtakumbuka kuwa mwakyembe kwa makusudi kabisa alificha ukweli kuhusu kampuni hewa ya richmond kwa kuhofia serikali kuanguka,alidiriki hata kutamka hadharani eti kama angesema yote serikali ingeanguka,ukweli hauwi nusu na kwa mwakyembe kuuficha ukweli amekosa uadilifu na hivyo kupelekea leo taifa kuingia gizani
  Sita akiwa spika hakuwatendea haki watanzania kwa kukubali ripoti nusu iliyoficha ukweli na kukubali kufunga mjadala wa richmond
  hawa wawili walikuwa na nafasi ya kutosha kuutetea ukweli na leo hii taifa tusingekuwa gizani na uzalishaji ungeendelea
  Hawa ni wanafiki,na wahujumu uchumi,na kwakuwa walishindwa kuutetea ukweli nao ni sehemu ya uovu,vinginevyo watuombe radhi
   
 2. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wewe ulitaka nini kingine kati ya mambo yaliyosemwa na hiyo kamati? kama mwakyembe angeyasema hayo unayofikiri hakuyasema je, ile mitambo na ile zabuni ingegeuka kuwa halali? Je, unakumbuka moja ya maazimio ya bunge ni kuitaifisha hiyo mitambo? Je, Unakumbuka kuwa sehemu ya tamko la kamati ya mwakyembe ni kwamba RICHMOND na DOWANS ni wahujumu uchumi?. Kama tamko lao ni uhujumu uchumi, Je ulitaka nini kingine kishauriwe au kizungumzwe na hawa jamaa? Je, kwa kutumia hoja ya uhujumu uchumi serikali isingeweza kumdhibiti huyo DOWANS kabla hata hajaenda huko ICC? Huoni kuwa mwenye makosa hapa ni Serikali na Si Bunge?
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa hilo nakubaliana na wewe mia kwa mia. Ni kinyume na maadili kutumia fedha za umma kwaajili ya uchunguzi wa jambo lenye maslahi makubwa kwa umma, halafu ukaficha baadhi ya mambo uliyoyagundua kwa kulinda maslahi ya baadhi ya watu au hata chama chako. Kitendo hicho ndicho hivi sasa kinatishia kupora watanzania 93 bilioni. Kama ukweli uliogunduliwa na tume ya Mwakyembe ungeliwekwa wote mezani sasa hivi pasingelikuwako Richmond au mtoto wake dowans.
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  jaribu kuwa na fikira pevu unapoongea juu ya Sitta na Mwakyembe unasahau kuwa walikuwa whistle blower na baada ya kupuliza kile kipenga serikali ilitakiwa ku-act kuanzisha mashitaka mahakamini! Lakini unajua kilichofuata? Mwakyembe alikoswakoswa na ajali ya truck akitokea Mbeya na Sitta naye kulikuwa na plot ya kuugonga msafara wake huku Rais akinyamaza kimya.....! na wewe muandikaji hata hukujitokeza kuandamana
   
 5. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Watanzania kuweni na shukrani japo kidogo,walichofanya mwakyembe na sitta nichakwanza kwa historia ya tanzania,watanzania tulitakiwa kutoichagua ccm basi
   
 6. n

  ngoko JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  We mtetezi wa RA?
   
 7. peck

  peck JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  nina wasiwasi na thread yako naamini umetumwa na MAFISADI wasiopenda mabadiliko ya tanzania safi, kwa yaliyobainishwa na mwakyembe kwenye kamati yake( kamati ilikuwa na wajumbe wengine na si yeye peke yake) yameweka bayana kuwa RICHMOND ni kampuni feki kwa hatua waliyofikia kamati ya Mwakyembe inatosha kuleta mafanikio ila Serikali MBOVU ya ccm na tabia ya kubebana ndo iliyotufikisha hapa tulipo. WALAANIWE WATU WOTE WANAOWALAUMU MWAKYEMBE na SITTA.
   
 8. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  giza tulilonalo ni planned in full stop. Mitambo ya dowani lazima ihalalishwe na kuanza kutumika.
   
 9. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Sitta ni mwanaume wa Shoka na anamsimamo sana sema tu kama binadamu alimheshimu mkwere akidhani mkwere ana heshima ni bora bunge lingemmwaga mkwere na sasa tungekua na mambo tofauti kabisa, kitendo chao cha kumhifadhi mkwere kimemugharimu mana amekuja kunyanganywa uspika na kupewa ka wizara kasiko na mashiko.

  Hata hivyo bado tunasonga naamini wengi tunamuunga mkono sitta na mwakyembe hawa ni mashujaa wetu
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi na uwezo wako..kama si ushabiki..hana lolote "opportunists" kwa kwenda mbele..tatizo vyeo mkuu
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MNYONGE ANAPOSHAMBULIWA MAMA MZAZI, HUGEUKA
  KUMPONGEZA MMBABE WAKE

  Kama kweli zile sauti za akina Mhe Sitta, Mwakyembe, Anna Kilango, Dr Slaa, Ole Sendeka na wengine wengi tu wa aina yao waliotutete kutokana na utapeli wa Richmond ambayo mpaka hivi leo yakaribia kubatizwa jina lingine baada ya kujiita Dowans juu ya ummeme nchini leo hii ni wa KUTAKIWA KUMUOMBA MTANZANIA YEYOTE RADHI, bali kwanza wanaoleta madai hayo wtangulie kwanza kutengeneza mabango makubwa sana ya kuwapongezea akina ROSTAM AZIZ, EDWARD LOWASSA wengine wengi wa aina yao ambao sharti wawataje waziwazi kama MASHUJAA wao wa kweli katika sakata zima na historia pia ikanakili hivyo kauli za hizo sauti za 'kimalaika' kama za huyu ndugu hapa juu!!

  Walevi wa aina hii ya Mwan Mpambanaji (kosa kujipa hilo jina) hata kijijini kwetu wapo. Tabia zao siku zote huwa ni hivi hivi; anatokea MMBABE mmoja kukanyaga na kuvunja kabisa kiko cha mama yake mzazi cha kuvutia ugoro (tumbaku) na kumrudi mzazi kwa masimango tele!!

  Mara utasiki lilevi lenyewe kwa uvivu wa kufikiri na udhaifu wa umbo likimgeuka mama yake kwa mashambulizi ya maneno kwa madai kwamba 'bore kiko chako kinge pasuliwa mara mia; kwa nini ukaiweke njiani wanakopita watu????'

  Kajana tulia kidogo kabla haujawalaumu akina Mhe Mwakyembe PhD na Mzee wa Viwango Samwel Sitta aka Standards & Speed katika hili usilolifahamu vema.

  Cha zaidi, jaribu kufikiria kidogo yule MMBABE WA KIKO CHA MZAZI wako jinsi atakavyokua anakuona, hata kama unacho kisomo kiasi fulani hivi, kuendelea kukucheka kwa mtindo wa 'jino pembe'!!
   
 12. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe na Sitta walitekeleza wajibu wao isipokuwa Mafisadi (JK, ED & Rostam Aziz- Muajemi) ndio wametufikisha hapa!!
   
 13. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Wewe wala si mpambanaj chochote wewe ni pambaf tu!

  Nyie ndo MAKUWADI WA Rostam Aziz na Edward Lowassa na Kiwete.
  You can not fool all the people all the time. Your days are numbered.

  Hii nchi inaonekana ni ya mazezeta wa kutupa. Haiwezekani Umeme wa DOWANS/RICHMOND ndiyo iwe SOLUTION PEKE YAKE KWA UMEME WA TANZANIA. Nasema Haiwesekani Asilan.

  1. Kwanini tunaendeleza kung'ang'ania KUWASHA MITAMBO YA DOWANS????This is NONSENSE.
  2. MITAMBO YA DOWANS/RICHMOND ILIZIMWA TANGU 2008,INA MAANA BAADA YA KUZIMA MITAMBO HIYO SERIKALI ILIKUWA IMEBWETEKA TU BADALA YA KUTAFUATA UFUMBUZI WA KUDUMU WA TATIZO LA UMEME?
  3. WALISAHAU KUWA MTERA ITAKAUKA TENA UKITOKEA UKAME KAMA MWAKA HUU?
  4. KWANINI SWALA LA UMEME NCHI HII LINAKUWA NI LA DHARURA KILA MWAKA,KUNATATIZO GANI??
  Nimeshangazwa sana na KAULI YA M/Kiti BOMU wa kamati ya Nishati na Madini Mhe. Januari Makamba pamoja na Waziri kivuli wa Nishati na Madini toka KUB Mhe.Mnyika. Kwamba mitambo ya DOWANS iwashwa kwa kuikodisha hata kama ni miezi MITATU. Hii ni kuwasaliti Watanzania kuendelea kung'ang'ania KUTUMIA MITAMBO YA KITAPELI YA DOWANS. Je, HAKUNA SOLUTION MBADALA YA TATIZO LA MGAWO WA UMEME TANZANIA?????????????

  Inasikitisha kuwa Tanzania HATUNA WAZIRI MAKINI WA NISHATI NA MADINI.Mhe.NGELEJA NI BOMU TENA LA KUTUPA NA MKONO. AMEBAKI KUPIGA DOMO TU BUNGENI HANA SOLUTION. TATIZO LA NCHI HII TUNAWAPA WANASIASA MADARAKA MAKUBWA KULIKO UWEZO WAO NA SIYO FANI(PROFESSION)ZAO. KILA SIKU ANASEMA KUNA MIPANGO YA MUDA MREFU/MFUPI NA RONGO RONGO KIBAO LAKINI HAKUNA OUTPUT YOYOTE. Uko wapi UMEME wa upepo tunaoambiwa upembuzi yakinifu ulishakamilika?NI SIASA TU.

  Naomba KIWETE AMWONDOE NGELEJA KWENYE NAFASI HIYO NA WIZARA HIYO APEWE MBUNGE AMBAYE KITAALUMA NI MTU WA UMEME PERCE YAANI AWE AN ELECTRICAL ENGINEER BY PROFESSION TENA KWA KIWANGO CHA DOCTORATE(PhD.)AU MASTERS.
   
 14. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwanza tuache ushabiki tujenge hoja,mtakumbuka na wote ni mashahidi wa jinsi sakata la richmond lilivyofungwa kwa ubabe na huyu Sita ambae kwenu mnamwona no shujaa,wote ni mashaidi kuwa maazimio 23 ya bunge hayakutekelezwa na sita akiwa spika akaufunga mjadala,kikanuni bunge lina wajibu wa kuilazimisha serikali kutekeleza maazimio yake,na linalindwa kikatiba,sita hakufanya hivyo akasema eti serikali itatekeleza
  Mwakyembe alipewa hadidu za rejea kuutafuta ukweli kuhusu richimond akaupata akauficha na yeye alikiri kuficha baadhi ya ukweli ili kuinusuru serikali,huu ni USALITI
  mimi sijatumwa na fisadi na wala hawawezi kunituma
  nitatetea ukweli daima
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wakiomba radhi itabdi ata EL arudishwe Upm?
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  Feb 16, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Nina wapongeza sana Sitta na Mwakyembe. Kupambana na kundi lenye nguuvu ndani ya chama na serikali haikuwa kazi rahisi.
  Sisi wananchi tukawaachia kazi kama ni yao tukibaki kushangilia.
  Waziri mkuu mwenye ulinzi wa juu nchini alitamka kuwa Mafisadi ni watu hatari sana. Huyu ni PM
  Rais wa nchi kaambiwa wezi ni hawa, lakini kakubali wastaafu kwa amani.
  Sitta akapangiwa ajali, mungu jalia haikutokea
  Ajali ya Mwakyembe ikaleta utata na kauli za kujichanganya, imebaki kitendawaili

  Hebu jiulize, Kama Waziri mkuu na Rais wanaogopa sembuse Sitta na Mwakyembe.
  Hata hivyo Sitta na Mwakyemebe wamebaki na misismamo yao ile ile licha ya kutishwa kwa kila aina ndani ya chama, mitaani na hata majimboni mwao. These are true heroes Tuwapongeze, japo kwa kile walichokifanya.
   
 17. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mwan mpambaf,

  Hiyo habari yote tunaifahamu unachoeleza ni historia mazee.

  Hivi wewe kwa akili yako UNAFIKIRI NI NANI ALIZIMA HOJA HIYO BUNGENI?
  Lowassa alimwaga manyanga,Karamagi na Bangusilo wakafuatia. Hili halikuwa jambo la ubabaishaji wala chuki za kisiasa kama alivyodai EL. Yale MAAZIMIO 23 ILIKUWA YATEKELZWE LAKINI MAFISADI WAKIONGOZWA NA RA PAMOJA NA KIWETE MWENYEWE WALIONA HALI YA UPEPO INAZIDI KUWA MBAYA WAKAAMUA KUIFUNIKA AU KUIPOTEZEA HIYO HOJA KIAINA.

  Hivi unafikiri kwa AKILI YAKO BARAZA LA MAWAZIRI LINGEVUNJWA KWA TUHUMA ZA JUU JUU TU? MBONA HATA RAIS WAKO KIWETE ALIKIRI KUWA KILICHOTOKEA KWA RAFIKI YAKE EL ILIKUWA NI AJALI YA KISIASA?

  Hivi unafikiri kwanini Mwakyembe alisema kuwa KUNA MAMBO/USHAHIDI mwingine hawakuutoa pale???Labda tu nikujuvye kidogo kuwa KULIKUWA NA VIMEMO VYA KUTOKA IKULU KWENDA KWA EL NA KWA KINA KARAMAGI NA BANGUSILO. Kama wangeweka mambo HADHARANI BASI IKULU INGEUMBUKA!

  Mimi naona kama Serikali kwa UNAFIKI inaanza kuwaona Mwakyembe na Sitta walidanganya Bunge eti WAOMBE RADHI NA KWA MAANA HIYO LOWASA,KARAMAGI NA BANGUSILO WARUDI KWENYE NYAZIFA ZAO,BASI NI WAKTI MWAFAKA KWA MWAKYEMBE NA SITTA KUWEKA MAMBO YOTE HADHARANI BILA KUTAFUNA MANENO. HAKUNA TENA KULINDANA KINAFIKI HAPA. KAMA MKWERE KIWETE ALISHIRIKI KWENYE KUIBEBA RICHMOND TUJUE MOJA ILI KAMA ANAJIUZULU SASA UCHAGUZI UITISHWE CHAPCHAP NA WANA-CHADEMA TUMWEKE RAIS WETU MTARAJIWA MHE. DK.WILBROAD PETER SLAA.

  Nini bwana tunakaa tunababaishana wakati mambo yako wazi!!
   
 18. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  kwa nchi ya siasa za funika kombe mwanaharamu apite walichofanya Mwakyembe na Sita ni kuweka rehani uhai wao..walithubutu kuonesha ukweli na kwa walioenda beyond pale walielewa lakini yote tisa...Rais Kikwete anajua kila kitu kuhusu hili dubwana DOWANS...km sivyo kwanini anafyata ilihali ni kiongozi mkuu wa nchi?
   
 19. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  add: ignore list
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [SIZE=+2]TO TYRANTS OF THE WORLD

  [/SIZE]By Tunisian Poet Abul Qasem El-Chebbi (1909 - 1934)

  Hey you, the ruthless tyrants...
  You lovers of darkness...
  You the enemies of life...
  You've made fun of innocent people's wounds; and your palm is covered with their blood
  You deforming the value of existence and sowed seeds of sadness in their land

  Wait, don't let the spring, the clearness of the sky and the shine of the morning light fool you...
  Because the darkness, the thunder rumble and the blowing of the wind are coming toward you from the horizon
  Beware because underneath the ash there is fire

  Who grows thorns will reap wounds
  The river of blood you shed will sweep you away and you will be burned by the fiery storm.

  (The Original Version)
  [​IMG]
  SOURCE: UNITED NATIONS. TO TYRANTS OF THE WORLD.

  UJUMBE HUMU:

  Ni ajabu na kweli kwamba kumbe yale yote yaliotokea Tunisia kupindua serikali dhalimu ya aliyekua Rais Ben Ali na kisha nguvu za virutubisho vya 'Matunda na Mboga Mboga' Shujaa Machinga Mohamed Bouazizi kuvuka mipaka yote YALISHATABIRIWA MNAMO MWAKA WA 1934 KUTOKEA.

  Mtunga mashairi mzaliwa wa nchini Tunisian, Ndg Abul Qasem El-Chebbi (1909 - 1934), aliyaona kwa macho yake udhalimu na ufisadi ukitendeka nchini mwake hata akaamua kuyaweka katika kumbukumbu za kimaandishi kama tulivyoyaona hapo juu.

  Baada ya takriban miaka 76 yale maoni yake yakaondoka kwenye karatasi; yakaenda mitaani na kugeuka moto mkubwa usiozimika uliotimulia mbali madikteta 2 hadi sasa na kuendelea kushika kasi!!! Mmachinga Mohamed Bouazizi ndiye silaha ya maangamizi iliokamilisha utabiri mzima!!!


  [​IMG]sidi‑bouzid‑12.jpg

  200 × 200 - Mohammed Bouazizi's (and Tunisia's) agony.


  [​IMG]

  6a00d8341c60bf53ef0133f5f3acc6970b‑500wi

  ... Tunisian Mohamed Bouazizi, whose immolation, December 17, launched the ...
  xomba.com

  Similar ‑ More sizes


  [​IMG]

  self‑immolation.jpg

  240 × 196 - In the case of Mohammed Bouazizi, the youth from Sidi Bouzid in Tunisia, ...
  jonathanfryer.wordpress.com  [​IMG]

  12626.jpg

  450 × 338 - Mohamed Bouazizi's fruit cart pushes over Ben Ali's throne
  israelagainstterror.blogspot.com


  [​IMG]

  b2f9473a7b98b167c7130b26111d028b.gif

  ... the Tunisian revolution began in with the suicide of Mohammed Bouazizi ...
  rozhlas.cz​
  Laiti watawa huwa huchukua japo dakika 30 tu kujisomea kila siku, badala ya kuendelea mfululizo kusikiliza maoni ya wanafiki, naamini wangeweza kuona shairi hili na kuzingatia zaidi onyo kali kwenye mistari ya 7 na ya 10 ili zahama yasiwakute kama ambavyo tunaendelea bado kushudia hivi leo.

  Enyi watawala: kuleni kidogo kwa afya njema na wala msizidishe kipimo chenu. Kila mmoja wetu katika jamii ANAYO UMUHIMU WAKE na wala asidharauliwe kitu.
   
Loading...