Mwakyembe amtaka Makonda ajibu maswali 9

Mwakyembe amtaka Makonda ajibu maswali 9

Labda swali namba 4 litakua kwa uthibitisho wa vyeti tueleze historia ya elimu yako
 
Alipewa nafasi ya kujieleza akakataa. Kwa hiyo hukumu itolewe kwa kukataa kujibu maswali, yaani iwe based upande wa Clouds na sharia.
Hayo mambo mengine ni kupoteza muda na rasilimali.
 
Nani anaweza kubashiri maswali atakayoulizwa???
 
hapo ndo mtihani unaopokuwa mugumu kama Nape katumbuliwa kwa ajili ya hilo tukio hapo mwakyembe anajiuliza mara mbili mbili lakini yy afanye kazi yake kama miongozo ya kiungozi unavyotaka kama mkulu akimtenda akubali matokeo kwani jamii inaona!
 
Yako wapi hayo maswali?
Hii tabia ya kukopi habari ya mbele ya magazeti nayo imekuwa too much humu ndani
Eti mkuu watu hawajui siku hizi dunia imepnuka habri unaipata popote ulipo... ACHENI KUKOPY HEADING ZA MAGAZETI.
 
Waziri wa Habari, michezo na utamaduni Dr Harrison Mwakyembe amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam ajibu maswali tisa ambayo yalipelekea kuvamia kituo cha habari cha Clouds televisheni, Mh Mwakyembe ameyasema hayo katika viwanja vya bunge wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari wa nipashe, kwamba kitendo cha Makonda kuvamia kituo cha luninga cha Clouds kitendo hicho
Katika majibu yake, Dk. Mwakyembe alisema suala hilo ni “zito” na haliwezi kuachwa lipite bila kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Huku akiendelea kuikosoa ripoti ya kamati ya Nape ambayo amekuwa akisisitiza haijakidhi matakwa ya kikatiba na kisheria kwa kushindwa kumhoji Makonda, Dk. Mwakyembe alisema Mkuu wa Mkoa huyo atahojiwa kwa mambo tisa yanayohusiana na tukio hilo.

“Hili ni suala zito maana linahusisha uvamizi ambao ni kesi ya jinai,” alisema Mwakyembe ambaye ni daktari wa sheria na Waziri wa Katiba na Sheria mpaka wiki mbili zilizopita.

“Kuna vitu tisa ambavyo upande wa pili (Makonda) utaulizwa.”

Dk. Mwakyembe hata hivyo, alikataa kuvitaja vitu hivyo tisa huku akisita pia kutaja tarehe ambayo Makonda atahojiwa.

“Upande wa kwanza (Clouds TV) tayari umeshahojiwa na ripoti tunayo. Upande wa pili nao tutauhoji na wenyewe pengine una hoja,” alisema Dk. Mwakyembe.

“Ili kukidhi matakwa ya kikatiba na kisheria, ni lazima tuuhoji upande wa pili. Hili suala kama nilivyotangulia kusema ni la jinai. Lazima mtuhumiwa apate haki ya kujitetea.
“Ukifika mahakamani, hata yule mwenye kesi ya mauaji lazima tumpatie wakili, hata kama tunao uthibitisho kwamba ameua.”

Machi 29, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari alipokaribishwa ofisi kwake mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe alisema hawezi kuikabidhi kwa wakubwa wake ripoti hiyo ya kamati ya Nape bila kuwapo na maelezo ya Makonda.

“Taaluma yangu ni sheria, hivyo siwezi kufanya jambo hilo la kupeleka malalamiko ya upande mmoja kwa mabosi zangu bila kusikiliza ule mwingine,” alisema Mwakyembe siku hiyo.

Alisema hatateua kamati nyingine ya kufuatilia jambo hilo, bali yeye na viongozi wenzake watakuwa kamati hiyo ili kuuhoji upande wa pili kisha kupeleka taarifa kwa wakuu wake ambao ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais mwenyewe.

JELA MIEZI SITA
Kamati ya watu watano iliyoundwa na Nape kuchunguza tukio la uvamizi wa televisheni ya Clouds ilibaini kuwa kiongozi huyo aliwatishia kuwafunga jela miezi sita wafanyakazi wake endapo wasingerusha kipindi alichokitaka.

Pia Kamati hiyo ilibaini Makonda aliwatisha kuwa angewaingiza wafanyakazi hao kwenye tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya kama wasingerusha kipindi chake.

Aidha, kamati ilibaini kuwa Makonda aliwatisha wafanyakazi wa kituo hicho ili wasitoe taarifa za uvamizi wake, kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Katibu wa Kamati hiyo, Deodatus Balile.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Dk. Hassan Abass, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, ni Mhariri Mkuu wa Magazeti ya The Guardian, Jesse Kwayu, Nengida Johannes wa Upendo Media na Mabel Masasi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Ilidaiwa Makonda akiwa na askari kadhaa wenye bunduki, alivamia kituo hicho na kuwalazimisha watangazaji wa kipindi cha ‘Da Wikend Show’ kurusha taarifa ya mama anayedai kuzaa na askofu Gwajima, bila ya kiongozi huyo wa kidini kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Ingawa taarifa ni ya upande mmoja, kwa mujibu wa Balile mtuhumiwa alikubali kuwaona, lakini wakati wakipanda ngazi kwenda ghorofani iliko ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala jijini, Makonda aliteremka kwa kutokea mlango wa nyuma.

hakikubaliki, hivyo anapaswa kujibu maswali kadhaa katika kuhoji upande wa pili maana kitendo hicho kimelaaniwa sana na jukwaa la wanahabari Tanzania na wadau wengine wa habari ndani na nje ya nchi.

Nipashe.
hamchoki tu??? nonsense
 
Makonda anapaswa aelewe anamfanya rais wetu aonekane kwamba hafai kumbe ni makosa ya mtendaji mmoja tu tena mjinga ambaye hajaenda hata shule yaani Bashite.
 
Kaambiwa tu aonyeshevyeti kalia,,hayo maswali atayaweza kweli?
 
Back
Top Bottom