Mwakyembe iombe radhi JF; Mazungumzo ya Kutoa bandari ya Mtwara haya hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe iombe radhi JF; Mazungumzo ya Kutoa bandari ya Mtwara haya hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Aug 2, 2012.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kambi ya upinzani walisema hivi juu ya jambo hili na chini attached nyaraka


  5.1 Shirika la ndege ATCL .
  Mheshimiwa Spika, Shirika la Ndege Tanzania ( ATCL) walikodishajiNdege aina ya Air Bus 420-214 mwaka 2007 kutoka kwa Kampuni ya Wallis Trading ya Lebanon kwa muda wa miaka sitana serikali iliweka dhamana ya mkopo huo kupitia kwa msajili wa hazina , mkopo uliokuwa na thamani ya kiasi cha dola za Marekani 60,000,000 na hadi kufikia30Juni 2011 dhamana hiyo pamoja na riba ni shilingi za kitanzania bilioni 108.

  Mheshimiwa Spika, Mwezi Julai 2009 Ndege hiyo ilipelekwa Ufaransa kwa ajili yakufanyiwa matengenezo makubwa yanayojulikana kama 12 years check na kukamilikamatengenezo lakini haikurudishwa kwa sababu ATCL walikosa fedha za kulipia matengenezoUSD 3,009,495.

  Mheshimiwa Spika, serikali mpaka leo inadaiwa jumla ya dola za kimarekani39,000,000 na kampuni ya Wallis Trading ya Lebanoni ambako ndiko ndege hiyoilikodishwa japo haijaweza kufanya kazi lakini serikali inalazimika kulipakutokana na thamana ambayo iliwekwa na Serikali.

  Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo ni kuwa mnamo tarehe 27 March2012 wawakilishi wa kampuni hii wakiongozwa na Mr.Diab wakiambatana na mawakili wao ambao ni Mr. Mkono na Dr. Kapinga walikuwa na kikao na wizara ya fedha ambapokwa upande wa Serikali iliwakilishwa na Mr. Latson Msongole ambaye alikuwa kaimukatibu mkuu wa wizara ya fedha na Mrs. Mlakiambaye ni msajili wa Hazina.

  Mheshimiwa Spika , katika kikao hicho muhutasari unaonyesha kuwaMr Mkono alipendekeza kuwa kutokana na serikali kuwa mstari wa mbele katikakuvutia wawekezaji alitaka kampuni ya Wallis ipewe fursa ya kuwekeza kwenyesekta ya madini au Real Estate na hivyo uwekezaji huo utakuwa mbadala wa deniambalo wanaidai serikali , ila Mwakilishi wa Wallis alitaka ama wapewe majengo na ardhi inayomilikiwa na ATCL vilivyopo Dar Es Salaam ila walijulishwa kuwa majengo na Ardhi ya ATCL vimeshachukuliwa na serikali.

  Mheshimiwa Spika, katika kikao hicho wawakilishi hao wa Walliswalitaka wapatiwe bandari ya Mtwara ili waweze kuiendesha mpaka deni laolitakapokuwa limeisha , na makubaliano kwenye kikao hicho yalikuwa kuwa Wallis wafanye utafiti kwa kushirikiana na Mrs. Mlaki na TIC ili waweze kujua kati ya mapendekezowaliyotoa ni wapi wataona fursa ya kufaa na hivyo wataweza kupatiwa eneo hilo.

  Mheshimiwa Spika, taarifa hizi ni kwa mujibu wa barua ya tarehe 3 April 2012iliyoandikwa na A H Wettern kwaniaba ya Wallis kwenda Wizara ya fedha na uchumi na nakala ya barua husika ikapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16 May 2012 kampuni ya Wallis waliandika barua kwakatibu Mkuu wa hazina na nakala kutolewa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kukumbushia maazimio na makubaliano ambayo waliyafikia pamoja na utekelezwajiwa kulipa madeni.

  Kambi yaupinzani, tunataka kupama majibu kuhusiana na mambo yafuatayo;
  i. Je? Wallis walishafanya utafiti na matokeo yake ni kuwekeza kwenye sekta gani?
  ii. Bandari ya Mtwara ipo salama? Serikali inatoatamko gani kuhusiana na wale wote ambao wameshiriki kwenye vikao vyamakubaliano haswa katika kutwaa rasilimali za nchi ili kulipia madeniyaliyosababishwa kwa uzembe wa baadhi ya watumishi?
  iii. Ni lini madeni haya yatalipwa ili taifa liondokane na aibu hii na pia waliohusika kuingia mikataba hii watachukuliwa hatua gani?
   

  Attached Files:

 2. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hii ni Serikali ya Aibu kuwahi kutokea duniani. Imeshanichosha. 2015 ni mbali mno kuiondoa madarakani.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu Mwake apo kwenye JF itabidi ufute kauli yako maana watu wana nondo umu
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hahaah! ndo raha ya kushindana na JF, watu wanatembea na nondo wanasubiri muda muafaka kuzitumia!! Sasa Mwakyembe inabidi afute kauli yake.
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  Msimsumbue bado hile sumu anayo! Msameheni.
   
 6. Q

  Qixima mQiqa Senior Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  natumai leo haitaisha bila mwakyembe kuingia Jf
   
 7. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  Walishasahau kuhusu mkutano huo,pollonium mchezo?
   
 8. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Nilijua tu watu watamwaga mambo hadharani.

  Tatizo kubwa la Mwakyembe na mwenzake Sitta ni u 'much know' na kuona wengine hawana maana. Kutoka Richmond move kukosa uspika kupewa uwaziri, tuhuma za kulishwa sumu then promotion coz ukiacha uwaziri Sita anakaimu bungeni Pinda asipokuwepo na Mwaki nae kawa full minister. Anachokifanya ni kuprove yeye ni jembe. Ukiacha too much sifa za usomi wakati kuna ma-proffesor kama mzee wangu Mwandosya ambae ni mtulivu katika kila kitu, na dharau angeweza kumove. Lkn kuona yeye ndo encyclopedia naamini atasusiwa na mambo hayataenda.

  Waziri ni sera tu utekelezaji unabaki kwa watendaji, ukijifanya mjuaji jamaa wanakususia then kunakuwa hakuna kitu. Tusubiri majibu tutayapata very soon.
   
 9. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hata Werema mwanasheria mkuu wa serikali nafikiri alimshangaa kwani anajua dili lote hilo sasa Mwakyembe anaizushia JF leo ndio zimeingia aache kuchezea hii kitu iko kila mahali na tutaanza kuimulika wizara yake na ujenzi wa gati 13&14 pale bandarini ili ajue kuwa kila kikao kinawekwa humu JF mpaka ajitokeze.
   
 10. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  haya ndio madudu yao "Mr Mkono, suggested that the Government being keen to attract foreign investors asked if Wallis might consider to inves in Tanzania in which part of the Ministry debt to Wallis would be swapped – e.g. in the mining or real estate, so that the investment cost for Wallis would be set-off against part of the Ministry debt to Wallis".

  "Wallis asked if ATCL (land and buildings in Dar) can be considered, but was surprised to hear that the property has been taken by the Government.
  Wallis asked if Mtwara Port for example could be acquired on BOT basis" –


  The Acting Permanent Secretary suggested that Wallis should start investigating with Mrs Mlaki, being in charge of State Assets, and with TIC.

  Mwakyembe .........

   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nadhani tumsamehe Mwakyembe, inaonekana bado ajakaa vyema sana.
   
 12. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  nini kimotokea wakuu! jamaa karopoka nini? nilikuwa pori ...nijuzeni
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  yule mzee ana matatizo
   
 14. r

  raymg JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Napita tu nikirudi nitawambia cha kufanya nawaomba mjipange kwa lolote wanajukwaa
   
 15. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Thanks to JF we have this in day light!!!

  Kidumu chama cha map...... Oooops, idumu JF.......?
   
 16. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kama kambi ya upinzani ilisema ndo tuamini?
   
 17. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Akiri kua anaumwa atasamehewa lakini sio kuisema JF kwa uzushi ili kuivunjia heshima yake
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  mzee kaumubuka ...aibuuuuuuuuuuuu.....
   
 19. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Fungua hizo PDF ujue kilichomo kuhusu hilo
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280

  utakuwa hujui kusoma kingereza au kwa makusudi hutaki kusoma hizo attachment
   
Loading...