Mwakyembe amshushua Tundu Lissu...

Mwakyembe amshushua Tundu Lissu...

Nabado

Member
Joined
Mar 31, 2014
Posts
46
Reaction score
12
Kwa mara ya kwanza kusikia akichangia bunge la katiba leo asubuhi nimejifunza mambo makuu yafuatayo.

1.Mwalimu hawawezi kukufundisha kila kitu anachokijua kwa kuwa anajua ukijua kila kitu unaweza kumzidi. Ukisikiliza namna alivyochangia utagundua kuwa Tundu Lissu alisoma vijarida tu vya sheria pale Mlimani badala ya kusoma vitabu vya sheria.
Namnukuu dr mwakyembe akihoji kitabu chake kutumiwa vibaya na tundu lissu "Mh mwenyekiti huwezi ukakisoma kitabu hiki kwa haraka haraka ukakielewa kama unavyosoma gazeti la Tanzania Daima"

2. Tundu lisu anaweza kunyanganywa degree yake wakati wowote. Akichangia leo amewataka waalimu waliomfundisha Tundu lisu kuanza kufikiria namna ya kumnyanganya tundu lisu degree yake hii ya mlimani kwani anakitia chuo hiki AIBU.

3.Maalimu Seifu hata siku moja hawezi akadai serikali tatu na ndio maana hakubaliani na wana UKAWA kuhusu serikali tatu ila yeye kasimamia kwenye hoja ya serikali ya mkataba sababu ni hii:- Akichangia leo dr mwakyembe alinukuu baadhi ya maneno ya maalimu seifu aliyowahi kuyasema na nukuu "Mh mwenyekiti unapokuwa kiongozi unatakiwa usimamie maneno yako naoma nimnukuu mh maalimu sefu maneno yake aliyokwisha kuyatoa bungeni kwamba nanukuu hatuwezi kuuvunja muungano wa tanganyika na zanzibar kwani kufanya hivyo umewarahisishia wale tuliowafukuza njia ya kurudi. Adui yao mkubwa na kikwazo kikubwa cha wao kutorudi ni muungano huu" . Katika hoja yake maalimu seifu alitahadharisha pia kuwa si kwamba muungano hauna dosari ila ni vizuri kuzitatua dosari hizo kuliko kuuvunja muungano.

4. Tundu Lisu ni MJINGA kabisa na anatakiwa arudi darasani kujifunza tena upya na ikiwezekana abadilishe fani kabisa SHERIA imemkataa.Katika uchangiaji wake dr mwakyembe alihoji kuwa hata mwananchuo wa mwaka wa kwanza anajua kuwa kama umedumu na muungano huu kwa miaka 50 na hujauhoji leo huwezi kuhoji sain au makataba wake kwani kwa muda ambao umedumu nao ni kwamba umeshaubariki kuna neno la kisheria alilitumia hapa.

5. Kuna hatari ya maproffesor na ma dk kukataa Tundu lisu asiwa wanukuu maandiko yao kutokana na kuyapotosha nafikiri hili linaruhusiwa. Atabaki kunukuu vitabu vya shigongo vya mapenzi na vya nyambari nyangwine.
 
Sikutegemea nae mwakyembea awe bomu hivyo.. Kitabu umeandika wewe..tena kwenye huo mstari umetumia neno..3 government is the ONLY way.. Leo unakana kwa sababu ya siasa za kipumbavu za ccm..kweli bongo tumelaaniwa
 
Mambo ya siasa acha kabisa. Yaani Maprofesa na wenye PhD zao wameziweka kando wanaanza kutetea ujinga! Inafika mahali mpaka Dr. Mwakyembe anakanusha kitabu chake?!
 
Hahahaaa, nasikia Mbunge wangu katukana mtu huko. Chezea Nkumba wewe Mkata viuno akiwa Secondary?

Sasa huyu Mwakyembe! Hahahaaa. Nina imani Tundu Lissu akija na athibitishe kuwa huyu ni Dr. Mwakyembe, yeye atasimama na kukana kwa kusema Tundu Lissu ni Mjinga kwani yeye siyo Dr. Harrison Mwakyembe.

Wasomi wa Tanzania wakiwa Bungeni, akili wanaziacha Msata. Ila wakifika Dodoma, Tundu Lissu anawashikisha akili nyingine. Ila wao wanaanza kukana kuwa zao wameacha Msata na hapo ndipo wanajianika wazi kuwa wakiwa Dodoma, hakuna cha Dr wala Profesa, wote wanakuwa kama Prof. Majimarefu.

Ila nawapongeza kwa hilo kwani si rahisi mtu kujivika Joho la Ujinga na kukana elimu yako yote.
 
Aliewaroga wafuasi wa ukawa ameshakufa.
Hili ni tatizo kubwa sana!
Wanahitaji dose kubwa.
 
Tundu Lissu ni mpotoshaji mkubwa sana na ni mtu hatari sana usalama, umoja na mshikamano wa nchi yetu! Ni mtu asiye na heshima na adabu kwa wakubwa zake!
Msije mkashangaa akimtukana baba yake hadharani kisa eti kadigrii kake ka sheria!
 
Sielewi nini kimemkumba Mwakyembe mpaka akawa anafuka moshi vibaya sana leo.

Mi nafikiri ameadhirika sana na ile janga lililompitia
Jason Bourne angepita hata atukumbushe tena ile sumu inavyosumbua waathirika kwa muda tena.

ccm hatari danger kwa Taifa letu!
 
Last edited by a moderator:
Kwa mara ya kwanza kusikia akichangia bunge la katiba leo asubuhi nimejifunza mambo makuu yafuatayo.

1.Mwalimu hawawezi kukufundisha kila kitu anachokijua kwa kuwa anajua ukijua kila kitu unaweza kumzidi. Ukisikiliza namna alivyochangia utagundua kuwa Tundu Lissu alisoma vijarida tu vya sheria pale Mlimani badala ya kusoma vitabu vya sheria.
Namnukuu dr mwakyembe akihoji kitabu chake kutumiwa vibaya na tundu lissu "Mh mwenyekiti huwezi ukakisoma kitabu hiki kwa haraka haraka ukakielewa kama unavyosoma gazeti la Tanzania Daima"

2. Tundu lisu anaweza kunyanganywa degree yake wakati wowote. Akichangia leo amewataka waalimu waliomfundisha Tundu lisu kuanza kufikiria namna ya kumnyanganya tundu lisu degree yake hii ya mlimani kwani anakitia chuo hiki AIBU.

3.Maalimu Seifu hata siku moja hawezi akadai serikali tatu na ndio maana hakubaliani na wana UKAWA kuhusu serikali tatu ila yeye kasimamia kwenye hoja ya serikali ya mkataba sababu ni hii:- Akichangia leo dr mwakyembe alinukuu baadhi ya maneno ya maalimu seifu aliyowahi kuyasema na nukuu "Mh mwenyekiti unapokuwa kiongozi unatakiwa usimamie maneno yako naoma nimnukuu mh maalimu sefu maneno yake aliyokwisha kuyatoa bungeni kwamba nanukuu hatuwezi kuuvunja muungano wa tanganyika na zanzibar kwani kufanya hivyo umewarahisishia wale tuliowafukuza njia ya kurudi. Adui yao mkubwa na kikwazo kikubwa cha wao kutorudi ni muungano huu" . Katika hoja yake maalimu seifu alitahadharisha pia kuwa si kwamba muungano hauna dosari ila ni vizuri kuzitatua dosari hizo kuliko kuuvunja muungano.

4. Tundu Lisu ni MJINGA kabisa na anatakiwa arudi darasani kujifunza tena upya na ikiwezekana abadilishe fani kabisa SHERIA imemkataa.Katika uchangiaji wake dr mwakyembe alihoji kuwa hata mwananchuo wa mwaka wa kwanza anajua kuwa kama umedumu na muungano huu kwa miaka 50 na hujauhoji leo huwezi kuhoji sain au makataba wake kwani kwa muda ambao umedumu nao ni kwamba umeshaubariki kuna neno la kisheria alilitumia hapa.

5. Kuna hatari ya maproffesor na ma dk kukataa Tundu lisu asiwa wanukuu maandiko yao kutokana na kuyapotosha nafikiri hili linaruhusiwa. Atabaki kunukuu vitabu vya shigongo vya mapenzi na vya nyambari nyangwine.
Mwakembe kama kweli ni jasiri ajaribu kutangaza nia ya kugombea urais,ajue kwamba safari hii hawatafanya kosa
 
Back
Top Bottom