Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
Kambi ya upinzani walisema hivi juu ya jambo hili na chini attached nyaraka
5.1 Shirika la ndege ATCL .
Mheshimiwa Spika, Shirika la Ndege Tanzania ( ATCL) walikodishajiNdege aina ya Air Bus 420-214 mwaka 2007 kutoka kwa Kampuni ya Wallis Trading ya Lebanon kwa muda wa miaka sitana serikali iliweka dhamana ya mkopo huo kupitia kwa msajili wa hazina , mkopo uliokuwa na thamani ya kiasi cha dola za Marekani 60,000,000 na hadi kufikia30Juni 2011 dhamana hiyo pamoja na riba ni shilingi za kitanzania bilioni 108.
Mheshimiwa Spika, Mwezi Julai 2009 Ndege hiyo ilipelekwa Ufaransa kwa ajili yakufanyiwa matengenezo makubwa yanayojulikana kama 12 years check na kukamilikamatengenezo lakini haikurudishwa kwa sababu ATCL walikosa fedha za kulipia matengenezoUSD 3,009,495.
Mheshimiwa Spika, serikali mpaka leo inadaiwa jumla ya dola za kimarekani39,000,000 na kampuni ya Wallis Trading ya Lebanoni ambako ndiko ndege hiyoilikodishwa japo haijaweza kufanya kazi lakini serikali inalazimika kulipakutokana na thamana ambayo iliwekwa na Serikali.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo ni kuwa mnamo tarehe 27 March2012 wawakilishi wa kampuni hii wakiongozwa na Mr.Diab wakiambatana na mawakili wao ambao ni Mr. Mkono na Dr. Kapinga walikuwa na kikao na wizara ya fedha ambapokwa upande wa Serikali iliwakilishwa na Mr. Latson Msongole ambaye alikuwa kaimukatibu mkuu wa wizara ya fedha na Mrs. Mlakiambaye ni msajili wa Hazina.
Mheshimiwa Spika , katika kikao hicho muhutasari unaonyesha kuwaMr Mkono alipendekeza kuwa kutokana na serikali kuwa mstari wa mbele katikakuvutia wawekezaji alitaka kampuni ya Wallis ipewe fursa ya kuwekeza kwenyesekta ya madini au Real Estate na hivyo uwekezaji huo utakuwa mbadala wa deniambalo wanaidai serikali , ila Mwakilishi wa Wallis alitaka ama wapewe majengo na ardhi inayomilikiwa na ATCL vilivyopo Dar Es Salaam ila walijulishwa kuwa majengo na Ardhi ya ATCL vimeshachukuliwa na serikali.
Mheshimiwa Spika, katika kikao hicho wawakilishi hao wa Walliswalitaka wapatiwe bandari ya Mtwara ili waweze kuiendesha mpaka deni laolitakapokuwa limeisha , na makubaliano kwenye kikao hicho yalikuwa kuwa Wallis wafanye utafiti kwa kushirikiana na Mrs. Mlaki na TIC ili waweze kujua kati ya mapendekezowaliyotoa ni wapi wataona fursa ya kufaa na hivyo wataweza kupatiwa eneo hilo.
Mheshimiwa Spika, taarifa hizi ni kwa mujibu wa barua ya tarehe 3 April 2012iliyoandikwa na A H Wettern kwaniaba ya Wallis kwenda Wizara ya fedha na uchumi na nakala ya barua husika ikapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16 May 2012 kampuni ya Wallis waliandika barua kwakatibu Mkuu wa hazina na nakala kutolewa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kukumbushia maazimio na makubaliano ambayo waliyafikia pamoja na utekelezwajiwa kulipa madeni.
Kambi yaupinzani, tunataka kupama majibu kuhusiana na mambo yafuatayo;
i. Je? Wallis walishafanya utafiti na matokeo yake ni kuwekeza kwenye sekta gani?
ii. Bandari ya Mtwara ipo salama? Serikali inatoatamko gani kuhusiana na wale wote ambao wameshiriki kwenye vikao vyamakubaliano haswa katika kutwaa rasilimali za nchi ili kulipia madeniyaliyosababishwa kwa uzembe wa baadhi ya watumishi?
iii. Ni lini madeni haya yatalipwa ili taifa liondokane na aibu hii na pia waliohusika kuingia mikataba hii watachukuliwa hatua gani?