Mwakinyo ikiwezekana badilisha uraia

Mwakinyo ikiwezekana badilisha uraia

Lile pambano na Mmalawi nia Aibu KUBWA kuwahi kutokea duniani. Jamaa alishindwa kwa mbali sana sana tu wale wataamuzi sijui nisemeje. Kwa kweli ule ni wizi wa mchana kweupe KABISA. Upande wa pamba la mwisho walisema ni SARE na ni vichekesho kwani kwa raoundi zote kuna mtu alipgwa hata chini alidondoka. Najua watu watakuja na povu lkn hakuna namna lazima tuseme kama tunataka kusonga mbele. Najua hakuna marefu yasiyo na ncha lazima siku moja kuna BONDIA atawawasha makofi hao majaji labda ndipo wataogopa

Lakini pia nakumbuka kuna siku Mwakinyo huyo huyo alipigwa wazi wazi na bondia mgeni lkn ushindi akapewa yeye.
Nakumbuka ilikuwa ni uwanja wa Taifa kama sio leaders club alipigana na mfilipino if I'm not mistaken alipigiwa kinyama

Boxing ni mchezo wa kingese ndio maana sijawahi kuupenda Huwa inaaamuliwa kidhulma dhulma sana fitna zinazo fanyika katika soccer Zina nafuu kuliko ktk boxing

Ila zile fitna za Mpira za msimu iliyopita zilizokuwa zinafanywa na waamuzi kwaajili ya kuibeba Simba mhhh Kwa kweli Ile ilivuka mipaka , itoshe tu kusema kwamba tz Kuna mambo mengi ya kingese ktk sekta ya michezo sekta ya michezo inanika Rushwa
 
Niko nimekaa naangalia eti mnaita boxing ..huu uchafu ndio boxing ? Hata anayeshinda anashangaa ameshindaje, anatangazwaje mshindi.

Wakati natafakari hayo yaliyonishangaza, picha ya Hassan Mwakinyo inanijia, kijana mtanzania alieamini katika kuipambania ndoto yake ya kua boxer wa kimataifa tena kutoka ardhi ya Tanzania, ila ni kama kila kitu kimefifia sijui, mwakinyo alipambana na amepambana kuondoa huu uchafu naoangalia hapa ili kuippeleka boxing ya Tanzania katika levels za kimataifa ila WAHUNI na WACHUMIA TUMBO walioko kwenye boxing industry waliona Kuna kidudu mtu anataka kuingilia ugali wao WA dhulma ..

Ndio mana sikushangaa kua boxer analipwa elfu 30 na hata hio elfu 30 hakuweza hata kuila akafariki. Ni mambo haya Mwakinyo alikua anapambana ayaondoe katika boxing yetu, ila alikosa watu wenye maono kama yake, nawaza kungekua na akina mwakinyo 100 hapa nchini ..huu uchafu usingekuepo..wengine tunapenda boxing ila kwa huu ujinga unaona hata aibu kuangalia ...mwakinyo ulipambana ila ni kama ulizuiwa kimakusudi..bora ubadilishe uraia ukapambanie ndoto zako nchi nyingine ambazo zitakuthamini, sio ajabu, wanamichezo wengine wanafanya wengi tu na wanafanikiwa. Angalia maisha yako, uzalendo wakati mwingine unaweza kufanya ukawa maskin zaidi badala ya kua tajiri.
Nazii
 
uzalendo wakati mwingine unaweza kufanya ukawa maskin zaidi badala ya kua tajiri.
Tanzania hakuna patriotism hata mara moja. Viongozi ni wabinafsi, wanawaza matumbo yao na ya watoto wao tu.

Asante sana Mungu kwa kunifungua macho mapema.
 
Hamna mchezo bongo unaochezeshwa kwa haki na kufata weredi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom