Nipashe
Member
- Nov 4, 2007
- 52
- 14
1. Kuna taarifa kwamba kuna marubani zaidi ya 60 ambao wapo nyumbani kwa miaka minne sasa na wanalipwa shillingi milioni sita kila mwezi. Hii ni sawa na zaidi ya milioni 400 kwa mwezi, zaidi ya bilioni nne kwa mwaka, karibia bilioni 20 katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Hizi ni fedha ambazo zinapotea bila wahusika kuwa na mchango wowote kwa shirika hili la umma.
2. Kuna watumishi ambao Mkurugenzi Mkuu wa zamani aliwaajiri kwa wingi sana kwa misingi ya urafiki wa kijinsia na undugu, na wengi ya hawa hawana sifa za nafasi zao, na kwa sasa hawana lolote la maana wanalofanya kwani hakuna kazi za kufanya katika shirika linalokufa, sana sana wanapoteza fedha za walipa kodi.
3. Kuna ushahidi tosha kwamba kuna mkono wa vigogo kuhakikisha shirika hili halifanikiwi, kama ilivyotokea kwenye sekta ya reli, ili kunufaisha biashara binafsi za vigogo katika sekta ya usafiri.
Dr. Mwakyembe, unasubiri nini kusafisha madudu haya badala ya kuokoa fedha za walipa kodi zinazo zidi kupotea kwa wingi?