ipinho
Member
- Sep 9, 2013
- 81
- 62
Niliwahi sema Mwakyembee ni msomi wa sheria kiwango cha PHD, lakini hana hekima. Ana elimu kubwa lakini hajamsaidia wala kumjengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kama kiongozi.
Hana msimamo wala anachokiamini. Kama kipo anachokiamini, basi ni Madaraka.
Wanaofuatilia na kutafakari juu ya mwenendo wa mwanasiasa huyo, wanadai tatizo lake ni hamu ya madaraka.
Yuko tayari kuitikia hata asiyoyapenda au kusaliti Mtazamo wake ili kulinda au kupata Madaraka.
Madaraka ni kilevi chake. Kila penye harufu ya Madaraka ni tatizo kwa Mwakyembe.
NINA MIFANO MICHACHE.
1.JK akiwa rais alimwona Mwakyembee anavyopambana bungeni. Haikuchukua muda kumsoma anachotaka. Ndipo JK akampa unaibu waziri na baadaye uwaziri kamili. Akatulia.
Baada ya kupata alichokuwa anakitafuta, ukawa ni mwendo mdundo kufanya lolote ili kushikilia alichonacho.
2.Aliandika andiko la PHD yake ya sheria. Huko alijadili akidai Muungano wa serikali tatu unafaa. Kwa ubora wa andiko hilo akapewa PHD.
Wakati kuandika katiba mpya ndani ya BMK alibadilika kuunga mkono serikali mbili. Alisaliti hata andiko lililompa heshima ya udaktari.
3.Alipokuwa waziri wa katiba na sheria, alifikiria na alisema atakifuta chama cha wana sheria Tanganyika(TLS) kwa sababu aliyegombea na kushinda urais wa chama hicho hapendwi na serikali, hata boss wake. TLS aliyotaka ifutwe ndio iliyompa heshima ya kuwa wakili.
4.Amepewa cheo cha uwaziri wa habari na michezo. Ameanza kazi kwa kuonesha umma kuwa mtangulizi wake alikuwa anakosea. Yote haya ni katika kuhalalisha makosa ya boss wake ya kumfukuza kazi waziri aliyetaka kumwajibisha mpendwa wake RC wa DSM.
5.Mwakyembee anazungumzia natural justice. Anasema kamati ya Nape haikumhoji RC wa mkoa wa DSM, wakati anajua RC huyo, alitoroka asihojiwe.
6.Lakini, Mwakyembe huyu huyu mwaka 2008 alikwenda kinyume na principle ya Natural justice. Aliwahi kuwa mwalimu wa sheria chuo kikuu cha DSM.
Alikuwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge 2007 iliyochunguza sakata LA Richmond.Alitoa Ripoti februari 2008 iliyomhusisha aliyekuwa waziri mkuu(Lowassa) akijua kuwa kamati yake hakumhoji au kumpa nafasi Lowassa kujitetea.
8.Baadaye mwakyembee alisimama bungeni na kudai kuna mambo aliyaficha ili kulinda heshima ya serikali.Mpaka Leo haweka hadharani mambo aliyoyaficha.
9.Huyu ndiye mwanasheria anayesifiwa na JPM kuwa ni mzuri na akaridhika na kuchekelea. Lakini,anayemsifia ndiye aliyemwondoa kwenye wizara ya katiba na sheria, inayoendana na taaluma yake ya sheria. Ina maana haridhiki naye. Hajui hilo.
Watu wa aina hii ya Mwakyembe mwisho wao huwa ni fedheha.
kibonadickson@gmail.com.